Fahamu kwanini Matajiri huendelea kuwa matajiri

Jumax

Senior Member
Mar 4, 2017
117
229
Habari za muda Great Thinkers,
Leo nimeona nilete elimu fupi juu ya makundi haya matatu ya watu waishio hapa ulimwenguni, ambao ni MATAJIRI (The rich), WATU WA MAISHA YA KATI (The middle class) na MASIKINI (The poor).

1.MATAJIRI
Nikianza na kundi hili, tafsiri halisi ya neno au kundi la watu hawa ni tofauti sana na mtazamo wa waliowengi. matajiri ni wale watu ambao humiliki Biashara kubwa au wamewekeza (invest) katika biashara kubwa na ambapo hupata pesa ikiwa wapo au hawapo eneo husika. Pia kwa tafsiri nyingine ni watu ambao pesa yao huwafanyia kazi au kuwaajiri watu wengine wawafanyie kazi. mfano; Bill gates, Aliko dangote, Mo dewji n.k (wawekezaji na wamiliki wa biashara kubwa)

2.WATU WA KIPATO CHA KATI
Hili ni kundi ambalo watu wengi hudhani kuwa ni matajiri lakini si kweli na hii yote ni kutokana na mwenendo na hali ya maisha ya watu hawa. Hapa nawazungumzia wale watu walio ajiriwa na kupokea mishahara minono, wamiliki wa biashara ndogo, na wale wenye taaaluma(specialists or talents) mbalimbali au kwa lugha nyepesi ni wale watu wanaotumia Muda, Nguvu na Akili zao kupata kipato yaani kama ikitokea mtu huyu hayupo eneo husika basi ndio unakuwa ukomo wa kupata kipato. mfano, wanamichezo, waajiriwa.

3.MASIKINI
Hapa tunawakuta wale wote ambao hushindwa kutimiza mahitaji muhimu katika maisha yao ikiwamo kula, kulala na hata mavazi yaani BASIC NEEDS kwa lugha ya kiingereza. Na maisha ya kundi hili mara yingi yamekuwa ni ya kukumbwa na simanzi, huzuni na kushindwa kupiga hatua kimaendeleo kutokana na sababu kadha wa kadha.

Vilevile ningependenda kugusia swali fupi ''Kwanini Matajiri wanazidi kuwa matajiri, Masikini wanazidi kuwa masikini na watu wa maisha ya kati wanabaki hapohapo walipo siku zote?''

''why the rich get richer, the poor get poorer and the middle class are getting squezed out?''

Siri kubwa hapa si kitu gani watu hawa hufanya bali ni kitu/vitu gani watu hawa hununua.

>>>>>>Nikianza na MATAJIRI kundi hili mara zote wamekuwa ni watu wa kununua vitegauchumi (assets) na ninaposema assets ama vitegauchumi simaanishi nyumba ya kuishi, magari au vitu vingine vya thamani bali ni vile vyote ambavyo ukinunua vinauwezo wa kukulipa (something that pays you money). Mfano nyumba kwa ajili ya biashara (real estate), gari kwa ajili ya biashara, Hisa (stocks), bond n.k

>>>>>>WATU WA MAISHA YA KATI (middle class) watu hawa hununua madeni yaani (LIABILITIES) ninaposema madeni ni kwamba watu hawa hununua vitu ambavyo hutoa pesa mifukoni mwao (somethings that cost money) mfano. gari la kutembelea, nyumba ya thamani ya kuishi, tena vile vile wengine hata hudiriki kuchukua mikopo bank ili wafanikishe hayo.

>>>>>>MASIKINI hawa siku zote hununua vitu ambavyo havina umuhimu sana maishani mwao.
ITAENDELEA...>>>>>>
 
tatizo kubwa ni kwamba wengi wetu hatujui kama dunia ishabadilisha utawala wa fedha tokea mwaka 1971 na sasa kuna utawala wa sarafu kwa kingereza ndio inaleta maana nzuri zaidi the rule of currency ambayo nikama electrical currency, yaana utawala wa sarafu inayozunguka, matajiri hawaweki fedha bali huzizungusha katika miradi mbalimbali, na sehem ambayo tajiri na masikini hukutana hua ni benki ambapo masikini au muajiriwa huenda kuweka au kutunza fedha zake kwakua hajui atazitumiaje wakati tajiri huenda kuchukua pesa hizo za masikini na daraja la kati kama mkopo kati yake yeye na benki kwakua anajua atazitumiaje katika miradi yake.
 
sehem ambayo tajiri na masikini hukutana hua ni benki ambapo masikini au muajiriwa huenda kuweka au kutunza fedha zake kwakua hajui atazitumiaje wakati tajiri huenda kuchukua pesa hizo za masikini na daraja la kati kama mkopo kati yake yeye na benki kwakua anajua atazitumiaje katika miradi yake.
Hakika

Hali hii ndio humfanya tajiri aendelee kuwa tajiri, na masikini kubakia kuwa masikini.
 
