Faida na hasara za ukuaji wa intaneti Tanzania

Wangoto jr

Member
Jul 18, 2022
7
3
Utangulizi

Internet ni
chombo mhimu sana kwa dunia ya sasa, kwasababu mambo mbali mbali kama biashala, ajila, matangazo, kusoma, na kufundishia tunatumia internet.

1. Faida za internet kwa jamii

(i) ajira. Hapo zamani ili uwezu kutuma maombi ya ajila/kazi ilkua ni lazima utembee na vyeti kibao pamoja na balua mkononi upeleke kwa waajili . rahasha kwa sasa kulingana na ukubwa wa internet watu tuna ambatanisha kila kitu kupitia internet na kuvituma kwa wa ajili bila ghalama za nauli bila hata usumbufu wa ofice kufungwa.

(ii) biashara. Kwa upande wa wafanya biashala wana nufaika kwa namna moja au nyingine kwa kupitia kutumia mitandao ya kijamii mtu unaweza uza au kutangaza biashala yako bila ghalama yeyote na watu waka ijua.

(iii) Upatikanaji haraka wa habari. Hapo zamani ili uweze jua mengi yanayo jili ulimwenguni kote ilikua inakuladhimu usikilize redio au uangalie television lakini kwa sasa kila kitu kinganjani mwako .

2. Hasara ya internet kwa jamii

(i) kuvunjika kwa maadili.
Kupitia kukua kwa internet watu wengi tumekua wahanga kwa kuinga mila na tamaduni za ughabuni kupitia hili tunakuta asilimia kubwa ya dadazet sikuhizi wamekua wahanga wakubwa kwenye hili, hususani kwenye mavazi ambayo haya madili hata kidogo.

(ii) Maudhui mtandaoni. Kupitia ku kidhili kwa matumizi ya mtandao wa Instagramu tz, watu wengi kama waganga wa kienyeji wamekua wakitumia fulsa hiyo kutangaza bidhaa zao kama vile madawa ya nguvu za kiume hilo si tatizo , lakini tatizo wale wanao weka hayo matangazo ya hizo bidhaa wengi wao wanaweka picha ambazo hazina afya kwa watumiaji wengine wa intarnet.

(iii) Ueneaji wa talifa potoshaji kwa jamii. Kulingana na kukua kwa nyanja ya intarnet Tanzania watu wengi wamekua wakitafuta umaalufu kwa nguvu iwe hata kwa kumkwaza mtu mwingine , kwa mfano mtu unakuta kaandika andiko la kumchafua kiongozi yeyote wa serkali ili watu wengi wa fuatilie hiyo taalifa (mange kimambi app) ni kati ya app ambayo huchapisha maudhui mbalimbali ya watu bila ridhaa yao mwisho wasiku wata wana dhalilika kupita yeye.

Mwisho: Matumizi ya intarnet ni ya muhimu kwa taifa la sasa lakini yazingatie zaidi kwenye mambo chanya🙏🏾
 
Back
Top Bottom