Fahamu undani wa mnyama simba


Ahsante Mkuu (noted with concern).
 
Kingine ni kwamba simba hua hapendi dharau za kuchekewa chekewa kutaniwa

anakula kilo 15 baada ya hapo anapumzika kuwinda lakini hii haimaanishi kwamba nyumbu wanaweza kupita mbele yake akawaacha.
Sijapendezwa na kitendo chao cha kula kilo 15 tu na kushiba wakati wanaangusha mnyama wenye kilo 200 hadi 300 kwa mfano wale nyumbu au mbogo. Ni waharibifu tu hao.
 
Je wajua ni kwanini simba jike anajitenga pale anapokaribia kuzaa na kwenda mafichoni kipindi cha miezi mitatu na anaporudi lazima awatambulishe watoto kwa mzee Wa familia na kinakuwa kipindi kigumu kwa familia zima kwani mzee akiwakataa watoto anawauwa.sababu kubwa ni hii.na ndio msingi mkubwa sana wasimba jike kwenda mafichoni.simba jike anakuwa na chuchu za matiti nne tuu.sasa kama unakumbuka simba wananyonyesha watoto Wa simba yoyote jike Wa ile familia yao sasa kama akijifungulia pale kwenye familia basi watoto wake watakufa kwa njaa maana hawana uwezo mkubwa wakunyonya maziwa ya mama yao kwakuwa wale wengine wameshakuwa wakubwa kuliko wao na watanyonya wakubwa tuu.hapo mama analazimika kuondoka tuu ilikulinda afya za watoto wake.sababu ndogo ndogo ni kwa kuogopa wasiumie kwenye familia.magonjwa ya milipuko.
 
Hawa simba dume ,vijana baada ya kufikisha miaka miwili wanatimuliwa kwenye familia zao ,swali je hakuna uwezekano baadae wakakutana na mama na dada zake ? Au anawajua dada na mama zake hivyo hatoweza kuwaingilia kimwili ?
 
Mkuu nakushukuru sana kwa masomo yako murua. Ubarikiwe sana. Huwa napenda kuangalia video za wanyama na nilishangazwa na kitendo cha simba kuwa dhaifu kwa chatu tofauti na chui ambao wana uwezo wa kuua chatu. Unaweza kunifafanulia kidogo kuhusu hilo suala?
 
Duuuh! Naona simba wana akili sana kuzidi wanyama wote isipokuwa binadamu
 
Sijapendezwa na kitendo chao cha kula kilo 15 tu na kushiba wakati wanaangusha mnyama wenye kilo 200 hadi 300 kwa mfano wale nyumbu au mbogo. Ni waharibifu tu hao.
Aahh.. Mkuu piga mahesabh vzur, simba hali mmoja, wanakuwa kadhaa hapo kila mmoja na kilo 15 zake tumboni.. Hizo kilo 200za myumbu bado hujatoa mifupa, kichwa, utumbo n.k.. Kwa hyo kuangusha hao wanyama ni sawa tu
 

AISEEE mnajuaje na hali hamjui lugha yao
 

INTERESTING.....
 
Mkuu,
Asante kwa kjishughulisha kutupa elimu hii nzuri ingawaje kuna wapuuzi wanashindwa kuona uthamani wa kupoteza muda wako wa kuweza kutoa elimu kama hii ambayo watu husota nayo pale mweka. Wanaleta topic za ujinga!
Nauliza kwa nini simba has a akifugwa kwenye game Sanctuary hazai?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…