Fahamu madhara ya uvutaji wa sigara.

Doctor Sebas

Member
Jul 19, 2017
30
125
Wavutaji sigara hupata magonjwa ya macho mara nyingi kuliko wasiovuta. Sehemu ya macho inayopitisha mwangaza inaweza kufichwa kama vile wingu linavyoficha jua(yaani kwa ikimombo) na kusababisha upofu.

Ugonjwa huu husababishwa kwa njia mbili. Kwanza moshi wa sigara huwasha macho na pili kemikali zilizo ndani ya sigara hupita kwenye mishipa , damu na hatimaye kudhuru macho. Sigara pia husababisha kudhoofika kwa sehemu ya kati ya macho( retina ) na hivyo kupunguza uwezo wa macho kuona vizuri na hata kutofautisha rangi( macular degeneration ).

3.Kukunjana kwa ngozi
Kemikali zinazopatikana ndani ya sigara hupunguza uwezo wa ngozi kujirekebisha hivi basi ngozi huzeeka haraka na kupoteza uwezo wa kulainika. Mvutaji wa sigara huonekana mzeee zaidi kuliko umri wake haswa.

4.Magonjwa ya masikio
Uvutaji sigara huleta magonjwa mengi ya masikio . Sababu ni kwamba uvutaji wa sigara husababisha uchafu kuganda kwenye mishipa ya damu na hivyo kupunguza mwendo wa damu hadi kwenye sehemu za ndani za masikio. Moshi na kemikali za tumbako pia hujeruhi sehemu za ndani za masikio na majeraha hayo yanaweza kuambukiza hata ubongo( menengitis ). Yote haya yanaweza kusababisha uziwi.

5.Saratani ya ngozi
Uvutaji sigara unasababisha saratani ya ngozi. Kemikali za sigara husababisha vidonda kwenye ngozi na ambavyo haviponi kwa urahisi. Baada ya muda hugeuka kuwa saratani .

6.Magonjwa ya meno
Sigara hutatiza mdomo na kuongeza uchafu unaoganda kwenye meno hivi kusababisha kuoza kwa meno, harufu mbaya mdomoni na uchafu wa meno. Sigara pia hutatiza kupona kwa vidonda hasa baada ya kung’olewa kwa jino. Saratani ya mdomo na ulimi inapatikana zaidi kwa wavutaji sigara na watumiaji wa tumbako za aina nyingine.

7.Magonjwa ya mapafu
Uvutaji wa siagara ndio sababu kubwa zaidi ya saratani ya mapafu. Pia husababisha kupasuka kwa vibofu vya hewa safi na kutoa harufu mbaya mwilini. Wavutaji pia hupata saratani ya koromeo na kuziba njia ya hewa na hivo basi inabidi kutobolewa kwa kishimo kwenye shingo hili kuwezesha mwadhiriwa kupumua.

8.Mifupa
Sigara inasababisha mifupa kuwa myepesi na kupunguza nguvu. Sababu ni kuwa kemikali zilizoko ndani ya sigara hupunguza uwezo wa mwili kujenga mifupa iliyo na nguvu. Mifupa kama hii huvunjika kwa urahisi na kuchukua muda mrefu sana(asilimia 80 zaidi ya mifupa ya kawaida)kupona.

9.Ugonjwa wa moyo
Sigara ndio sababu kubwa zaidi ya magonjwa ya moyo. Inasababisha moyo kupiga kwa kasi zaidi na hivyo kuongeza msukumo wa damu mwililni( high blood pressure ). Mwishowe husababisha mshtuko wa moyo na hata kifo.Moja kati ya kila vifo tatu ulimwenguni hutokana na magonjwa ya moyo na huua zaidi ya watu milioni moja kwenye nchi za Afrika.

10.Vidonda vya tumboni
Sigara hupunguza uwezo wa mwili kujikinga dhidi ya viini vinavvyosababisha vidonda tumboni. Pia hupunguza uwezo wa tumbo kustahimili nguvu ya asidi baada ya kula. Vidonda vya mvutaji basi huwa ni vigumu kutibu, na mara nyingi hutokea tena baada ya kupona.

11.Vidole
Kutu ya sigara hukusanyika na kuganda kwenye kucha na vidole vya mvutaji. Kisha hubadilisha rangi ya vidole na kucha kuwa za manjano au maji ya kunde. Ngozi ya vidole pia hukauka na kuwa ngumu sababu ya joto na kemikali za sigara.

