Fahamu zaidi kuhusu Jua la utosi

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Habari wanaJF,

Machi 21 inaaminika kuwa ni siku ambayo Jua (The Sun) linapita sawia na mstari wa kubuni wa kijiografia wa Ikweta. Kwa mnasaba wa tukio hilo siku hii huitwa "Siku ya Jua la Utosi".

Tukio hili la kipekee ambalo kijiogrofia huitwa "Equinox" hutokea mara mbili kwa kila mwaka, Machi 21 na Septemba 23. Siku zote hizo huwa ni siku za Jua la utosini.

Nilipokuwa mwanafunzi wa shule ya Msingi Mwalimu wetu wa jiografia kila siku kama hii alikuwa anatukumbusha anatusimulia, na kutufafanulia namna jua linapokuwa sawia na mstari wa kubuni wa Ikweta.

Ili tusisahau na tuelewe vizuri kuhusu "Equinox" basi inapotimu SAA 6:00 mchana hututoa nje ya darasa na kutupeleka kwenye Kiwanja cha wazi kisha kila mmoja husimama eneo lake na kuangalia kivuli chake kuona namna ambavyo jua linammulika sawia utosini. Tulijikuta tukiipenda kuishiriki siku ya Jua la Utosi. Sina hakika kama na wanafunzi wa zama hizi wanafanya hayo tuliyokuwa tukifanya sisi.

index.jpeg

Kimsingi hiyo ilitusaidia sana kuelewa vizuri siku Jua linapokuwa katika Tropiki ya Ikweta (Machi 21 na Septemba 23), linapokuwa Tropiki ya Kansa (Juni 21) na linapokuwa Tropiki ya Kaprikoni (Desemba 22).

Haikutuhitaji kusoma na kukariri kuhusu hili bali tulielewa na kutekeleza.

Mafunzo kwa vitendo huwa yana faida zake. Mojawapo ni hii mpaka leo bado naendelea kuzikumbuka hizi siku.
 
View attachment 331397

umetukumbusha mbali. zamani shule ya msingi ilikuwa raha,miaka ya 70 kwenda 80. asante mkuu
 
Ahsante saanaa..yaani kama namuona mwalimu wangu wa Jiografia aisee! Na umenikumbusha mambo ya tropiki hizo tarehe nilikua nshazisahau
 
Back
Top Bottom