Faida za Kiafya za Kitunguu Swaumu (Garlic) Featured | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Faida za Kiafya za Kitunguu Swaumu (Garlic) Featured

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Jul 9, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 9, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,608
  Trophy Points: 280
  [​IMG]  ​Kitunguu swaumu ni jamii ya vitunguu ambayo kwa kitaalamu huitwa Allium sativum. Jamii hii ilianza kutumika katika mabara mbalimbali duniani hususani Asia, Afrika na Ulaya takribani miaka 6000 iliyopita. Matumizi makuu nyakati hizo yakiwa viungo katika mboga na tiba.


  Kitunguu swaumu kimetajwa kwenye vitabu mbalimbali vya dini vikielezea faida zake katika kutibu maradhi mbalimbali yasababishwayo na bakteria, matatizo katika mapafu, matatizo katika mfumo wa umen'genyaji chakula, na matatizo ya kuishiwa nguvu.


  Historia inaonesha kuwa, vitunguu swaumu vilianza kutumika China mwaka 510 K.K na pia vilitumiwa na wanajeshi wa Ugiriki na Roma. Aidha wasafiri wa vyombo vya baharini na vijijini pamoja na wakulima barani Afrika walivitumia sana.


  Mwaka 1858, mtafiti na mwanasayansi wa nyakati hizo, Louis Pasteur aligundua uwezo wa kitunguu swaumu katika kuua vimelea mbalimbali vinavyosababisha magonjwa, na hivyo vikaanza

  kutumika kama dawa ya kusafishia vidonda na kuzuia kidonda ndugu hasa zama za vita ya kwanza na pili ya dunia. Isitoshe, mpaka sasa zipo dawa kadhaa zilizotengenewa kwa kutumia jamii hii ya

  vitunguu swaumu ikiwemo dawa ya kusafisha mdomo (mouth wash) ingawa watumaiji wake wengi huilalamikia dawa hiyo kwa sababu ya harufu mbaya ya dawa hiyo inayowasababishia kunuka kwa mdomo.  Faida za vitunguu swaumu


  Katika tafiti mbalimbali vitunguu swaumu vimeonekana kuwa na uwezo wa kutibu maambukizi ya bakteria, fangasi na virusi vya aina mbalimbali. Aidha husaidia kuzuia magonjwa ya moyo ikiwemo kuondoa lijamu katika mishipa ya damu na hivyo kusaidia katika kurekebisha shinikizo la damu. Faida nyingine za vitunguu swaumu ni pamoja na

  • Kutibu saratani ikiwemo saratani ya tumbo na utumbo mkubwa. Tafiti zinaonesha idadi ndogo ya wagonjwa wa saratani katika nchi ambazo wakazi wake wana utamaduni wa kutumia vitunguu swaumu kwa wingi.
  • Vitunguu swaumu husaidia kudhibiti kiwango cha sukari katika damu. Hata hivyo inashauriwa kwamba wagonjwa wa kisukari wanaotumia sindano za insulin wasitumie kitunguu swaumu kwa wingi mpaka watakaposhauriwa na daktari.
  • Huzuia kusanyiko la chembe sahani zinazosaidia kuganda kwa damu (platelet aggregation)
  • Husaidia ufyozwaji wa thiamin, hivyo kusaidia kuepusha mwili na ugonjwa wa beriberi
  • Ina kiasi kikubwa cha vitamini C ambayo husaidia kuzuia ugonjwa wa kiseyeye
  • Hutumika kutibu magonjwa nyemelezi kama toxoplasmosis, hasa kwa watu wenye upungufu wa kinga mwilini.

  Ushahidi wa Kitafiti


  Katika utafiti uliofanyika nchini Czech ilionekana kuwa matumizi ya vitunguu swaumu yalisaidia sana katika kupunguza kusanyiko la lijamu (cholesterol) pamoja na mafuta yasiyofaa mwilini (low

  density lipoproteins) katika mishipa ya damu. Aidha, mwaka 2007 BBC iliripoti matumizi ya vitunguu swaumu katika kusaidia kumkinga mtumiaji dhidi ya aina fulani ya mafua

  iliyosababishwa na virusi. Mwaka 2010, ulifanyika utafiti mwingine ambao ulijumuisha wagonjwa 50 wenye shinikizo la damu sugu ambalo lilikuwa ni vigumu kudhibitiwa hata kwa matibabu

  yaliyozoeleka ya dawa na njia nyingine. Kama njia ya kuchunguza ufanisi wa vitunguu swaumu katika kutibu shinikizo la damu, baadhi ya wagonjwa hao walipewa vitunguu swaumu wakati

  wengine walipewa dawa isiyohusika na matibabu ya shinikizo la damu (au placebo). Ilionekana kuwa wale waliopewa vitunguu swaumu kama dawa ya shinikizo la damu walionesha maendeleo

  mazuri kwa vitunguu swaumu kuweza kushusha vizuri kiwango cha shinikizo la damu, hususani systolic pressure, tofauti na wale waliopewa placebo.  Nini siri ya kitunguu swaumu?


