Fahamu utofauti wa Asset na Liability

Southern Highland

JF-Expert Member
Mar 22, 2017
13,194
21,527
Salaam wakuu. Nimeitoa huko nikaona itapendeza nikishare nanyi. Hiyo hapo tiririka nayo.

ASSET~ni kitu chochote kinacho kuingizia pesa mfukoni uwepo au usiwepo.

LIABILITY~ni kitu kinachotoa pesa mfukoni kwako.
Ukitaka kuwa tajiri hiki ndio kitu pekee unacho hitaji kukijua na kukifanyia kazi.

Matajiri wote wananunua Assets lakini Masikini na wenye wenye maisha ya saizi ya kati wananunua Liabilities wanazodhani kuwa ni Assets.

Watu wengi ukiwauliza una Asset gan unayomiliki atakutajia vitu kama nyumba, gari, simu, laptop, duka.

Ni sawa kama tu hivyo vitu vinakuingizia pesa, lakini kama havikuingizii chochote hivyo sio Assets bali ni Liabilities.

Hebu tuangalie nyumba
Kama una nyumba yako ya kuishi mwenyewe hiyo ni Liability kubwa sana maana haikuingizii hata mia badala yake inakutolea pesa utalipa umeme, maji, ukarabati na malekebisho ya vitasa, taa, furniture n.k. Hayo yoote yanatoa pesa mfukoni.

Lakini kama nyumba umepangisha hiyo ni Asset. Gari kama unaitumia kwa matumizi yako binafsi ya kila siku hiyo ni Liability kubwa itahitaji mafuta, service na kama umenunua kwa mkopo wa Bank ndio balaa zaidi, ila kama ni la biashara hiyo ni Asset.

Simu ambayo haikuingizii pesa yoyote zaidi ya kukumalizia vocha na kuishia kuchat hiyo ni Liability, Tv na radio hata duka pia, maana siku umelifunga huingizi chochote, matumizi yoote unategemea dukani, badala ya duka kukupa faida, unachukua mshahara unaongeza mtaji.

Wasomi wengi walioajiriwa wanakufa masikini kwasababu mishahara yao na mikopo wanayochukua inaishia kununua liabilities kama furniture, TV, radio, simu kubwa, gari, fridge, nguo, viatu, badala ya Asset ambazo zingewaingizia pesa zingine, mwisho wanaishia kuuza liabilities zao na kubaki masikini kabisa.

Watu wengi wanadhani wakiongezewa mshahara wata tatua matatizo yao, badala yake matatizo yanaongezeka maana mshahara (Income) ukiongezeka, matumizi (Expenses) pia yanaongezeka hivyo kuongeza column ya Liabilities. Na hii yote ni kwasababu hatufundishwi elimu ya pesa darasani.

Matajiri woote wana kuza upande wa kipato (Income) na kupunguza upande wa matumizi (Expenses) kwa kununua Assets nyingi na kupunguza Liabilities, wananunua Luxuries kama gari, tv ,simu kubwa pale tu Assets au vitu walivyowekeza vinapowapatia faida, hivyo faida ndio inanunua magari, nyumba, TV n.k,

Ndio maana wanasema siri ya utajiri ni ubahili, lakini watu wengine kadri kipato kinapoongezeka na matumizi yanaongezeka. Kama unataka kua tajiri lazima ujue pia maana halisi ya neno utajiri(Wealth).

WEALTH~ Is a person's ability to survive so many numbers of days toward, or if you stopped working today, how long could you survive?
Maana yake kama leo utaacha kufanya kazi ambazo zinakuingizia kipato una uwezo wa kuendelea kuishi kwa muda gani?

Ukiona ukiacha kufanya kazi huna uwezo wa kumudu mahitaji ya kila siku kwa muda hata wa mwaka mmoja ujue wewe bado huna Mali(wealth) maana huna Assets zinazoweza kukuingizia kipato cha kuweza kukufanya uendelee kuishi pindi uachapo kazi.

Jiulize msharaha wako unanunua Assets au Liabilities na pia ujiulize are you Wealth or not?

Thanks
Wandugu, muwe na siku njema na jipime unawekeza kwenye asset au liabilities?

C&P WhatsApp Group
 
wewe mnaona unashindwa kutofautisha kati investments na assets mkuu, kama hujasoma hata accounts jifunzie hata mtandaoni unufaike

Assets ni mali yoyote unayomiliki inayoweza kupimwa kwa fedha..mfano nyumba, simu, tv, gari lako binafsi, gari la biashara n.k

Kila investiment ni asset ila sio kila asset ni investment

Liability ni madeni unayodaiwa unayotakiwa ulipe... mfano kama bill za maji ambazo unadaiwa, mkopo wa benk, mkopo wa rafiki pengine, mishahara ya wafanyakazi wako ambayo hujalipa n.k

Hizo definition ulizotoa hapo ni za mtaani sio za kiuchumi au kihasibu... kwa hiyo hao unaowaona hawapo sahihi ndio walio sahihi as far as accounting is concerned

assets definition and meaning | AccountingCoach
 
Na wewe unachanganya liability na EXPENSES.
 
