Kibo10
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 11,278
- 8,868
- Thread starter
- #21
Tatizo mara nyingi hizi hoja hujengwa upande mmoja. Juzi juzi kulikuwa na sifa za mwanaume anayefaa kuwa mume. Kama hizo ndio sifa za mwanamke, je huyo mwanaume anayetaka sifa hizo, yeye binafsi awe na sifa zipi? Au iandikwe wanandoa watarajiwa wawe na sifa zipi? Kibaya zaidi hata hizo zilizotajwa kila mtu ana tafsiri yake. Mfano mdogo - mwanamke mvumilivu ni yupi? Anayevumilia shida na raha katika ndoa, anayevumilia kipodo, anayevumilia michepuko ya mumewe?
Mkuu Tunajua kwamba maisha siku zote hayatabiriki, yanaweza kutokea matatizo ya kiafya ama kifedha.Huu ndio wakati wa kuona uvumilivu wa mtu.Kama mwanamke anatarajia kwamba siku zote ni za raha tu na pindi matatizo yanapotokea anachukua uamuzi wa kumtoroka mwanume, huyo siyo mwanamke wa kuoa.