hydroxo
JF-Expert Member
- Oct 19, 2015
- 3,247
- 6,767
1.Wakati mwanadamu anatumia ulimi kutambua ladha ya vyakula na vitu mbalimbali,vipepeo utumia miguu yao kutambua ladha za vyakula.
2.Wakati mwanadamu anakadiriwa kuwa na misuli zaidi ya 600,viwazi(larvae) wa vipepeo wenye urefu kati ya sentimeta moja mpaka tano wanakadiriwa kuwa na misuli mara 2 ya mwanadamu inayomwezesha kujongea.
3.Vipepeo hawawezi kupaa ikiwa joto la mwili wao ni chini ya nyuzi 25 za sentigredi.
4.Ingawa mbawa za vipepeo huonekana zina rangi,ukweli ni kwamba mbawa zao wala hazina rangi.*
5.Vipepeo wana uwezo wa kupaa kwa zaidi ya kilomita 8-20 kwa saa.
6.Macho ya vipepeo yana lenzi zaidi ya 600.
7.Wanasayansi wengi waliamini vipepeo ni viumbe wasiosikia mpaka, mwaka 1912 walipogundua kwa mara ya kwanza masikio yanayowawezesha kusikia.
8.Wastani wa umri wa kuishi kwa vipepeo ni siku 30,ingawa wapo wanaishi kwa zaidi ya miezi 6 na wengine siku 5 tu.
9.Vipepeo hupatikana kwenye mabara yote,isipokuwa bara la Antarctica tu.
10.Kipepeo mkubwa kabisa ana urefu wa inchi 12.