Fahamu sayansi ya ufanyaji kazi wa uume na matatizo yanaweza kupelekea uwezo wa nguvu za kiume kupungua

Dr Norman

Member
Oct 6, 2019
11
40
Ufanyaji kazi wa uume unategemea ushirikiano wa vitu vinne katika usawaziko sawa; mfumo wa neva za fahamu, mfumo wa homoni, mfumo wa mishipa ya damu na mfumo wa akili na saikolojia.

Ili uume usimame na kuendelea kusimama tendo huamshwa na mfumo wa akili na taarifa husaifiri kupitia mfumo wa neva za fahamu, mishipa hutanuka na kujaa damu na uimara wa uume kusimama huendelea kuzingatia uwepo wa vichocheo vya homoni na utulivu wa saikolojia.

image.jpg

KUNA AINA TATU ZA MIITIKIO YA UUME KUSIMAMA

1. Uume kusimama kutokana na mwitikio wa kiakili/ kisaikolojia

Mwitikio huu huitwa Psychogenic Erection, taarifa zinazotoa amri uume usimame hutoka kwenye ubongo. Mwitikio huu sio wa hiari, mtu hawezi kuuzuia. Mwitikio huu hutokana na maono, sauti zinazosisimua kimapenzi. Mfano kutazama picha ya mapenzi, kuona mwanamke aliye uchi nk. Taarifa hii hutoka katika ubongo na kutembea kwenye uti wa mgongo hadi kwenye uume. Huamuru damu inayotembea kwenye mishipa ndani ya nyonga iende kwenye Uume na kujaza sponji maalum inayoitwa Corpus Carvenosa na Uume husimama.

Vijana au wanaume wa umri wa makamo hutegemea zaidi taarifa za picha, sauti ili kuamsha hisia za uume kusimama

2. Uume kusimama kutokana na mwitikio wa mguso (Tactile Reflex)

Mguso kwenye uume au eneo la siri hutuma taarifa kwa njia ya neva za fahamu hadi kwenye uti wa mgongo, usawa wa kiuno. Uti wa mgongo hutuma taarifa kusisimua mishipa ya damu ijaze damu kwenye uume na uume kusimama.

Uume wa watu wazima huitaji zaidi mwitikio wa mguso ili usimame zaidi ya maono au akili

3. Uume kusimama kutokana na kulala (Nocturnal Erections)

Mwanaume anapolala kwa usingizi mzima usiku uume husimama mara 3 hadi 4. Hali hii huanza kipindi cha balehe na huendelea hadi utu uzima. Kwa baadhi uume husimama hadi asubuhi, wengine hulala kabla ya kuamka

UMUHIMU WA MZUNGUKO BORA WA DAMU NA NITRIC OXIDE

Ili uume usimame vyema huitaji mfumo madhubuti wa mzunguko damu, uume una tishu maalum kama sponji ambazo hujaa damu na kufanya uwe mgumu.

Ndani ya chemba za damu za uume kuna kampaundi inayoitwa nitric oxide; uwepo wa kampaundi hii husaidia kutanua chemba za damu na kufanya uume usimame, Nitric Oxide huitaji uwepo wa hewa ya kutosha ya oksijeni

Ukosefu wa nitric oxide ya kutosha ndani ya chemba za uume husababisha kupungua kwa uwezo wa uume kusimama vyema. Tatizo hili huonekana zaidi kwa Wavuta sigara, wagonjwa wa kisukari na watu wenye upungufu wa homoni ya testosterone.

UMUHIMU WA HOMONI YA KIUME (TESTOSTERONE)

Homoni ya testosterone huchukua nafasi muhimu katika utendaji kazi wa viungo vya uzazi vya mwanaume. Upungufu mkubwa testosterone huchangia mwanaume kushindwa kusimamisha uume vyema kwa sababu huchochea ashiki ya mapenzi (libido) na huongeza nitric oxide katika chemba za uume

NB: Dawa kama Viagra hufanya kazi kwa kuongeza kiwango cha Nitric Oxide ndani ya chemba za uume

UMUHIMU WA HOMONI YA KIUME (TESTOSTERONE)

Homoni ya testosterone huchukua nafasi muhimu katika utendaji kazi wa viungo vya uzazi vya mwanaume. Upungufu mkubwa testosterone huchangia mwanaume kushindwa kusimamisha uume vyema kwa sababu huchochea ashiki ya mapenzi (libido) na huongeza nitric oxide katika chemba za uume

BAADHI YA SABABU AMBAZO HUCHANGIA KUPUNGUA KWA UWEZO WA UUME KUSIMAMA VYEMA

download (3).jpg

1. Magonjwa yanayoathiri neva za fahamu kama Kisukari, Ugonjwa wa parkinson nk
2. Baadhi ya dawa kama dawa za kutibu tezi dume, baadhi ya makundi ya dawa za presha,
3. Magonjwa ya Tishu - sponji ya uume kama ugonjwa wa Peyronie's
4. Matatizo ya kisaikolojia, msongo wa mawazo, woga
5. Athari za upasuaji maeneo ya nyonga kama upasuaji wa kuondoa tezi dume
6. Umri hasa baada ya miaka 60
7. Ugonjwa wa figo
8. Uvutaji sigara
9. Unene uliopitiliza huchangia mafuta kurundikana kwenye mishipa inayohudumia uume
 
Hapo kwenye mguso nakazia maarifa kabisa..
Majuzi kuna manzi kaja mbele yangu nilipoketi then akachukuwa kiti na kunisogelea zaidi huku miguu yake akiigusisha na yangu, sembuse nilivaa kaptula na ile miguu yake ya bia laini aisee nilijisikia utamu na kudinda hapohapo. Duuuh hatare jamani hizi hisia. Sema aliondoka muda si mrefu but without that hali ilikuwa inaelekea pabaya
 
Nilichogundua kuna baadhi ya dawa Pain killers zinasababisha less sensation kwenye uume na kusababisha kuchelewa kumwaga. Sababu zinapo fanya kazi kwenye nerves na ubongo kupunguza maumivu pia zinathiri neva za kwenye uume.
 
Hahaha kuna umri ukifika bila mguso gari haliwaki.

vijana uhitaji picha tu , ila wazee hadi starter ya kuguswa
 
Nilichogundua kuna baadhi ya dawa Pain killers zinasababisha less sensation kwenye uume na kusababisha kuchelewa kumwaga. Sababu zinapo fanya kazi kwenye nerves na ubongo kupunguza maumivu pia zinathiri neva za kwenye uume.

Kuna tofauti kubwa kati ya kushindwa kusimamisha uume (erectile dysfunction) na kuwahi kumwaga (premature ejaculation) , visababishi ni toauti na matibabu ni tofati.
 
Back
Top Bottom