Fahamu utofauti wa Asset na Liability

Ukikopa hela bank inaitwa mkopo ukienda kuufanyia biashara inaitwa mtaji ila all in all zote ni fedha.

Financial obligation zote unazotakiwa kuzilipa ni liability lakini unacholipa ni expenses. Hoja yangu ni kwamba kwanini unachanganya liability & expenses??

Naomba nisaidie kutofautisha expenses and liability na muingiliano wake.
Aisee mbna hajajib hili swali ili na mie niondoke na ktu hapa.. em jibu tu mkuu
 
mtu bahili ni yule anaetumia kiasi kidogo tofauti na kile anachozalisha kufanikiwa ama kutofanikiwa sana itategemea kama ana elimu juu ya somo la pesa sijui wewe ulikuwa unataka kutoa ufafanuzi upi
Bahili kwenye uchumi huwa haendelei na uchumi haushauri ubahili.

Kuna tofauti kati ya bahili na mchumi.

Nadhani wewe unatamani kuwa mchumi.
 
mtu bahili ni yule anaetumia kiasi kidogo tofauti na kile anachozalisha kufanikiwa ama kutofanikiwa sana itategemea kama ana elimu juu ya somo la pesa sijui wewe ulikuwa unataka kutoa ufafanuzi upi


Huyoo sio bahili ni mchumi.

Ametumia kidogo chini ya anachokipata


Elimu ya darasani au ya mtaani inasadiki hivyo hivyo nilivyokwambia.
 
mtu bahili ni yule anaetumia kiasi kidogo tofauti na kile anachozalisha kufanikiwa ama kutofanikiwa sana itategemea kama ana elimu juu ya somo la pesa sijui wewe ulikuwa unataka kutoa ufafanuzi upi


Mchumi ana angalia scale of preference(list ya uhitaji) anachagua vyamuhimu vinavyoendana na kipato chake kisizidi.

Bahili anayo scale of preference lakini hachagui unavyovihitaji zaidi ya kubana ata vya muhimu mfano food medicine nakadhalika.
Na siku zote bahili anakufa tajiri lakini kilichomua ni vidonda vya tumbo(kubania ata hela ya kula kwake anakula mlo mmoja!!mchumi anakula milo mitatu kesho au mwaka ujao apate nguvu ya kutafuta fedha zaidi)au watoto kufa kwa kwashakoo au watoto kutokwenda shule au hela kuliwa na panya

Kuwa mchumi usiwe bahili
 
*JE UNA ASSETS AMA LIABILITIES?*

*Asset* ni kitu chochote kinacho kuingizia pesa mfukoni uwepo au usiwepo.

*Liability* ni kitu kinachotoa pesa mfukoni kwako.

Ukitaka kuwa tajiri,hiki ndio assets na liabilities ndio kitu pekee unacho hitaji kukijua na kukifanyia kazi.

Matajiri wote wananunua Assets,lakini sisi Masikini na wenye wenye maisha ya kiwango cha kati tunanunua Liabilities tunazodhani kua ni Assets.

Watu wengi ukiwauliza wana Asset gani wanazomiliki watakutajia vitu kama,nyumba,gari,simu,laptop, duka n.k.

Ni sawa kama tu hivyo vitu vinakuingizia pesa,lakini kama havikuingizii chochote hivyo sio Assets bali ni Liabilities.

Hebu tuangalie nyumba,kama una nyumba yako ya kuishi mwenyewe hiyo ni Liability kubwa sana,maana haikuingizii hata mia,badala yake inakutolea pesa,utalipa umeme,maji,ukarabati na marekebisho ya vitasa,taa,furniture n.k,hayo yoote yanatoa pesa mfukoni.

Lakini kama nyumba umepangisha,hiyo ni Asset.

Gari,kama unaitumia kwa matumizi yako binafsi ya kila siku hiyo ni Liability kubwa,itahitaji mafuta,service,na kama umenunua kwa mkopo wa Bank ndio balaa zaidi,ila kama ni la biashara hiyo ni Asset.
Simu ambayo haikuingizii pesa yoyote zaidi ya kukumalizia vocha na kuishia kuchart,hiyo ni Liability, Tv na radio hata duka pia,maana siku umelifunga huingizi chochote,matumizi yoote unategemea dukani,badala ya duka kukupa faida,unachukua mshahara unaongeza mtaji.

Wasomi wengi walioajiliwa wanakufa masikini kwasababu mishahara yao na mikopo wanayochukua inaishia kununua liabilities kama furniture, TV,radio,simu kubwa,gari,fridge,nguo,viatu, badala ya Asset ambazo zingewaingizia pesa zingine,mwisho wanaishia kuuza liabilities zao na kubaki masikini kabisa.

Watu wengi wanadhani wakiongezewa mshahara wata tatua matatizo yao,badala yake matatizo yanaongezeka maana mshahara (Income) ukiongezeka,matumizi(Expenses) pia yanaongezeka hivyo kuongeza kolamu ya Liabilities. Na hii yote ni kwasababu hatufundishwi elimu ya pesa darasani.

