Jamani nisaidieni,uzee unaanzia miaka mingapi?
Babu hapa uko sawa kabisa, haya mambo ni ya kuyazingatia sana leo waishije na kesho yapitaje............but ni stepping stone ya future hii.kwa sababu unaishi leo ukifikiria ya kesho, ikifika kesho utafikiria ya kesho kutwa maisha yanaendelea lakini kwa kuwa huna miadi na MUNGU lini anakuhitaji.huna budi kuwaza yajayo what if ukianguka ghafla leo..umejiandaandaaje? unamwachaje Mama Matesha na Matesha? Kuna akiba kiasi gani, watajisitiri wapi?? na kwa namna gani?? Uzee ndio huu.unapoifikiria kesho ni kufikiria uzee wako indirectly!! HONGERA kwa hilo.
hoja yangu ni kwamba kufunga ndoa na mtu sio mwisho wa kujenga mahusiano. tuna kazi ya kuendelea kujenga mahusiano na watu wote wakiwemo wenzi wetu siku zote hata mwisho wa maisha yetu.
kwangu mimi, fainali ni LEO!
...tusipomtegemea Mungu, kila siku tutakuwa tunajiandaa na maisha ambayo hatutakuja kuyafikia na ambayo Mungu kwa rehema zake tayari kishatuandalia na daima hutuwazia mambo mema na makubwa akitupa tumaini katika siku zetu za mwisho.
kwa majaliwa yetu wanadamu ni ngumu sana kufahamu kwa hakika yatakayotokea hata kesho tu, sembuse huko uzeeni? tunaweza kuwa makini kuchagua wenzi wa maisha, tukaridhika na assessment zetu za kibinadam tukiongozwa na macho na akili za nyama laini mwisho wake hatuwezi kuujua lolote na kwa kweli hatuwezi kitu!
Mbu post yako imenipa mawazo mengi sana,nipo late 20s naamini sijachelewa kufanyia kazi unayosema.
Nimeikubali sana hii.. Naamini moja ya akiba ya uzeeni ambayo ni kubwa kabisa ni jinsi gani ya kupigana na upweke..Hata kama ukiwa na pesa kiasi gani lakini ukiwa mpweke ni kazi bure .. Kama tuna bahati ya kuwa wawili basi inabidi tulee mahusiano yetu..yaani wawili ni wawili hata maandiko yamesema hivyo...
Ecclesiastes (Mhubiri) 4:9-12 Two are better than one, If either of them falls down, one can help the other up. But pity anyone who falls and has no one to help them up. Also, if two lie down together, they will keep warm. But how can one keep warm alone?
Bravo! Kama mtihani nakupa 110% ..yaani umetuchoma mkuki moyoni... Thanks kwa hilo
Ni kweli kabisaaaa!..Tukimweka Mungu mbele daima ..basi tutaona upendo wa kweli.. Tutapenda wake zetu, wake watapenda waume zao, tutapenda watoto na familia zetu, tutapenda majirani zetu na marafiki.. Hatutakuwa wapweke tena..Ni upendo..Love, Love, Love..
"And now these three remain: faith, hope and love. But the greatest of these is love." 1 Corinthians 13:13
Mbu;
Mbu- Ahsante kwa hii topic ambayo inatugusa sisi vijana. Wengi wetu tumejisahau kama uzee unakaribia kwa kadiri unavyolala na kuamka. Tunajiona bado tuna mda mwingi wa kutengeneza maisha bora huko uzeeni na hivyo kipato chetu cha sasa ni cha kutumbuwa kwa sasa na saving ya uzeeni ni baada ya miaka michache ijayo tutaifanya....kumbuka, pensheni yako haitokutosheleza kulipia;
1. kodi ya nyumba/chumba
2. ada ya shule kwa mwanao/wanao.
Ugumu wa maisha unaoupata sasa ni 'ishara' ya huko unakoelekea, na huenda yakazidi ugumu, upweke na ukiwa.
Wakati huo ushapoteza kazi, marafiki, na hata ndugu ulowainua kwa pesa zako za ujana. Wahenga walisema, ' mtumai cha ndugu...' Hala hala usijekimbiwa hata na wanao.
Jiwekee 'akiba'...jenga, nunua hisa kama unaamini, nunua pensheni, jiwekee bima ya afya, jipangie maisha...Muda unakuacha mkono.