mkuu nimekua najiuliza maswali mengi, hivi utajiri unapimwa kwakua na pesa nyingi au ni spiritual thing? kwanini kuna watu wengine anaweza ishiwa fedha zote na miradi yote kufilisika ila baada ya muda flani anarudi kivingine na kua bora zaidi ya mwanzo? nadahani pia utajiri na umasikini unatokana na mindset ya mtu, unaweza kupewa pesa nyingi au kubahatika kurithi mali ila kama una poor mentality zitaisha tu na utarudi kwenye state yako tu.
nadhani somo la muhimu saana katika harakati za kuukimbia umasikini cha muhimu ni kuanza na kubadilisha mitazamo yetu dhidi ya umasikini na utajiri.
 
tatizo kubwa ni kwamba wengi wetu hatujui kama dunia ishabadilisha utawala wa fedha tokea mwaka 1971 na sasa kuna utawala wa sarafu kwa kingereza ndio inaleta maana nzuri zaidi the rule of currency ambayo nikama electrical currency, yaana utawala wa sarafu inayozunguka, matajiri hawaweki fedha bali huzizungusha katika miradi mbalimbali, na sehem ambayo tajiri na masikini hukutana hua ni benki ambapo masikini au muajiriwa huenda kuweka au kutunza fedha zake kwakua hajui atazitumiaje wakati tajiri huenda kuchukua pesa hizo za masikini na daraja la kati kama mkopo kati yake yeye na benki kwakua anajua atazitumiaje katika miradi yake.
Nakubaliana na wewe Mia kwa mia mkuu
 
mkuu nimekua najiuliza maswali mengi, hivi utajiri unapimwa kwakua na pesa nyingi au ni spiritual thing? kwanini kuna watu wengine anaweza ishiwa fedha zote na miradi yote kufilisika ila baada ya muda flani anarudi kivingine na kua bora zaidi ya mwanzo? nadahani pia utajiri na umasikini unatokana na mindset ya mtu, unaweza kupewa pesa nyingi au kubahatika kurithi mali ila kama una poor mentality zitaisha tu na utarudi kwenye state yako tu.
nadhani somo la muhimu saana katika harakati za kuukimbia umasikini cha muhimu ni kuanza na kubadilisha mitazamo yetu dhidi ya umasikini na utajiri.

Mkuu utajiri au umasikini WA mtu mtu huanza kwenye fikra(mindset) ya mtu huyo mf. Unaweza ukampokonya tajiri pesa zake zote na kumpa masikini lakin baada ya muda kadhaa huyo tajiri anaweza kurudi tena kuwa tajiri na kwa kuwa yule maskini Hana fikra pevu so within a shot time atarudi kwenye hali yk ile ile.
 
absolutely, upo sahihi, pia nimejifunza kua wengi wetu wanaishi bila kua na malengo wala kujua nini wanahitaji katika maisha, kuna mtu mmoja ni graduate wa sheria ila cha kushangaza alihangaika kutafuta kazi yoyote ili aweze ku survive na mwisho wa siku akaishia kua muhudumu wa super market, nikamuuliza sasa kwanini alipoteza miaka mi4 kusoma sheria? akaniambia kua alisoma kwakua alihisi akiwa mwanasheria atakua na maisha mazuri na matokeo yake kakwama na kushindwa kwenda law school ili afikie ndoto yake, pia vilevile mifumo ya elimu yetu inawaharibia watu wengi maisha kwa kuwafanya wawe watafutaji wa ajira baada ya watazamaji wa fursa na kuzifanyia kazi, mwisho wa siku tunakua na idadi kubwa ya watafuta ajira kuliko watengenezaji wa ajira wenyewe....

naamini umasikini wa mtu hauwezi isha kwa kutegemea mshahara kwakua kila mara mshahara hua hautoshi kutatua kero na mahitaji yote.
mimi naamini kila mtu ni mzuri na ana kipaji au uwezo flani wa kufanya kitu flani kwa ufanisi zaidi, ila tatizo mfumo wa malezi pamoja na elimu unawakaririsha watu kua bila kusoma sana na kuajiriwa na kulipwa mshahara hauwezi kua na maisha bora na matokeo yake imepelekea watu kurogana kugombania madaraka na kushinda kwa waganga ili ajira isiishe.

najiuliza kwanini mwanafunzi wa havard mark zukerberg alikataa ofa ya kuajiriwa na microsoft huku akiahidiwa mamilioni ya dola toka kwa bill gates na kuamua kukomaa na mradi wake wa face book? jibu ni lepesi sana aliisikia sauti ndani yake na kuifanyia kazi na matokeo yake leo ni kijana tajiri saana nadhani kuliko vijana wote wa umri wake.

kuna mtu mmoja aliwahi niuliza kwanini sitaki kuajiriwa na kwenda kufanya kazi kwenye taasisi yao? nikamjibu kua maisha ni kama maji na pia sisi nikama aina ya samaki, kuna vidagaa,samaki wa saizi ya kati na wale nyangumi sasa basi maji yangu ni marefu deep see, hivyo basi nitakomaa zaidi mpaka nifikie level ya maji yangu, na ujasiri huo niliupata baada ya kusoma vitabu vingi kama vile think and grow rich, retire young and retire rich, rich daddy and poor daddy, how to increase financial IQ na vinginevyo....
naendeleza mapambano huku nikiwa na imani kuu kua lazima nitafikia malengo yangu na kuacha legacy behind.

