Katika mapenzi, uchawi na ulozi umegawanyika katika makundi makuu manne;
i. Uchawi wa kuanzisha uhusiano wa kimapenzi. Hapa ni pale inapotokea umempenda mtu lakini unaogopa kumwambia. Basi huwa kuna uchawi maalumu unao tumika hapa,unaye mpenda atakufuata mwenyewe.
ii. Kudumisha uhusiano wa kimapenzi. Hapa ni pale inapotokea kuwa tayari upo katika uhusiano wa kimapenzi na mtu lakini unataka kumfunga mtu huyo asitoke nje ya mahusiano na abaki na wewe tu. Hapa hutumika uchawi maalumu wa kuifunga nafsi ya mpenzi wako na kumfanya asitoke nje ya mahusiano hadi anaingia kaburini.
iii. Uchawi wa kumlinda mpenzi. Hapa ni pale unapotaka mpenzi wako asitoke kimapenzi na mtu mwingine yoyote Yule. Hufanyika uchawi maalumu wa kumfunga mpenzi wako na kumfanya asitoke kimapenzi na mtu mwingine yoyote yule.
iv. Kuharibu uhusiano wa kimapenzi. Hapa ni pale mtu unaye mpenda anapokuwa katika mahusiano ya kimapenzi na mtu mwingine. Basi hufanyika uchawi maalumu wa kutenganisha na kufarakanisha nafsi za watu hao wawili na kuwafanya wachukiane nakupotezeana kabisa.
Kama wanakaa mtaa mmoja, watakuwa wanapishana kama hawajuani vile. Maziwa, na majiya kichawi kutoka katika mojawapo ya mito saba ya kuzimu, ni baadhi ya dawa zinazo tumika katika uchawi huu. Maji hayo ya kuzimu ndio yanayo tumiwa na wachawi kuwanywesha misukule baada ya kuwachukua ili kuwafanya wasahau kuhusu maisha yao yaliyopita.