Ms Judith,...tumtamainie mungu nasi tujishughulishe. Kushinda kutwa kucha kwenye nyumba za ibada i.e kanisani, msikitini... hakutatusaidia lolote, hata Mungu hapendi... ndio maana hata Ibada zina muda wake maalumu ili muda mwingine tuutumie kwenye mipangilio mingine ya maisha, ikiwamo kujenga familia zetu.
ndugu yangu mpendwa Mbu,
hapo kwenye bold umekimbia hoja kadhaa nilizozungumzia. nani kapendekeza tushindie makanisani/misikitini kutwa kucha?
kwa kweli hata ukishinda mbele ya laptop ukipanga na kupangua utakavyoishi uzeeni nako ni kazi bure!! hata ukitoa sehemu ya damu mwilini mwako uiuze ili kujiwekea akiba ya uzeeni hapa duniani nayo ni kazi bure. watu wengi huvuruga mipango yao kwa sabababu nyingi zikiwemo zile zisizotarajiwa. imagine leo una akiba ya 100m kwa ajili ya kuitumia uzeeni, lakini ukipata maradhi utagoma kuitumia kwa matibabu eti ukiusubiri "uzee" hujaona bado hapo haja ya kumtumaini Mungu?
ninachoongea ni kwamba tusijidanganye tukifikiri "we can control the future!!" na pia tusidangayane kuwa uzeeni tutakimbiwa na marafiki au kuwa ujanani ndio tuna marafiki wengi!! huo wote ni uongo mkubwa. hata leo tuna vijana wengi sana wapweke, wale wenye marafiki wamshukuru sana Mungu na sio wajishukuru wenyewe. hata leo vilevile tuna wazee wengi sana wenye marafiki wengi hata kushinda vijana wa leo, nao wamshukuru Mungu, na sio kujishukuru wao.
tujifunze kumtumaini Mungu na kumshukuru kwa kila jambo analotujaalia maishani. planning is just a theory na theories zote ni mawazo ya kibinadamu tu hata zingekuwa zimenyooka kiasi gani, zina limitations chungu mzima.
lets trust in the Lord wapendwa!
Glory to God!
...Chauro mydear, nakuombea hayo mawazo yawe yenye changamoto, siyo msongo utaokufanya upoteze raha.
Ni wachache wetu tunaotumia muda mchache kusikiliza na kuuzingatia "utabiri wa hali ya hewa."
Kumekucha jamani, shime tukajiandalie pensheni zetu...fainali Uzeeni.
Tunavyowapiga vikumbo wastaafu wa Jumuiya ya Africa mashariki, na hata wengine kuwadhihaki, ina maana hatukumbuki ipo siku nasi twaweza angukia
kwenye mzunguko huo huo. Mwenye macho haambiwi ona, na mwenye masikio halazimishwi sikiliza.
What goes around comes around.... Usipojiwekea akiba ya uzeeni, ujue unachezea shilingi chooni.
Tujiandae! Ujana ni moshi...unafuka huoooo wenda zake!...kufumba na kufumbua utajikuta marafiki wanapungua
kwa rate ya mafungu ya 10%...na kujikuta mkiwa...
Je, umejiandalia nini uzeeni? Una japo kibanda cha kujistiri? au unabahatisha maisha wewe? wanao ni Insurance, lakini pia usiitegemee 100% ipo siku watakusaidia....Jiandaee...fainali uzeeni!
...Maisha ya uzee ni ukiwa!...story zako hazitakuwa na mvuto tena. Twaona wazee wengi wa miaka ile wamepitwa na wakati. hawawezi hata kuwapigia hata hadithi wajukuu sababu ya hizi Big Brother, Egoli, etc... watoto wa kisasa hawadanganywi na hadithi za sungura na fisi...
Old age is like everything else. To make a success of it, you've got to start young.
When marrying, ask yourself this question: Do you believe that you will be able to converse well with this person into your old age?
Everything else in marriage is transitory.
anza sasa kujijengea mahusiano mazuri na mkeo uwe na mtu wa kujifariji nae miaka hiyo ya ukiwa, ....fainali uzeeni!
Kwani huko uzeeni tutafika? After all kuishi kwingi ni kwa vile mtu una matunzo mazuri, kama hayapo unakitoa soon after........ Why bother on earth!!!!!!!!!!!!!!
Miss Judith bana..... Unasemaje huwezi icontrol future wakati kwa siku 29 za mwezi waenda kazini kuihangaikia kesho? Kwani future inaanzia lini?
Miss Judith bana..... Unasemaje huweziicontrol future wakati kwa siku 29 za mwezi waenda kazini kuihangaikia kesho? Kwani future inaanzia lini?