Faili la Nassari mtihani tosha kwa DPP

mwinukai

JF-Expert Member
May 3, 2011
1,447
630
Ni mafaili mengi sana yamepelekwa kwa DPP lakini mpaka leo hayajapatiwa ufafanuzi na kuchelewa huko kama kuna fanya matukio hayo kuanza kusahaulika mafaili ya EPA toka 2008, mafaili ya yaliyodaiwa kupelekwa na Dr. Hosea kuhusu ufisadi, Faili la Sitta kuhusu uchochezi ni miongoni mwa mafaili ambayo yapo ofisini mwa DPP. Mara nyingi kuchelewa huko kumekuwa kukitafsiriwa kuwa ni kwa sababu mrundikano wa mafaili katika ofisi ya DPP.



Faili la Nassari kupelekwa katika ofisi hii ni mtihani tosha, kama ofisi hii haiburutwi na CCM basi mafaili ya mwanzo yatapatiwa ufafanuzi kwanza kabla ya faili hili la Nassari. Lakini kama ofisi hii inaburutwa na CCM basi tutegemee faili hili la mwisho likawa la kwanza kushughulikiwa
 
Back
Top Bottom