12.Wanawake
Sigara huongeza hatari ya kupata saratani ya fuko la uzazi(cancer of theuterus ). NI vigumu zaidi kwa mwanamke mvutaji sigara kutungwa mimba na ni rahisi sana kwake kumpoteza mtoto katika mimba.( miscarrige ). Uvutaji wa sigara pia humfanya mwanamke kumzaa mtoto aliyekufa(stillbirth ) au aliye na uzito usiotimia wa kawaida. Watoto hawa huwa na afya duni baadaye. Sababu ni kuwa kemikali za sigara hupunguza mwendo wa mtoto kukua akiwa angali mimbani. Sigara pia husababisha ugumba( menopause ) kabla ya wakati wake. Sigara pia inaweza kumfanya mwanamke kuwa tasa.

13.Wanaume
Sigara inapunguza mpigo wa damu kwenye sehemu za uume. Sigara pia huharibu mbegu za wanaume na kwa hiyo watoto wanaowazalisha huwa na uwezekano mkubwa zaidi wa kupata magonjwa ya saratani. Sigara pia huwafanya wanaume kuwa tasa.

14.Magonjwa ya ngozi
Sigara huleta magonjwa mengi ya ngozi kama vile uvimbe, kuwashwawashwa na hudhoofisha hali ya ngozi.
15.Ugonjwa wa ‘Buerger’
Huu ni ugonjwa wa uvimbe kwenye mishipa ya damu ya miguuni na mikononi. Mishipa hii huzibika na kuzuia mwendo wa damu kwenye sehemu zilizoathirika. Isipotibiwa kwa haraka,mvutaji anaweza kukatwa miguu au mikono.

16.Saratani
Zaidi ya kemikali 40 zinazopatikana kwenye tumbako zimethibitishwa kusababisha saratani . Ukilinganisha na asiyevuta sigara :

16(a).Mapafu
Mvutaji ana uwezekano wa mara 22 zaidi wa kupata saratani ya mapafu

16(b).Pua
Mvutaji ana uwezekano wa mara 2 zaidi kupata saratani ya pua.

16(c).Ulimi
Mvutaji ana uwezekano wa mara 2 zaidi kupata saratani ya ulimi.

16(d).Tumbo
Mvutaji ana uwezekano wa kupata saratani ya tumbo mara 3 zaidi.

16(e).Figo
Mvutaji ana uwezekano wa kupata saratani ya figo mara 5 zaidi.
Saratani Zinginezo

Uchunguzi unaonyesha kuwa saratani ya mdomo ni hadi mara 27, koo(mara 12), koromeo(mara10).Uchunguzi pia umebaini kuwa kuna uhusiano fulani kati ya uvutaji sigara na saratani ya matiti.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Castr

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
19,714
2,000
Mvutaji wa sigara huonekana mzee....

Manji na mimi (sijawahi kuvuta sigara) mimi naonekana babu na kaniacha miaka mingi tu.
 

MZEE MKUBWA

JF-Expert Member
Jun 24, 2017
3,771
2,000
Ngumu kuelewa mzee wangu zaidi ya miaka ishirini anavuta sigara na bado yuko njema kiafya...
Tatizo ni afya ya mtu siyo sigara mkuu
 

Author

JF-Expert Member
Jan 24, 2014
1,320
2,000
Wajameni wana JF tujadili kwa pamoja...Hivi kuvuta sigara ni dhambi?
 

Odhiambo cairo

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
13,598
2,000
Mimi naamini maandiko ya Biblia "Mwili ni hekalu takatifu ya Mungu"
Sasa kuvuta sigara mwisho wake lazima uathiri mapafu (mwili). Lakini pia huufanya mwili u?ufanye kazi tofauti na asili yake.

Kwa hiyo jambo lolote linaloichafua hekalu la Mungu "mwili" ni dhambi .
 

k29

JF-Expert Member
Dec 14, 2014
682
1,000
Mimi naamini maandiko ya Biblia "Mwili ni hekalu takatifu ya Mungu"
Sasa kuvuta sigara mwisho wake lazima uathiri mapafu (mwili). Lakini pia huufanya mwili u?ufanye kazi tofauti na asili yake.

Kwa hiyo jambo lolote linaloichafua hekalu la Mungu "mwili" ni dhambi .

Vp kuhusu magonjwa yanayoharibu mwili kama, tb, cancer, na mengineyo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom