Fahamu utajiri uliopo kwenye uwekezaji wa dhamana za Serikali (Treasury Bills & Bonds)

Davion Delmonte Jr.

JF-Expert Member
Oct 27, 2013
2,149
1,710
UTAJIRI MKUBWA ULIOPO KWENYE UWEKEZAJI WA DHAMANA ZA SERIKALI

Uwekezaji kwenye dhamana za serikali umegawanyika makundi mawili.

i) Dhamana za muda mfupi (treasury bills)
ii) Dhamana za muda mrefu (treasury bonds)

Kwa nchi yetu ya Tanzania biashara ya dhamana za serikali inasimamiwa na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kwa niaba ya serikali ya Tanzania.

Dhamana za muda mfupi (treasury bills)
Hizi ni dhamana za muda mfupi ikimaanisha zinaiva ndani ya mwaka mmoja. Lengo kubwa hasa kwa serikali kuweka Treasury bills ni kupata fedha kwa ajili kukabiliana na mapungufu ya fedha katika bajeti na pale inapohitaji fedha kwa haraka.

Dhamana za muda mfupi zipo katika makundi manne kutegemea na mda zitakapoiva: ya siku 35, siku 91, siku 182 na siku 364.

Uwekezaji katika Treasury bill una faida zifuatazo kwa mwekezaji:

i)Hazina hatari yoyote kubwa (risk free) kwa mwekezaji na ni uwekezaji wa uhakika kwa sababu zinatolewa na serikali.

ii)Zaweza kuhamishika kutoka umiliki wa mtu mmoja kwenda kwa mwingine. Ikimaanisha pale mwekezaji anapotaka kuuza anaweza akafanya hivo.

iii)Zaweza kutumika kama dhamana za kuombea mikopo kwenye taasisi za fedha bila usumbufu wowote kwa sababu thamani ya treasury bill coupon haibadiliki kwa hiyo ni rahisi kwa taasisi za fedha kuzipa kipaumbele kutumika kwenye dhamana.

iv)Gawio ni kubwa pale unapowekeza kwenye treasury bills zaidi hata ya kuwekeza kwenye taasis yeyote ya fedha kupitia fixed deposits. (namaana ya kwamba riba katika treasury bills ni kubwa maradufu ya riba za benki)

Soko la treasury bills

Biashara na soko la treasury bills zinafanyika kwa njia mbili;

a) Soko la awali (primary market) hapa ni pale banki kuu ya Tanzania inapotoa kwa mara ya kwanza treasury bills kwa wawekezaji.

b) Soko la pili (secondary market) hii inahusisha kuuza na kununua treasury bills na hii inafanyika Dar es salaam stock exchange DSE. Hapa ndipo pale mtu anapotaka kuuza treasury bills anayoimiliki anaweza kwenda kuuza.

Kianzio cha kuwa mwekezaji wa moja kwa moja kwenye treasury bills kwa Tanzania ni sh. 5,000,000. Ina maana kwamba ukiwa na mtaji wa kuanzia milioni tano basi unaruhusiwa moja kwa moja kushiriki kwenye mnada wa treasury bills (treasury bills auction).

Kwa wawekezaji wa mtaji chini ya milioni tano basi wao watashiriki kwenye mnada kupitia primary dealers ambao kwa urahisi ni mabrokers na commercial banks

Primary dealers ambao wamethibitishwa na BOT ni hawa wafuatao (ambao wale wenye mitaji chini ya milioni tano watapitia kwao) Akiba Commercial Bank Ltd, Citibank (T) Ltd, CRDB Bank Ltd, Diamond Trust Bank (T) Ltd, Eurafrican Bank (T) Ltd.Exim Bank (T) Ltd. Habib African Bank Ltd. International Commercial Bank (T) Ltd. Kenya Commercial Bank (T) Ltd.NBC Limited. NMB Ltd. Stanbic Bank (T) Limited Standard Chartered Bank Ltd.Orbit Securities Co. Ltd. Rasilimali Limited Solomoni Securities Ltd. Core securities Ltd. Tanzania securities Ltd. Vertex International Securities.