  Sifa kuu zinazokifanya kitunguu swaumu kuwa na uwezo na faida zilizoainishwa hapo juu ni kule kuwa kwake na viasili kadhaa (ingredients) ambavyo vinafanya kazi tofauti tofauti. Uwezo wake wa kiutendaji unatokana na mambo yafuatayo;

  • Vina uwezo wa kusababisha kutanuka kwa mishipa ya damu (vasodilation) kwa kubadilisha polysulfides zilizopo ndani yake kuwa hydrogen sulfides kwenye seli nyekundu za damu.
  • Husaidia uthibiti wa kiwango cha sukari mwilini kwa kushusha kiwango cha kemikali ya homocystine na kupunguza madhara ya kisukari.
  • Iwapo vitapondwa pondwa vizuri, vitunguu swaumu hutoa kemikali iitwayo Allicin ambayo ni dawa dhidi ya bateria, na phytoncide ambayo huua fangasi wa aina mbalimbali.
  • Harufu mbaya ya kitunguuu swaumu hutokana na gesi aina ya hydrogen sulfide ambayo inayotolewa baada ya kuvila.


  Nini Madhara ya vitunguu swaumu?  Ukiacha faida zake, vitunguu swaumu pia vina hasara na madhara mbalimbali kwa mtumiaji. Madhara hayo ni pamoja na;

  • Harufu mbaya mdomoni ambayo hutokana na kemikali ya AMS (allyl methyl sulfide). Harufu mbaya hii, hata hivyo, yaweza kupunguzwa kwa kunywa maziwa au kunywa maji mengi.
  • Kwa baadhi ya watumiaji, vinaweza kuwaletea mzio au mcharuko mwili (allergies au inflammatory reactions)
  • Kichefuchefu, Kutapika na kuharisha.
  • Huweza kusababisha hatari ya kuvuja damu, kwa sababu huzuia kazi ya seli sahani (platelets) zenye kusaidia kuganda kwa damu kushindwa kufanya kazi yake vizuri, na hususani kwa mama wajawazito, baada ya upasuaji au mara baada ya kujifungua.
  • Huingiliana katika utendaji kazi wake na dawa kadhaa kama vile warfarin, antiplatelets, saquinavir, dawa za shinikizo la damu kwa ujumla hasa calcium channel blockers, na antibiotiki za jamii ya quinolone kama vile ciproflaxacillin.
  • Aidha, vinaelezwa pia kuwa na madhara kwa wanyama jamii ya paka na mbwa.
   
 2. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #2
  Jul 9, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Santee..
  Ingawa nimesoma faida tu...
   
 3. Daffi

  Daffi JF-Expert Member

  #3
  Jul 9, 2011
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 160
  NIMEIPOKEA,thanks
   
 4. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #4
  Jul 9, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  nipoa mkuu je inakuwaje ukiweka kama kwenye upele ili uive ina maaana hakuna madhara mengine baada ya uvimbe kuwa umeisha pasuliwa..
   
 5. zaratustra

  zaratustra JF-Expert Member

  #5
  Jul 9, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 849
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Nashukuru kwa habari hii ya vitungu swaumu. Mimi ni mmoja wa watumiaji wazuri wa "dawa" hii tangu muda mrefu baada ya kuambiwa na rafiki yangu mmoja mzungu kuwa inasaidia sana kutibu mafua (niko allergic na moshi (hasa wa sigara), vumbi, perfume zenye harufu kali, hata maji ya baridi ya kuoga). Sijui kwa maelezo ya mleta thread, inatumiwaje kama tiba? Mimi nilishauriwa kuwa nameza nzima nzima kisehemu kimoja cha kile kitunguu, at least kila asubuhi kabla ya kutia chochote tumboni! Je kuna namna nyingine, eg. kutafuna, kumung'unya, n.k.?
   
 6. Jeji

  Jeji JF-Expert Member

  #6
  Jul 9, 2011
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 1,981
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Asante kwa kutuelimisha, nilikuwa sijui.
   
