DELETED ACCOUNT
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 9,805
- 15,470
Baada ya mechi ya kwanza ya nusu fainali dhidi ya Al Masry, nilikumbushia kwamba Simba ina tatizo sugu la kuleta ugumu pale njia rahisi inapokuwa mbele yake.
Simba ndiyo wakali wa hizi kazi, inafuzu kwenda nusu fainali vizuri tu
Nilichokuwa nina uhakika nacho ni kuwa Simba ingeenda kusahihisha makosa nikiwa na uhakika wa kucheza nusu fainali. Na kweli hilo lilitimia, Simba ilicheza mpira mkubwa sana na kutawala mchezo ila hali ya uwanja na tatizo la kutotumia vizuri nafasi likapelekea ushindi usubiri hatua ya penati.
Simba inapoenda kurudiana na Stellenbosch baada ya kupata ushindi wa goli 1-0 ni kwamba nafasi ya Simba kufuzu ni kubwa sana. Hii ni kwa sababu matokeo mengi yanayowezekana siku hiyo yana faida kwa Simba. Matokeo ya South Africa ya 0-0, 1-1, 2-2, 2-1 Simba anavuka moja kwa moja. Hata Stellenbosch ikishinda 1-0 tunaenda kwenye matuta. Hapa utaona Simba ina nafasi zaidi ya kuvuka kuliko kutolewa.
Kwenda kwao na mtaji wa 2-0 ingekuwa bora zaidi ila pia ni kama nilivyosema kwa Al Masry, haya matokeo magumu kwa Simba yana faida zake za kuifanya timu isibweteke katika mechi ya marudiano.
Niliwahi pia kusema hawa Stellenbosch hawana mentality ya kutegemea sana uwanja wa nyumbani kama timu nyingi zenye uzoefu wa mpira wa Africa. Jinsi walivyocheza mechi ya kwanza ndiyo hivyo hivyo watacheza huko kwao. Hawa jamaa ni hatari zaidi wakiwa ugenini kuliko hata nyumbani kwao kama nikivyosema katika uzi huu.
Stellenbosch ni hatari zaidi wakiwa ugenini
Simba inahitaji kuwa na nidhamu kubwa eneo la ulinzi kama iliyoonyesha jana na kuwa na utulivu na ushirikiano kwenye kiungo na safu ya mbele. Kwa nafasi nyingi ambazo Simba inatengeneza, uhakika wa kupata goli kule kwao ni mkubwa na hawana timu ya kumfunga Simba goli 3 au zaidi ndani ya dakika 90.
Mziki tuliowachezea jana siyo wa kitoto. Ni vile tu tukio la mwisho la Ahoua limetuvuruga hadi tumesahau jinsi tulivyotawala mchezo na makanzu na matobo tuliyowapiga. Angalia sura zao baada ya mechi ya jana, wanajua ugumu wa mechi ya marudiano kule kwao.