Username 20
JF-Expert Member
- Sep 21, 2017
- 741
- 1,513
Hii mechi imekuwa na sintofahamu nyingi ni wapi itafanyika, Caf walishatoa ratiba Simba wanalijua hilo na TFF wanayo taarifa kamili ni wapi mchezo huo utafanyika
Maajabu ni kwamba Simba na TFF ni kama wanaisaidia serikali kupoteza ukweli kuwa uwanja wa Benjamin Mkapa ni mbovu sehemu ya kuchezea (pitch) kwa ubovu ule uliooneka siku ya mechi ya marudio ya robo fainali kati ya Simba dhidi ya Al Masry haingekuwa rahisi hivyo kufanya marekebisho ndani ya mwezi mmoja
Simba imewakosea sana mashabiki zake, imekubali kutumika kupoteza uchafu wa serikali,
Caf waliufanyia marekebisho makubwa uwanja wa Mkapa kwa ajiri ya African Footbali League, ajabu eti serikali tena ikatoa bilioni 30 kwa ajili ya marekebisho na ukiangalia hakuna kilichofanyika zaidi ya kurekebisha mfumo wa umeme, wifi (haifanyi kazi yoyote mpaka sasa) na kubadili viti(wametoa vya zamani ambavyo vingeweza kuendelea kutumika bado) na hapo bil. 30 ndo ikawa imeishia
Narudia tena kusema Simba imewakosea sana mashabiki wake wanajua ratiba kamili ya wapi mchezo utafanyika wamekubari kuwa sehemu ya ulaghai wa serikali na mbaya zaidi wamekuwa wakiendelea kusisitiza watu wanunue tiketi, kivyovyote vile hakuna uwezekano wa mchezo kufanyika Benjamin Mkapa na wao wanajua kwanini wameruhusu hili?
Kwa mazingira yale ya mchezo wa robo fainali mnadhani ndani ya mwezi mmoja ingewezekana uwanja kufanyia warekebisho? Uwanja ule unatakiwa kuondolewa tabaka la juu (udongo) isingewezekana ndani ya mwezi mmoja hizi ni propaganda za serikali na Simba imetumka kwenye hili, uwanja wa mkapa ni mbovu na hauna vigezo vya kuandaa mchezo wa fainali
Wacha tusubiri mda ufike Simba kwa unyonge wajifanye kama wamezulumiwa na Caf (wakati walijua mapema na ukweli wanaujua kuhusu uwanja wa Benjamin Mkapa)