Mkuu gharama ulizotumia kununua gari mwaka juzi ukitaka kuliuza utapata pesa ileile uliyonunulia.?

Nilichoandika kinaweza kisiwe sawa asilimia 100 lakini kina zaidi ya asilimia 90 ya ulichoandika.
 
Tofautisha kati ya investment na Assets, sio kila kilichoandikwa kwenye Rich dad, Poor dad ni mstari kutoka kwenye msahafu usioweza kubadilishwa!
Investment ni kitega uchumi cha kuingiza pesa na Asset ni kitu Chako unachoweza kubadilisha kikawa pesa ukafanyia kazi nyingine. Thanks 4 sharing anyway.
 
Mkuu gharama ulizotumia kununua gari mwaka juzi ukitaka kuliuza utapata pesa ileile uliyonunulia.?

Nilichoandika kinaweza kisiwe sawa asilimia 100 lakini kina zaidi ya asilimia 90 ya ulichoandika.
Kwenye bandiko lako kuu, ukubali umetoa tafsiri isiyo sahihi kitaaluma (uchumi na usimamizi fedha) ila inakidhi uelewa wa mtu wa kawaida kuhusu mapato na matumizi.

Kitaaluma maneno hayo yanatumika katika mizania ya kifedha (Balance Sheet) ambayo inatamka kwamba:
Assets = Equity + Liabilities
Assets ni mali yote, inayobadilika (current asset) km pesa taslimu, na isiyobadilika (fixed asset) km nyumba, ambayo anamiliki mtu/ kampuni nk. Mali hii imepatika aidha kutokana na mtaji (equity) ya mmiliki au madeni (liabilities).

Hivyo utajiri (networthness) wa mtu ni mali aliyokuwa nayo na siyo biashara anayoifanya yenye faida au kuwa na ukwasi wa kifedha.
 
hivi hawa wanaobishana wamefundishwa na wabongo wa chuo kipi! definitions zinatofautiana!
 
Kwenye bandiko lako kuu, ukubali umetoa tafsiri isiyo sahihi kitaaluma (uchumi na usimamizi fedha) ila inakidhi uelewa wa mtu wa kawaida kuhusu mapato na matumizi.

Kitaaluma maneno hayo yanatumika katika mizania ya kifedha (Balance Sheet) ambayo inatamka kwamba:
Assets = Equity + Liabilities
Assets ni mali yote, inayobadilika (current asset) km pesa taslimu, na isiyobadilika (fixed asset) km nyumba, ambayo anamiliki mtu/ kampuni nk. Mali hii imepatika aidha kutokana na mtaji (equity) ya mmiliki au madeni (liabilities).

Hivyo utajiri (networthness) wa mtu ni mali aliyokuwa nayo na siyo biashara anayoifanya yenye faida au kuwa na ukwasi wa kifedha.

Kitu kinacho nifanyaga nisibishane na wasomi(uchumi na wengineo) ni kama Ulichoandika.

Yani wasomi wote wanakuaga na hoja na definition zinazofanana utafikiri mapacha. Yani najua kabisaa mawazo ya wasomi yalivyo ndani ya box yamewekwa mipaka yakutofikiri nje walichokaririshwa darasani.

Majibu ya wasomi huwa yanafanana Tanzania nzima. THINK OUT OF BOX.
 
Huyo jamaa point yake ni kuwa ukiwa na kitu ambacho hakikuingizii hela basi ni mzigo (mzigo ndio liability kwenye definition nyingine isiyo ya kiuchumi) hii inaweza kuwa kweli kutokana na maisha yako yalivyo... gari linawezaa kuwa haliningizii hela ila linaniwaisha kazini mapema, simu inaweza kuwa hainingizii hela ila nawasiliana na watu watakaonipa deal na kukamilisha biashara, nyumba niliyojenga ninayokaa hainingizii hela ila imeokoa fedha (kodi) ambazo ningetumia kupanga nyumba nyingine. Utasemaje hizi ni mzigo kwako?
 
Salaam wakuu. Nimeitoa huko nikaona itapendeza nikishare nanyi. Hiyo hapo tiririka nayo.

ASSET~ni kitu chochote kinacho kuingizia pesa mfukoni uwepo au usiwepo.

LIABILITY~ni kitu kinachotoa pesa mfukoni kwako.
Ukitaka kuwa tajiri hiki ndio kitu pekee unacho hitaji kukijua na kukifanyia kazi.