 7. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #7
  Jul 10, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,913
  Likes Received: 214
  Trophy Points: 160
  Mkuu hii ya kumeza chembe nzima bila kuitafuna matokeo yake huwa ni kutoka kikiwa kizima vile vile kwa kupitia njia ya haja kubwa. Ninakushauri ujaribu kukitafuna kabla hujakimeza, hii itasaidia kurahisisha mmeng'enyo wake tumboni.
   
 8. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #8
  Jul 11, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,055
  Likes Received: 6,495
  Trophy Points: 280
  Asante sana.
   
 9. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #9
  Jul 11, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Thank you for the useful information!
   
 10. Kivumah

  Kivumah JF-Expert Member

  #10
  Jul 11, 2011
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 2,413
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Asante Mzizi
   
 11. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #11
  Jul 12, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  nanikinga kubwa ya kipindupindu niliwamsikia dr ndodi
   
 12. Mgariga

  Mgariga Senior Member

  #12
  Jul 12, 2011
  Joined: Apr 1, 2011
  Messages: 176
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  very useful information, great indeed.
   
 13. upele

  upele JF-Expert Member

  #13
  Jul 12, 2011
  Joined: Mar 3, 2010
  Messages: 365
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  be blessed mwana yeeah yap i like jf
   
 14. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #14
  Oct 21, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,608
  Trophy Points: 280
  KITUNGUU saumu kimekuwa kikitumika kutibu na kuboresha afya ya mwili na hivyo kumfanya mtumiaji awe mrembo na mwenye afya bora.
  Matumizi ya kitunguu saumu kibichi yamekuwa yakisaidia vitu vingi sana mwilini.

  Baadhi ya hayo ni pamoja na kupambana na virusi, bakteria, fangasi na pia sumu mbalimbali hasa zile zinazosababishwa na baadhi ya vyakula mwilini.

  Kutokana na hilo, matumizi ya kitunguu saumu kama tiba na kipodozi, ni jambo linalopendekezwa na wataalamu wa urembo wa asili.
  Katika matumizi yake kitunguu saumu hutumika kwa kula na wakati mwingine kupaka, ambapo hili hutegemea zaidi na mahitaji au matatizo ya mtumiaji husika.

  Pamoja na njia hizo nilizotaja hapo juu, lakini wataalamu wanashauri ulaji wa kitunguu saumu kibichi kila siku, kwani husaidia kuboresha afya ya muhusika.

  Ikiwa utashindwa kukitafuna chenyewe, unaweza kuchanganya kwenye chakula kingine ambacho unatumia alimradi tu ukipate kikiwa halisi.
  Kwenye urembo, kitunguu saumu husaidia kuondoa matatizo yafuatayo;
  Chunusi

  Changanya kitunguu saumu kilichosagwa kijiko kimoja na kijiko kimoja cha juisi ya ndimu. Chukua pamba na paka sehemu zote zilizoathirika. Kaa na mchangyiko huo kwa muda wa dakika 15 hadi nusu saa.Ikiwa utaendelea kwa muda wa wiki moja. Tatizo la chunusi litakuwa limeondoka kabisa.

  Kunyonyoka kwa nywele

  Ni kwa muda mrefu sasa kitunguu saumu kimekuwa kikitumika kama tiba ya kunyonyoka kwa nywele. Unachotakiwa kufanya ni kutumia mafuta yake kwa kupakaa kwenye ngozi ya kichwa kila siku kabla ya kulala.
  Fanya hivyo mara kwa mara kwa muda usiopungua miezi mitatu na utaona matokeo yake. Ikiwa utakosa mafuta yake, si vibaya ikiwa utatumia kitunguu chenyewe kilichosagwa kwa kupaka kwenye ngozi ya kichwa kila siku usiku na kuosha asubuhi yake.

  Fangasi vidoleni

  Kupambana na fangasi kwenye vidole vya miguu na mikono, unashauriwa kutumia kitunguu saumu kilichosagwa kwa kupaka eneo lililoathirika. Hakikisha unakaa nacho usiku kucha ukiwa umevaa soksi ama glavu. Fanya hivyo kila siku hadi utakapoona muwasho na maumivu yameisha.

  Mba

  Paka kitunguu saumu kilichosagwa katika ngozi ya kichwa ama sehemu yeyote iliyoathirika. Hakikisha unatumia hadi pale ugonjwa utakapokuwa umetoweka kabisa.
   
