Fahamu kuhusu Wabeba Majeneza wa Ghana

666 chata

JF-Expert Member
Mar 14, 2013
1,688
3,816
Kama ulikua kwenye mitandao kwa wiki mbili hizi kwa namna moja au nyingine basi utakua ulifurahishwa na kuchekeshwa sanaa na memes au video fupi za vitimbi vya jamaa kadhaa waliokua wanapata ajali mbali mbali alaf mwishoni linaonekana kundi la watu waliobeba jeneza na kucheza huku wakiwa katika mavazi nadhifu.

2017 BBC World iliwafanyia mahojiano jamaa hao ambao ni raia wa Ghana, maarufu kama Ghana's Dancing Pallbearers, mahojiano hayo yalihusu ni namna gani wao wanajisikia kufanya kazi hio ya kumtumbuiza marehemu akiwa ana enda kuzikwa na walipata wapi wazo ilo?

walisema mengi ikiwemo swala la wao kukosa ajira na kama vijana wakabuni wazo jipya na kisha kujiajiri kwa staili hio, walielezea pia namna walivyoanza kua maarufu nchini Ghana na shows mbali mbali kubwa za kimisiba walizo zipiga na namna walivyotengeneza pesa kwa ubunifu huo ambao haukuwai kutokea pengine kwa staili kama hio ya kwao.

Ndani ya wiki mbili jamaa wamekua maarufu sanaa duniani, vichekesho vilivyojumlisha picha na video zao zimetizamwa na mabilion ya watu na sasa wamekua maarufu sanaa pengine kuliko hata rais wa Ghana na wanamuziki wa nchi hio, ubunifu wao wa kucheza na jeneza umeonekana kuwafurahisha wengi.

ni wazi ubinifu hauna mipaka, na njaa ndio chanzo cha maarifa.
 

Attachments

  • VID-20200406-WA0015.mp4
    901.2 KB
  • adamchomvu___B-hbRDJDkMh___.mp4
    1.7 MB
  • adamchomvu___B-gjURYjm2D___.mp4
    1.3 MB
  • adamchomvu___B-hGlyPDJ0L___.mp4
    518.1 KB
  • VID-20200401-WA0029.mp4
    1,001.9 KB
  • VID-20200406-WA0015.mp4
    901.2 KB
  • IMG-20200405-WA0033.jpg
    IMG-20200405-WA0033.jpg
    30.5 KB · Views: 2
  • kamboyceogram___B-hiCUJgaao___.mp4
    1.1 MB
  • adamchomvu_2___B-h32J2jHpB___.mp4
    772.5 KB
Back
Top Bottom