Maoni yangu kwa Tume ya Kupitia Taasisi za Haki Jinai: Mamlaka ya DPP kwenye Makosa ya Uhujumu Uchumi yapunguzwe

Mgeni wa Jiji

JF-Expert Member
Jul 27, 2017
7,901
13,339
Salamu wana JF,

Katika kuweka mizani ya utawala na utendaji wa haki nchini sawa tumeona Rais akiunda na kuituma kazi Tume ya kupitia utendaji wa taasisi za haki jinai, hili ni jambo zuti hasa tukiangalia Tume hii imeundwa kwa wingi na watu waliofanyakazi katika mfumo wa haki jinai, ingawa wapo walioibeza kuwa haitaweza kurekebisha jambo kwani ni hao hao lakini tukumbuke uzoefu ndie mwalimu mzuri

Baada ya utangulizi huo mfupi niende moja kwa moja kwenye msingi wa uzi huu.

Uzi huu ni mapendekezo yangu kwa Tume hii iliyoundwa na Mheshimiwa raisi, kwakuwa sitaweza kuonana nayo ana kwa ana basi naona vema nikawasilisha mapendekezo yangu haya hapa JF naamin watayapata pia.

Mapndekezo yangu ni juu ya Mamlaka aliyopewa Mundesha mashitaka Mkuu wa Serikali yaan DPP katika kufungua, kuendesha na kuhitimisha kesi za uhujumu uchumi.

Binafsi niseme amlaka haya ni makubwa mno na pia mamlaka haya yanakinzana na Katiba ya Jamhuri kwa kuingilia Mamlaka ya Mahakama ya Tanzania.

Ofisi ya DPP ipo kikatiba na mamlaka yake yamewekwa na Katiba ya Jamhuri pamoja na sheria nyinginezo. Hapa nitaiongelea Sheria ya uhujumu uchumi na magenge ya uhalifu (EOCCA).

Hii sheria imempa DPP mamlaka ya kuamua ni Mahakama ipi ikasikilize kesi ya uhujumu uchumi, hapa tukumbuke kuwa tayari ipo sheria inayosema na kuipa mamlaka Mahakama Kuu kuwa Mahakama pekee ya kusikiliza kesi hizo, lakini DPP anao uwezo wa kuamua kesi ya uhujumu uchumi ikasikilizwe Mahakama zilizo chini ya Mahakama Kuu.

Haya ni Mamlaka makubwa sana na pia ni mamlaka yanayokinzana na Katiba ya Jamhuri inayotamka kuwa Mahakama ni chpmbo huru. Kwa DPP kuwa na mamlaka ya kuipokonya Mahakama mamlaka yake na kuamua kesi fulani kuipeleka Mahakama za chini ya Mahakama Kuu sio tu ni kuingilia uhuru wa Mahakama bali pia ni uvunjwaji wa Katiba ya Jamhuri.

Jambo la pili ni Mamlaka ya kutoa cheti kuruhusu mtu kushitakiwa kwa makosa ya uhujumu uchumi. Haya nayo ni mamlaka makubwa sana aliyopewa DPP, yaani ni kwamba bila DPP kuruhusu mtu kushitakiwa kwa kosa la uhujumu uchumi mtu huyo hawezi kushitakiwa kwa kosa hilo na kama atashitakiwa bila kuwepo kwa cheti hicho basi hukumu na mwenendo wa kesi hiyo ni batili.

Hebu fikiria, makosa ya uhujumu uchumi yapo na yanajulikana lakini haiwezekani kushitakiwa mtu kwa makosa hayo hadi DPP aruhusu mtu huyo kushitakiwa. Je asiporuhusu?. Je kama mtuhumiwa ni swahiba wa DPP?

Hali hizi mbili zinafanya kesi na makosa ya Uhujumu uchumi kuonekana kama kesi na makosa ya kisiasa kwani DPP amepewa mamlaka ya ziada zaidi hadi ya kuipa Mahakama Mamlaka ya kushitaki.

Ikumbuke kuwa DPP naye anatetea upande katika kesi ambao ni Jamhuri, sasa mamlaka haya ni sawa na Jamhuri inatafuta uwanja mzuri wa wao kuendeshea kesi yao.

Maoni yangu ni kuwa mamlaka haya yaondolewe kwa DPP kwani;

1. Mamlaka ya Mahakama hayaamuliwi na wahusika katika kesi.

2. Mahakama Kuu divisheni ya makosa ya rushwa na uhujumu uchumi ndio Mahakama yenye mamlaka ya kusikilizana kuamua makosa ya uhujumu uchumi.

3. Kuwepo kwa cheti kinachotolewa na DPP kukubali mtuhumiwa kushitakiwa kwa makosa ya uhujumu uchumi ni sawa na kumhukumu mtuhumiwa kuwa mhujumu uchumi.

Kwa leo nitaishia hapa na naamini wapo wataalamu wengine wa sheria wamekwishaliongelea swala hili nyakati tofauti tofauti, na sasa ni muda mamlaka haya yakaangaliwe upya yasije yakatokea yanayoendelea kuhusu utendaji wa DPP aliyepita.

Shukrani Wakuu.
 
Back
Top Bottom