Unapata vipi pesa kupitia dhamana za muda mfupi?
Serikali kupitia BOT inapotoa treasury bills zinakuwa katika mfumo wa zabuni ikimaanisha kwamba wawekezaji watatakiwa kwa mfano kusema watanunua kila shilingi 100 ya serikali kwa kiasi gani? (hatua hiyo ya kwanza inaitwa bidding)

Ili kupata faida kwa wawekezaji wanatakiwa kutoa bei ambayo ipo katika discout, ikiwa na maana mwekezaji anaweza kununua shilingi 100 ya serikali kwa shilingi 93 hivo mda wa kuiva ukifika atapata faida ya shilingi 7.

Mfano serikali imetoa treasury bills ya siku 365. Kisha mwekezaji akaweka bid ya kununua kila shilingi 100 kwa shilingi 75. Kama mwekezaji atafanikiwa kwenye zabuni hiyo atapata treasury bill yenye (face value) ya Tzs 100,000,000 ingawaje kiasi alichotoa ni Tzs 75,000,000 kwa sababu ndicho kiasi alicho bid katika kabrasha la zabuni yake.

Baada ya treasury bills kuiva yaani kutimia siku 365, mwekezaji atalipwa na BOT kiasi cha TZS 100,000,000 ambayo italeta faida ya (TZS 100,000,000-TZS 75,000,000= TZS 25,000,000). Hivo faida itakuwa ni TZS 25,000,000.

Ukiweka katika asilimia ni kama ifuatavyo;
- Kanuni ya kukokotoa riba katika treasury bills:
Riba=(F-P)/P ×(365×100)/N

F= face value ya treasury bills ambayo ni 100
P= bidding price ambayo ni 75 kama mfano unavosema
N= idadi ya siku treasury bills itapoiva mfano wetu ni siku 365

Riba= (100-75)/75 ×(365×100)/365
=0.3333×100
Riba = 33.33%

Ikiwa na maana kwa pesa ambayo utatoa kununua treasusry bills utapata gawio la asilimia 33.33% ndani ya siku 365 yaani mwaka mmoja tu.

Piga mahesabu kama umewekeza milioni 100 ambazo huna matumizi nazo ina maana baada ya siku 365 utakuwa na faida ya kama milioni 30 ambazo hata kujazitolea jasho.

Nataka pia kuwamegea siri kwamba mabenki ya kibiashara na wafanyabiashara wakubwa ndio wamekuwa wakitajirikia hapa kwani wao wanawekeza kuanzia bilioni na kwenda juu. Kwa hiyo unaweza kufikiri ni pesa kiasi gani wanatengeneza.

Kuna watanzania wengi sana wana mamilioni ya pension benki hizi ndizo fursa za kuchangamkia ambazo huwezi kuzisikia zikitangazwa kwa maana ndipo pesa ilipo.

Kama hujaelewa waweza acha comment yako hapa then ntakujibu.

=========

SOMA PIA:

1) Tofauti ya uwekezaji wa hati fungani na masoko mengine ya mitaji kama Hisa - JamiiForums

2)
 
Ni nzuri sana kwa watu wenye pesa na hawazihitaji kwa muda huo na hawajui kufanya biashara.....

Kama una fedha nyingi, ni biashara poa sana. Kama sikosei familia nyingi nchi za WEST wanaishi maisha mazuri ingawa ukiwauliza wanafanya kazi wapi, jibu ni hatufanyi kazi. Wanaishi kwa riba kwenye fedha za Mabank, biashara kubwa, Oil and Gas field nk......
 
Ni moja ya njia za uwekezaji mzuri sana.

Kwa mfano mmoja wa wazazi akifariki na ameacha pesa nzuri ya kutosha, kiasi fulani kinaweza kuchukuliwa na kuwekezwa kwenye kununua hizo bonds za kila mwaka na watoto wakawa wanalipiwa shule yoyote waitakayo.

Hii imenifundisha kwamba unaweza ukawaona watu wengine wamekaa kiajabuajabu lakini wana uwezo kutokana kutumia njia kama hii.
 
Fact kabisa.. Karibu kila familia America inajihusisha na uwekezaji kwenye masoko ya fedha.
 
Ni moja ya njia za uwekezaji mzuri sana.

Kwa mfano mmoja wa wazazi akifariki na ameacha pesa nzuri ya kutosha, kiasi fulani kinaweza kuchukuliwa na kuwekezwa kwenye kununua hizo bonds za kila mwaka na watoto wakawa wanalipiwa shule yoyote waitakayo.