 15. m

  majogajo JF-Expert Member

  #15
  Oct 23, 2011
  Joined: Oct 9, 2011
  Messages: 321
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  kwa nguvu za kiume je?
   
 16. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #16
  Oct 24, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,608
  Trophy Points: 280
  Mbona nimeandika Dawa nyingi tu za nguvu ya Kiume? Unataka Dawa ya nguvu ya Kiume wewe? haya chukuwa hii hapa Chukua Mdalasini pamoja na asali uchanganye kwa pamoja atie na maji ya Uvuguvugu , halafu kila chakula chako kisikose kipande cha tango..

  Sababu 9 muhimu zinazo sababisha upungufu wa nguvu za kiume
  Zipo sababu nyingi zinazosababisha wanaume kupungua nguvu za kiume katika hizo ni hizi zifuatazo:
  1.ubugiaji wa tumbaku .
  2.uvutaji wa sigara.
  3.utafunaji wa mirungi.
  4.unywaji wa pombe.
  5.kupooza kwa mwili kunakosababishwa na maradhi.
  6.ugonjwa wa kisukari.
  7.kujisaidia kwa njia ya mkono. (Punyeto)
  8.kuwa na mawazo kupita kiasi.
  9.kufanya kazi ngumu.

  TIBA YAKE:
  chukua mbegu za tikiti maji zikaange halafu zitwange ili zitoe unga, chukua juici ya kitunguu thaumu lita moja na asali lita moja changanya pamoja juisi ya kitunguu thaumu na asali weka na vijiko kumi vikubwa vya unga wa tikiti maji koroga vizuri na uwe unakunya dawa hii kikombe kimoja cha kahawa mara tatu kila siku kwa muda wa wiki moja.

  Chanzo: Mzizimkavu

  [​IMG]


  Namna kujitibu maradhi ya kuwahi kushusha manii haraka wakati la tendo la ndoa na bila kujitibu wanaathirika wote khususan mwanamke.
  Madawa yake ni:

  1.Tangawizi.
  2.Uwatu.
  3.Asali.
  4.Mdalasini.

  Chukua unga wa tangawizi kiasi cha vijiko vitatu vya chakula kisha changanya na dawa iitwayo uwatu unga wake kiasi cha vijiko vitatu vya chakula, na hakikisha madawa haya ni ya unga yaani yatwange hadi yawe unga kisha chemsha kwa maji glasi tatu baada ya kuchemsha hakikisha

  glasi moja inapotea kwa kuchemsha, halafu mgonjwa wa tatizo hilo atakuwa akijipaka kwenye dhakari yake na kwenye korodani kila siku mara moja na wakati anatumia dawa hiyo itamlazimika atumie asali kijiko kimoja c
   
 17. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #17
  Nov 2, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,608
  Trophy Points: 280
  Garlic: Bad for Your Breath, Good for Your Brain


  [​IMG]  Garlic is known to be a breath destroyer, but is it possible that what’s known as the stinking rose could help stave off dementia? In the quest to find a potential cure and treatment for Alzheimer’s disease, a by-product of garlic called aged garlic extract was recently studied on mice and it showed some serious promise. Alzheimer’s disease, the most common form of dementia and now the 7th leading cause of death in the United States, results from the deposit of proteins called amyloid-beta protein peptides that can cause inflammation and form plaque in the brain.


  The available drugs today only treat the symptoms, so serious efforts are underway to search for a cure, or at least to stop the disease progression. Currently, treatment costs associated with Alzheimer’s disease are climbing and therefore, cheaper, natural food substancesfor treatment drugs are being investigated worldwide. One of such substances being tested is garlic. When reviewing preliminary results of various animal and laboratory studies

  involving aged garlic extract and one of its key compounds, S-allyl-L-cysteine, garlic extract treatment showed protective effects against inflammatory process and chemical changes in the brain that occur in Alzheimer’s disease patients. In the study on mice, the four-month-long treatment with aged garlic extract decreased the number of plaques in their brains.


  Where does this extract come from? Garlic has sulfur-containing compounds that can be unfavorable and undesirable. When garlic is soaked in ethanol-water mixture for 20 months, unfavorable compounds are destroyed and useful ones become soluble resulting in aged garlic extract, which it contains S-allyl-L-cysteine or SAC.


  Thus far, studies conducted in the area of Alzheimer’s disease and potential benefits of treatments with natural food substances are still conflicting. While more research is in dire need, researchers are hopeful that remedies including garlic and curcumin (turmeric) are potentially beneficial in the treatment of

  Alzheimer’s disease. Like garlic, curcumin also has shown to help alleviate all types of inflammation, helping to fight various intestinal diseases or even slow down cancer growth.

