SoC01 Fahamu kuhusu Nyayo za Kidigitali

Stories of Change - 2021 Competition

Faith Luvanga

Member
Aug 21, 2018
14
15
IMG_6949.jpg

Mtu yeyote anapokuwa kwenye mitandao ya kijamii hufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kutafuta, (Search) kupenda (like) au kusambaza (Share or Repost) kupakia ( upload) taarifa mbalimbali mtandaoni, ifahamike kuwa vitendo vyote hivyo hurekodiwa na vinaweza kutumika kukutathimini na kukujua wewe ni mtu wa aina gani.

Kitaalamu huitwa Nyayo za Kidigitali au #digitalfootprints hizi ni taarifa za kipekee zinazokusanywa kutoka kwa mtumiaji wa Mtandao anapofanya shughuli mbalimbali kwenye mtandao, anapofanya mawasiliano, miamala katika vifaa au majukwaa ya #mtandaoni

Taarifa hizi zinapoendelea kukaa bila kutolewa kwenye mtandao zinaweza kutumika kufuatilia vitu anavyofanya na kupendelea mtu anapokuwa mtandaoni. Aidha, ifahamike kuwa taaifa hizi zikisha wekwa mtandaoni husalia hapo kwa muda mrefu napengine zikawa ni za kudumu.

Inashariwa kuwa na nyayo za kidigitali zilizobeba taarifa chanya kukuhusu kwasababu taarifa hizo ndio hubeba uwakilishi wa wewe ni nani hasa katika mitandao ikitokea Mtu akakutafuta au akatafuta jina lako basi apate taarifa chanya kukuhusu

Kwa hiyo unaweza kuwa makini kwa kile unachofanya kwenye mitandao ya kijamii kwa kuweka vitu chanya zaidi kwani Digital footprint zinaweza kutumika kuamua hatma yako katika nyanja mbalimbali za Maisha. Mfano: Ajira kwa waajiri wanaweza kuzitumia kuamua kama wakuajiri au la, wasimamizi na watekelezaji wa sheria wanaweza kuzitumia, unapoomba Visa ya kuingia taifa tofauti na lako zinaweza pia kutumika kuamua kama upewe au unyimwe. kwasababu Nyayo ya kidijitali itakutambulisha kwa watu tabia na aina ya maisha yako.
IMG_6948.jpg
 
Back
Top Bottom