Hii imenifundisha kwamba unaweza ukawaona watu wengine wamekaa kiajabuajabu lakini wana uwezo kutokana kutumia njia kama hii.
Sema vile watu hawajui.. Lakini faida za kuwa na hizi financial assets ni kubwa mno. Kuliko unavoweza kufikiri
 
Ni kweli tupu lakini wengi wa wanaJF tuna pesa za mboga chini ya 10m na si za kuingiza huko kwa mwaka mzima, nafikiri kwa sasa tuanze na Hisa za makampuni na SACCOS kisha tukikuza mtaji ndo tuwekeze huko uliposhaur

Sifahamu kuhusu saccoss, ukipata muda naomba uelezee.
 
DAVIOn Delmonte Jr Je vipi kuhusu inflation. Je hiyo Treasury bills inakua inahusika na kuporomoka kwa thamani ya fedha?? mfano ukiweka 10m ambayo inaweza kununua kiwanja Kibamba alafu baada ya mwaka kiwanja cha Kibamba kikauzwa 15m huwezi kununua kwa kua pesa yako ikiiva inakua 13.33m. Au wakati unanua hizo bills dola moja ya US ilikua 1500Tsh baada ya bills kuiva thamani ya 1USD ni zaidi ya 2200Tsh. Unakua umepata hasara. Je hili wanalifikria??
Though asante kwa maelezo yako mazuri
 
Last edited by a moderator:

ulichosema ni sahihi kwamba inflation na kupanda kwa dola kunaweza kushusha thamani ya uwekezaji wako. Lakini ukiangalia kwa upande mngine hiyo milioni 10 kama ungeiacha bank ungeumia zaidi kwa sababu hiyo faida ya 3 milioni siyo haba.
 
Last edited by a moderator:
UTAJIRI MKUBWA ULIOPO KWENYE UWEKEZAJI WA DHAMANA ZA SERIKALI

Uwekezaji kwenye dhamana za serikali umegawanyika makundi mawili.

i) Dhamana za muda mfupi (treasury bills)
ii) Dhamana za muda mrefu (treasury bonds)

Kwa nchi yetu ya Tanzania biashara ya dhamana za serikali inasimamiwa na banki kuu ya Tanzania (BOT) kwa niaba ya serikali ya Tanzania.

Dhamana za muda mfupi (treasury bills)
Hizi ni dhamana za muda mfupi ikimaanisha zinaiva ndani ya mwaka mmoja. Lengo kubwa hasa kwa serikali kuweka Treasury bills ni kupata fedha kwa ajili kukabiliana na mapungufu ya fedha katika bajeti na pale inapohitaji fedha kwa haraka.

Dhamana za muda mfupi zipo katika makundi manne kutegemea na mda zitakapoiva: ya siku 35, siku 91, siku 182 na siku 364.

Uwekezaji katika Treasury bill una faida zifuatazo kwa mwekezaji;
i)Hazina hatari yoyote kubwa (risk free) kwa mwekezaji na ni uwekezaji wa uhakika kwa sababu zinatolewa na serikali.

ii)Zaweza kuhamishika kutoka umiliki wa mtu mmoja kwenda kwa mwingine. Ikimaanisha pale mwekezaji anapotaka kuuza anaweza akafanya hivo.

iii)Zaweza kutumika kama dhamana za kuombea mikopo kwenye taasisi za fedha bila usumbufu wowote kwa sababu thamani ya treasury bill coupon haibadiliki kwa hiyo ni rahisi kwa taasisi za fedha kuzipa kipaumbele kutumika kwenye dhamana.

iv)Gawio ni kubwa pale unapowekeza kwenye treasury bills zaidi hata ya kuwekeza kwenye taasis yeyote ya fedha kupitia fixed deposits. (namaana ya kwamba riba katika treasury bills ni kubwa maradufu ya riba za benki)

Soko la treasury bills
Biashara na soko la treasury bills zinafanyika kwa njia mbili;

a) Soko la awali (primary market) hapa ni pale banki kuu ya Tanzania inapotoa kwa mara ya kwanza treasury bills kwa wawekezaji.

b) Soko la pili (secondary market) hii inahusisha kuuza na kununua treasury bills na hii inafanyika Dar es salaam stock exchange DSE. Hapa ndipo pale mtu anapotaka kuuza treasury bills anayoimiliki anaweza kwenda kuuza.