  So while further human studies need to be done to verify and expand on these results, it wouldn’t hurt you to add some fresh garlic to your spaghetti tonight or pop an aged garlic extract supplement pill. Just remember to buy some breath mints, too.


  Active Ingredient in Aged Garlic Extract Studied on Mice for Effect on Alzheimer’s Disease


  Summary
  Alzheimer’s disease is the most common form of dementia in older people and the 7th leading cause of death in the United States. Years before symptoms of Alzheimer’s disease appear, peptides called amyloid-beta start depositing in the brain. This results in destabilization of microtubules that are responsible for transportation of cellular material, as well as swelling in the brain. The swelling causes damage to neurons and neuronal networks, resulting in dementia in older people. The available treatments do not completely cure Alzheimer’s disease, and new drug targets are being investigated. Garlic extract and S-allyl-L-cysteine (SAC), a component present in the extract, were tested for their effect on neuronal degeneration related to Alzheimer’s disease on mice.


  Introduction
  The proportion of elderly population with Alzheimer’s disease is increasing worldwide. Three main features of this disease are: deposition of amyloid-beta peptides causing brain inflammation that damages neurons; chemical changes in tau protein affecting cellular transport via microtubules; and loss of neurons releasing acetylcholine that controls the functions of heart and muscles. The available drugs that target single steps in the progression of the

  disease can provide some symptomatic relief, but these drugs cannot control or cure the disease. “We hypothesize that an agent effective in modulating multiple pathological pathways could be an appropriate therapeutic agent in preventing and restricting Alzheimer’s disease progression.” Natural substances such as garlic and turmeric are tested because of their low costs, easy availability and fewer possible side effects. Garlic affects different aspects of the progression of the disease, showing the potential to be a possible cure for Alzheimer’s disease.


  Methods

  * Garlic has sulfur-containing compounds that can be unfavorable. When garlic is soaked in ethanol-water mixture for 20 months, unfavorable compounds are destroyed and useful ones become solubilized. The result is aged garlic extract (AGE) and it contains S-allyl-L-cysteine or SAC.
  * In vitro and in vivo studies were performed on mouse and rat models of Alzheimer’s disease using these extracts.
  * The changed chemical status (phosphorylation) of tau protein was tested in mice with Alzheimer’s disease treated with or without AGE and SAC.
  * The chemicals that increase upon inflammation were recorded.


  Results

  * In vitro studies with SAC showed that it can dissolve amyloid-beta plaques. In vivo, four-month-long treatment with AGE and SAC decreased the number of plaques in the brains of mice.
  * Mice with Alzheimer’s disease showed tangled neuronal microtubules due to chemical changes in tau protein. The treatment with AGE and SAC showed decreased levels of the changed tau protein.
  * Garlic extract treatment showed increase in the levels of glutathione, an enzyme that protects neurons from inflammatory agents.
  * The changes in various other factors seen in the disease improved with AGE or SAC treatment.


  Shortcomings/Next steps

  Authors recommend more research and have confirmed that the “current FDA-approved drugs for the treatment of Alzheimer’s disease fail to completely cure the disease.” Most of the new drugs that have been tried in clinical trials have failed to demonstrate definite curative effects in these trials. The authors also propose a combined formulation of curcumin with AGE or SAC, which can produce synergistic properties to alleviate the pathology of Alzheimer’s disease, and its associated symptoms, and these types of combinations would also require further research in preclinical and clinical settings.


  Conclusions

  The numbers and cost of treatment of patients with Alzheimer’s disease is increasing, emphasizing the need for a cheaper and more successful new treatment. The authors suggest that the failure to find a cure is because of the multi-faceted nature of this disease. A drug will have to address all these

  aspects of the pathology to prove to be successful as a treatment for Alzheimer’s disease. The ingredients present in AGE seem to reduce the chemical changes in proteins affecting transport in brain cells, and also affect many aspects of interconnected chemical pathways to reduce swelling in the brain. While more research is needed, remedies such as garlic and curcumin (turmeric) are potentially beneficial in restricting the symptoms of Alzheimer’s disease.
   
 18. kashengo

  kashengo JF-Expert Member

  #18
  Apr 23, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 2,632
  Likes Received: 449
  Trophy Points: 180
  Thank yuo MZIZI MKAVU
   
 19. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #19
  Apr 23, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,608
  Trophy Points: 280
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #20
  Apr 23, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,608
  Trophy Points: 280
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...