Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,746
- 25,662
Mnyama huyu hufahamika pia kwa jina la ndovu au kwa lugha ya kigeni huitwa Elephant, lakini pia jina lake la kisayansi hufahamika kama Loxodanta Africana.
Tembo ndio mnyama pekee ambaye ni mkumbwa kuliko wote anayepatikana ardhini na inaelezwa kwamba tembo dume mkubwa huweza fikia takribani kilo 2000 – 6000 (Tan 2- Tan 6) huku jike akiwa na kilo 2000-4000 (Tan2-Tan4).Mbali na hayo mtoto wa tembo huzaliwa akiwa na kilo zisizo pungua 120.
Jambo lingine ambalo tungependa ufahamu kutoka Jicho Letu Porini leo ni kuhusu mnyama huyu, ni kwamba kuna spishi mbili za tembo yaani kuna tembo wa Afrika na tembo wa Asia.
Kuna mengi ambayo humuhusu mnyama huyu na ambayo huwezi kuyakuta kwa mnyama mwingine wa porini miongoni mwa hayo mengi ni pamoja na haya yafuatayo…
Tembo wanahuwezo wakusikilizana umbali wa kilomita 8.
Tembo wa Afrika wanahisia nzuri kuliko mnyama yoyote.
Tembo huogopa nyuki.
· Ukiacha na binadamu, tembo ndio mnyama mwenye kidevu.
· Tembo ni mnyama ambaye hulala mda usio pungua masaa mawili hadi matatu kwa siku.
Tembo huhitaji takribani kilo 300 kwa siku na lita 160 ili kumuwezesha kushiba, na chakula chake ni majani, magome ya miti, mizizi pamoja na matunda.
Tembo ndio mnyama pekee anayebeba mtoto tumboni (mimba) kwa kipindi cha muda mrefu kuzidi wote dunia ni miezi 22, na mtoto hutoka mmoja tu.
· Tembo hushika mimba kila baada ya miaka miwili
Meno ya tembo hukaliliwa kufika kilo 200 (yote mawili)
· Kundi la tembo au Familia ya tembo huongozwa na jike
Tembo ni mnyama mwenye kumbukumbu nzuri
Tembo akiwa porini huweza kuishi takribani miaka 60-65.
Tembo anaanza kutokwa na meno ya nje baada ya miezi kumi na sita ila ifikapo miezi 30 ndio huuanza kuonekana.
Kinyesi cha tembo huaminika kuwa ni dawa.
Tembo ni miongoni mwa wanyama anayepatikana katika hifadhi zetu hapa nchini yapaswa kujivunia na kuwatunza kwa faida ya vizazi vijavyo pia
NYONGEZA
#1.TEMBO unayemjua wewe kwa wastani ana uzito wa kilogramu elfu kumi kwenda mbele (Hapa namuongelea tembo mkubwa) Tembo pamoja na ukubwa wake akitembea hana kishindo kabisa miguu yake kwa chini ni kama ina sponge hivi.
#2. Wakati mwanamke anabeba ujauzito kwa kipindi cha miezi tisa, TEMBO mkubwa wa kike anabeba ujauzito kwa jumla ya miaka miwili yaani miezi ishirini na minne kabla hajazaa.
#3. Ukimwondoa mwanadamu ambaye ana KIDEVU, Tembo ndiye mnyama mwinginbe ambaye pia anacho kidevu…..
#4. Tembo anao uwezo wa kumsikia Tembo mwenzake akilia kutoka umbali wa kilometa tano….Tembo hana uwezo mkubwa wa kutambua vitu kwa kuona. hutegemea zaidi pua na masikio kuweza kufanikisha shughuli zake. kutokana na hali hiyo, mara nyingi ukiwa porini unashauriwa kumpiga picha tembo BILA ya kutumia flash. hii inatoka na kwamba, endapo utatumia flash wakati unampiga picha, tembo atajenga hisia ya kutoelewa nini kimetokea. kwa kifupi hataweza kutofautisha kama ni kitu cha kawaida au ni hatari. katika mazingira haya, huanza ku-charge kuelekea upande ule ambao mwanga
#5. Ni Tembo wa Afrika pekee mwenye uwezo wa kutofautisha kabila, jinsia na umri wa mwanadamu. Ikiwa jana alijeruhiwa na mtu anayezungumza kiingereza, akisikia kiingereza anakumbuka upesi…
#6. Takribani Tembo mia moja huuwawa kila siku kwa sababu ya pembe zao….
#7. Kila mnyama kuna kitu anakiogopa sana, lakini ni ajabu sana kwa Tembo ambaye anamuogopa nyuki kuliko kitu chochote.
#8. Tembo mkubwa na mzito kupita wote anapatikana Afrika…
#9. Ikiwa mwanadamu hulala walau masaa nane kwa siku, kwa Tembo ni tofauti… Tembo hulala masaa mawili hadi matatu kwa siku!!
#10. Kuhusiana na mambo ya kula na kunywa… Tembo mkubwa huitaji walau kilo mia tatu za chakula na maji lita 160 kwa siku!!! Kama unahitaji kumfuga ujiandae……
11. Tembo anategemea sana uwezo wake wa kunusa ili kuweza kutambua mazingira aliyopo na vitu vinavyomzunguka. Sambamba na harufu, tembo pia ana uwezo mkubwa wa kusikia kupitia masikio yake makubwa (by the way, tembo porini huitwa Masikio).
12 Tembo ana fanya mapenzi kwa masaa 12; masaa 6 ya mwanzo anamuandaa mwenzi wake na 6yanayobaki ndio shughuli yenyewe na hiyo ni ile raundi ya kwanza.
13 Tembo dume huwa na wanawake wawili mpaka wanne
14. Akipiga bao tembo dume manii zake ni ujazo wa lita tano
[HASHTAG]#IFAKARA[/HASHTAG] BABY [emoji8] [emoji8] [emoji8] [emoji8] [emoji8]