nachoamini ni kwamba kuzaliwa masikini sio kosa au uamuzi wa mtu bali kufa masikini ni maamuzi na makosa yetu yenyewe.
watu wengi wanafikiri utajiri ni lazima uwe na pesa kwanza kumbe unaanzia katika state of mind.
we become who we are from what we think.
nawasilisha.
 
mkuu nimekua najiuliza maswali mengi, hivi utajiri unapimwa kwakua na pesa nyingi au ni spiritual thing? kwanini kuna watu wengine anaweza ishiwa fedha zote na miradi yote kufilisika ila baada ya muda flani anarudi kivingine na kua bora zaidi ya mwanzo? nadahani pia utajiri na umasikini unatokana na mindset ya mtu, unaweza kupewa pesa nyingi au kubahatika kurithi mali ila kama una poor mentality zitaisha tu na utarudi kwenye state yako tu.
nadhani somo la muhimu saana katika harakati za kuukimbia umasikini cha muhimu ni kuanza na kubadilisha mitazamo yetu dhidi ya umasikini na utajiri.
Kuna jamaa alipata hela za mgao wa nyumba yao ya urithi kariakoo,yeye alipata mil 320.
Haujapita hata mwaka tangu achukue hizo hela,leo hii anaweka bondi simu kwa laki 1 tu.
Ni kweli ulivyosema ni mindset
 
Mimi kuna jamaa namfaham hapa A rush a nae kauza nyumba ya urithi 45ml. Haijapita hata mienzi 6 sahivi ameanza kuweka dhamani za ndani bond.
 
Na wakishakua na hizo,zikiondoka hupagawa.Huyu jamaa alipata za mgao wa familia kisha akapata za Udalali,waliuza nyumba Kariakoo,wenzie walichukua araund 250 mil,yeye 320
 
absolutely, upo sahihi, pia nimejifunza kua wengi wetu wanaishi bila kua na malengo wala kujua nini wanahitaji katika maisha, kuna mtu mmoja ni graduate wa sheria ila cha kushangaza alihangaika kutafuta kazi yoyote ili aweze ku survive na mwisho wa siku akaishia kua muhudumu wa super market, nikamuuliza sasa kwanini alipoteza miaka mi4 kusoma sheria? akaniambia kua alisoma kwakua alihisi akiwa mwanasheria atakua na maisha mazuri na matokeo yake kakwama na kushindwa kwenda law school ili afikie ndoto yake, pia vilevile mifumo ya elimu yetu inawaharibia watu wengi maisha kwa kuwafanya wawe watafutaji wa ajira baada ya watazamaji wa fursa na kuzifanyia kazi, mwisho wa siku tunakua na idadi kubwa ya watafuta ajira kuliko watengenezaji wa ajira wenyewe....

naamini umasikini wa mtu hauwezi isha kwa kutegemea mshahara kwakua kila mara mshahara hua hautoshi kutatua kero na mahitaji yote.
mimi naamini kila mtu ni mzuri na ana kipaji au uwezo flani wa kufanya kitu flani kwa ufanisi zaidi, ila tatizo mfumo wa malezi pamoja na elimu unawakaririsha watu kua bila kusoma sana na kuajiriwa na kulipwa mshahara hauwezi kua na maisha bora na matokeo yake imepelekea watu kurogana kugombania madaraka na kushinda kwa waganga ili ajira isiishe.

najiuliza kwanini mwanafunzi wa havard mark zukerberg alikataa ofa ya kuajiriwa na microsoft huku akiahidiwa mamilioni ya dola toka kwa bill gates na kuamua kukomaa na mradi wake wa face book? jibu ni lepesi sana aliisikia sauti ndani yake na kuifanyia kazi na matokeo yake leo ni kijana tajiri saana nadhani kuliko vijana wote wa umri wake.

kuna mtu mmoja aliwahi niuliza kwanini sitaki kuajiriwa na kwenda kufanya kazi kwenye taasisi yao? nikamjibu kua maisha ni kama maji na pia sisi nikama aina ya samaki, kuna vidagaa,samaki wa saizi ya kati na wale nyangumi sasa basi maji yangu ni marefu deep see, hivyo basi nitakomaa zaidi mpaka nifikie level ya maji yangu, na ujasiri huo niliupata baada ya kusoma vitabu vingi kama vile think and grow rich, retire young and retire rich, rich daddy and poor daddy, how to increase financial IQ na vinginevyo....
naendeleza mapambano huku nikiwa na imani kuu kua lazima nitafikia malengo yangu na kuacha legacy behind.

nachoamini ni kwamba kuzaliwa masikini sio kosa au uamuzi wa mtu bali kufa masikini ni maamuzi na makosa yetu yenyewe.
watu wengi wanafikiri utajiri ni lazima uwe na pesa kwanza kumbe unaanzia katika state of mind.
we become who we are from what we think.
nawasilisha.
Ahsante
 
Back
Top Bottom