Kianzio cha kuwa mwekezaji wa moja kwa moja kwenye treasury bills kwa Tanzania ni sh. 5,000,000. Ina maana kwamba ukiwa na mtaji wa kuanzia milioni tano basi unaruhusiwa moja kwa moja kushiriki kwenye mnada wa treasury bills (treasury bills auction).

Kwa wawekezaji wa mtaji chini ya milioni tano basi wao watashiriki kwenye mnada kupitia primary dealers ambao kwa urahisi ni mabrokers na commercial banks

Primary dealers ambao wamethibitishwa na BOT ni hawa wafuatao (ambao wale wenye mitaji chini ya milioni tano watapitia kwao) Akiba Commercial Bank Ltd, Citibank (T) Ltd, CRDB Bank Ltd, Diamond Trust Bank (T) Ltd, Eurafrican Bank (T) Ltd.Exim Bank (T) Ltd. Habib African Bank Ltd. International Commercial Bank (T) Ltd. Kenya Commercial Bank (T) Ltd.NBC Limited. NMB Ltd. Stanbic Bank (T) Limited Standard Chartered Bank Ltd.Orbit Securities Co. Ltd. Rasilimali Limited Solomoni Securities Ltd. Core securities Ltd. Tanzania securities Ltd. Vertex International Securities.

Unapata vipi pesa kupitia dhamana za muda mfupi?
Serikali kupitia BOT inapotoa treasury bills zinakuwa katika mfumo wa zabuni ikimaanisha kwamba wawekezaji watatakiwa kwa mfano kusema watanunua kila shilingi 100 ya serikali kwa kiasi gani? (hatua hiyo ya kwanza inaitwa bidding)

Ili kupata faida kwa wawekezaji wanatakiwa kutoa bei ambayo ipo katika discout, ikiwa na maana mwekezaji anaweza kununua shilingi 100 ya serikali kwa shilingi 93 hivo mda wa kuiva ukifika atapata faida ya shilingi 7.

Mfano serikali imetoa treasury bills ya siku 365. Kisha mwekezaji akaweka bid ya kununua kila shilingi 100 kwa shilingi 75. Kama mwekezaji atafanikiwa kwenye zabuni hiyo atapata treasury bill yenye (face value) ya Tzs 100,000,000 ingawaje kiasi alichotoa ni Tzs 75,000,000 kwa sababu ndicho kiasi alicho bid katika kabrasha la zabuni yake.

Baada ya treasury bills kuiva yaani kutimia siku 365, mwekezaji atalipwa na BOT kiasi cha TZS 100,000,000 ambayo italeta faida ya (TZS 100,000,000-TZS 75,000,000= TZS 25,000,000). Hivo faida itakuwa ni TZS 25,000,000.

Ukiweka katika asilimia ni kama ifuatavyo;
- Kanuni ya kukokotoa riba katika treasury bills:
Riba=(F-P)/P ×(365×100)/N

F= face value ya treasury bills ambayo ni 100
P= bidding price ambayo ni 75 kama mfano unavosema
N= idadi ya siku treasury bills itapoiva mfano wetu ni siku 365

Riba= (100-75)/75 ×(365×100)/365
=0.3333×100
Riba = 33.33%

Ikiwa na maana kwa pesa ambayo utatoa kununua treasusry bills utapata gawio la asilimia 33.33% ndani ya siku 365 yaani mwaka mmoja tu.

Piga mahesabu kama umewekeza milioni 100 ambazo huna matumizi nazo ina maana baada ya siku 365 utakuwa na faida ya kama milioni 30 ambazo hata kujazitolea jasho.

Nataka pia kuwamegea siri kwamba mabenki ya kibiashara na wafanyabiashara wakubwa ndio wamekuwa wakitajirikia hapa kwani wao wanawekeza kuanzia bilioni na kwenda juu. Kwa hiyo unaweza kufikiri ni pesa kiasi gani wanatengeneza.
Kuna watanzania wengi sana wana mamilioni ya pension benki hizi ndizo fursa za kuchangamkia ambazo huwezi kuzisikia zikitangazwa kwa maana ndipo pesa ilipo.

Kama hujaelewa waweza acha comment yako hapa then ntakujibu..

Somo zuri. Ila ungeweka comparison ya hisa vs bonds., Kwa uelewa wangu mdogo Bonds hazina risk ila xzzina low return uklinganisha na hisa. Hisa zina return kubwa ila risk ni kubwa
 
Back
Top Bottom