Matajiri wote wananunua Assets lakini Masikini na wenye wenye maisha ya saizi ya kati wananunua Liabilities wanazodhani kuwa ni Assets.

Watu wengi ukiwauliza una Asset gan unayomiliki atakutajia vitu kama nyumba, gari, simu, laptop, duka.

Ni sawa kama tu hivyo vitu vinakuingizia pesa, lakini kama havikuingizii chochote hivyo sio Assets bali ni Liabilities.

Hebu tuangalie nyumba
Kama una nyumba yako ya kuishi mwenyewe hiyo ni Liability kubwa sana maana haikuingizii hata mia badala yake inakutolea pesa utalipa umeme, maji, ukarabati na malekebisho ya vitasa, taa, furniture n.k. Hayo yoote yanatoa pesa mfukoni.

Lakini kama nyumba umepangisha hiyo ni Asset. Gari kama unaitumia kwa matumizi yako binafsi ya kila siku hiyo ni Liability kubwa itahitaji mafuta, service na kama umenunua kwa mkopo wa Bank ndio balaa zaidi, ila kama ni la biashara hiyo ni Asset.

Simu ambayo haikuingizii pesa yoyote zaidi ya kukumalizia vocha na kuishia kuchat hiyo ni Liability, Tv na radio hata duka pia, maana siku umelifunga huingizi chochote, matumizi yoote unategemea dukani, badala ya duka kukupa faida, unachukua mshahara unaongeza mtaji.

Wasomi wengi walioajiriwa wanakufa masikini kwasababu mishahara yao na mikopo wanayochukua inaishia kununua liabilities kama furniture, TV, radio, simu kubwa, gari, fridge, nguo, viatu, badala ya Asset ambazo zingewaingizia pesa zingine, mwisho wanaishia kuuza liabilities zao na kubaki masikini kabisa.

Watu wengi wanadhani wakiongezewa mshahara wata tatua matatizo yao, badala yake matatizo yanaongezeka maana mshahara (Income) ukiongezeka, matumizi (Expenses) pia yanaongezeka hivyo kuongeza column ya Liabilities. Na hii yote ni kwasababu hatufundishwi elimu ya pesa darasani.

Matajiri woote wana kuza upande wa kipato (Income) na kupunguza upande wa matumizi (Expenses) kwa kununua Assets nyingi na kupunguza Liabilities, wananunua Luxuries kama gari, tv ,simu kubwa pale tu Assets au vitu walivyowekeza vinapowapatia faida, hivyo faida ndio inanunua magari, nyumba, TV n.k,

Ndio maana wanasema siri ya utajiri ni ubahili, lakini watu wengine kadri kipato kinapoongezeka na matumizi yanaongezeka. Kama unataka kua tajiri lazima ujue pia maana halisi ya neno utajiri(Wealth).

WEALTH~ Is a person's ability to survive so many numbers of days toward, or if you stopped working today, how long could you survive?
Maana yake kama leo utaacha kufanya kazi ambazo zinakuingizia kipato una uwezo wa kuendelea kuishi kwa muda gani?

Ukiona ukiacha kufanya kazi huna uwezo wa kumudu mahitaji ya kila siku kwa muda hata wa mwaka mmoja ujue wewe bado huna Mali(wealth) maana huna Assets zinazoweza kukuingizia kipato cha kuweza kukufanya uendelee kuishi pindi uachapo kazi.

Jiulize msharaha wako unanunua Assets au Liabilities na pia ujiulize are you Wealth or not?

Thanks
Wandugu, muwe na siku njema na jipime unawekeza kwenye asset au liabilities?

C&P WhatsApp Group
Asset = Ajira (mshahara)
Liability = Mchepuko...
 
Nimesoma kwa makini, na nimeondoka na kitu

#. Ili ufanikiwe unatakiwa kuwa bahili kiasi, japo kipato kinaongeza kila siku lakini ubahili ubakie kuwa ndio tabia yako.

Bahili kwenye uchumi huwa haendelei na uchumi haushauri ubahili.

Kuna tofauti kati ya bahili na mchumi.

Nadhani wewe unatamani kuwa mchumi.
 
Expense zikishakuwa accrued tayari ni liability mkuu... yaani kama unadaiwa bill ya miezi 3 na Tanesco hiyo ni liability

Ukikopa hela bank inaitwa mkopo ukienda kuufanyia biashara inaitwa mtaji ila all in all zote ni fedha.

Financial obligation zote unazotakiwa kuzilipa ni liability lakini unacholipa ni expenses. Hoja yangu ni kwamba kwanini unachanganya liability & expenses??

Naomba nisaidie kutofautisha expenses and liability na muingiliano wake.
 
Back
Top Bottom