Matajiri woote wana kuza upande wa kipato (Income) na kupunguza upande wa matumizi (Expenses) kwa kununua Assets nyingi na kupunguza Liabilities. Wananunua Luxuries kama gari,TV ,simu kubwa pale tu Assets au vitu walivyowekeza vinapowapatia faida,hivyo faida ndio inanunua magari,nyumba,TV nnk, ndio maana wanasema siri ya utajiri ni ubahili,lakini watu wengine kadri kipato kinapoongezeka na matumizi yanaongezeka.

Kama unataka kua tajiri lazima ujue pia maana halisi ya neno utajiri(Wealth).

*Wealth* is a person's ability to survive so many numbers of days toward, or if you stopped working today,how long could you survive?
Maana yake,kama leo utaacha kufanya kazi ambazo zinakuingizia kipato,una uwezo wa kuendelea kuishi kwa muda gani??

Ukiona ukiacha kufanya kazi huna uwezo wa kumudu mahitaji ya kila siku kwa muda hata wa mwaka mmoja ujue wewe bado huna Mali(wealth) maana huna Assets zinazoweza kukuingizia kipato cha kuweza kukufanya uendelee kuishi pindi uachapo kazi.

Jiulize msharaha wako unanunua Assets au Liabilities, na pia ujiulize are you Wealth or not?



uwe na siku njema na jipime unawekeza kwenye asset au liabilities?
 
wewe mnaona unashindwa kutofautisha kati investments na assets mkuu, kama hujasoma hata accounts jifunzie hata mtandaoni unufaike



Assets ni mali yoyote unayomiliki inayoweza kupimwa kwa fedha..mfano nyumba, simu, tv, gari lako binafsi, gari la biashara n.k

Kila investiment ni asset ila sio kila asset ni investment

Liability ni madeni unayodaiwa unayotakiwa ulipe... mfano kama bill za maji ambazo unadaiwa, mkopo wa benk, mkopo wa rafiki pengine, mishahara ya wafanyakazi wako ambayo hujalipa n.k

Hizo definition ulizotoa hapo ni za mtaani sio za kiuchumi au kihasibu... kwa hiyo hao unaowaona hawapo sahihi ndio walio sahihi as far as accounting is concerned

assets definition and meaning | AccountingCoach
Una hoja nzuri, ila uliposema "not all assets can be investments"hapa ulimaanisha ninj?je hizi sio liabilities?
 
Usipotoshe watu...unasema ASSET NI KITU chochote kinachokuingizia kipato uwepo usiwepo...sio kwl...ASSET NI KITU CHOCHOTE ambacho KILA SIKU KINAPANDA THAMANI.....MFANO KIWANJA,,SHAMBA,,NYUMBA,,DHAHABU,,MADINI ....na vitu kama SIMU,,GARI,,TV ..makochi sio ASSET.....kama unasema asset ni kitu kinachokupa pesa HATA UKIWA na banda LA kuonyesha MPIRA...pia ni asset?
 
Mleta Mada Upo Shallow Sana,japo Utasapotiwa Na Ambao Hawajasoma Uchumi Au Makabati
Nyumba Nayoishi Mie Ni Assets Naokoa Zaidi Ya Million 4 Kulipa Kodi Kwa Mwaka,hapo Sijaongelea Kuiliquidate Bado
 
Una mawazo mazuri ila umeenda chaka kweli hasa ktk mifano ya liability tambua kuwa ili uprocess asset you need to have liability.Nyumba ni bonge ya asset hata gari ni asset inaitwa non fixed asset yaani asset ibayotembea.
Siwrzi kukulaumu kwa kuwa kwa njia hii yawezekana unataka kujifunza zaidi.Ingia mtandaoni google, types of asset,liability and their examples.
 
Tofautisha kati ya investment na Assets, sio kila kilichoandikwa kwenye Rich dad, Poor dad ni mstari kutoka kwenye msahafu usioweza kubadilishwa!
Investment ni kitega uchumi cha kuingiza pesa na Asset ni kitu Chako unachoweza kubadilisha kikawa pesa ukafanyia kazi nyingine. Thanks 4 sharing anyway.
Not all assets are investment but all investment are assets.
Not all agreement are contract but all contracts are agreement(business law)
 
Mleta mada na real G, kitabu cha RICH DAD POOR DAD, kilikuwa self published, sababu ni kuwa wasomi wote wakiwepo wachapishaji wa vitabu walimwambia kaandika rubbish, hawawezi kuchapisha, hivyo akaenda kuchapisha mwenyewe.

Ninaamini definition ya Robert Kiyosaki kuhusu asset na liability ndio sahihi, ila najua hakuna mtu anaweza kuelewa, ni wachavhe tu kama mimi, ni Conventional wisdom, kwamba nyumba unayoishi ni asset, to save money is smart nk nk. Kwa hiyo kama mtunzi wa vitabu alishindwa kueleweka, ni ngumu sana kwa mtu kama mimi au mleta mada kueleweka.
 
Non-Current Assets and Liabilities......The main components of Statement of financial position...
C=A-L
 
Back
Top Bottom