KACHORI :
Mahitaji :
Viazi 1/2 kilo
Kotmiri ilokatwa katwa
Pilipili ya kijani 1 ilokatwa ndogo ndogo
Chumvi
Garam Masala kjk 1 cha chai
Manjano ya unga 1/2 kjk cha chai
Sukari kjk 1 cha chai
Tangawizi na kitunguu saumu kilichopondwa kjk 1 cha chai
Mchanganyiko wa kuchomea :
Unga wa dengu gramu.
Hamira ya soda/chapa ya maandazi kidogo .
Maji
Mafuta ya kukaangia
Maelekezo :
Kosha na chemsha viazi
Vikiwiva menya na uviponde kisha weka pilipili, kotmiri, Garam Masala, sukari, tangawizi na kitunguu saumu, chumvi na kamulia ndimu kisha changanya.
Mchanganyiko wa viazi utakuwa tayari.
Tengeneza maumbo ya mipira
MCHANGANYIKO WA UNGA:
Anza kwa kuweka unga wa dengu kwenye bakuli, kisha weka hamira ya soda na chumvi , changanya vizuri kisha weka maji kidogo
Tengeneza uji mzito kisha engeza maji uwe mwepesi kiasi
Weka mafuta jikoni yakipata moto chovya kachori kwenye mchanganyiko wa unga na uzikaange mpaka ziwe na rangi nzuri
Andaa kuliwa kwa chatine