Fahamu kuhusu Biashara ya mkonge nchini Tanzania na Changamoto zake

RESEARCHER 1

Member
Nov 30, 2016
16
15
Kutokana na wadau wengi kutaka kujua hasa gharama za uzalishaji wa mkonge na muda gani unaaza kupata faida ikanilazimu niwaandalie hii bajeti ambayo tunaitumia kwa mkoa wa Tanga ila inaweza kubadilika kutokana na upatikanaji wa mahitaji na hali ya shamba ilivyo.


================== Ufafanuzi kutoka kwa wadau mbalimbali==============

1597988482862.pngKILIMO CHA MKONGE TANZANIA
Mkonge au Katani ni moja kati ya zao la biashara Jina la kisanyansi inaitwa Agave sisalana. Asili ya zao hili ni Mexico na baadae likasambaa katika nchi nyingine, kwa mara ya kwanza lilitambushwa katika nchi za kitropikia na subtropikia India,Tanzania, Brazil, Kenya south Africa, Angola, Mozambique Morocco Uganda, Zimbabwe na Mauritius.

Zao la mkonge liliingizwa nchini mwaka 1892 na mtaalamu wa kijerumani Dr. Richard Hindorff ambaye alikuwa ni mtafiti wa mimea na udongo. Mtaalamu huyo alichukua miche 1000 kutoka Pwani ya Mexico kwenye jimbo la Yuctan na kuisafisha kwa kupitia Frolida, Marekani na Humburg Ujerumani. Kati ya miche 1000, ni miche 62 tu ndiyo iliyofika Tanganyika na ilipandwa sehemu iitwayo Kikokwe huko Pangani Tanga.

Mkonge ulisambaa maeneo mengi ya Tanganyika mpaka kufikia mwanzoni mwa miaka 1960 Tanganyika ilikuwa inaongoza kwa uzalishaji wa mkonge ikifatiwa na Brazil na mexico kwa mauzo ya tani 230,000 kwa mwaka nje ya nchi. Kutokana na sababu mbalimbali zilizojitokeza miaka ya 1970 uzalishaji ulipungua toka tani 230,000 hadi tani 19,700 kwa mwaka 1997.

Hata ivyo mageuzi ya kiuchumi yaliyoanza miaka 1980 ambayo yalilenga katika ubinafisishaji na biashara huria , uhuru wa taasisi za kifedha za ndani na nje ya nchi yalifufua kilimo cha mkonge na hasa kukamilika kwa ubinafishaji mwaka 2005 uzalishaji umepanda hadi kufikia tani 40,000 mwaka 2015 hii inatokana na kuongezeka kwa mahitaji ya mkonge na bidhaa zake pamoja na kupanda bei kwenye soko la dunia pamoja na ndani.

Soko kuu la mkonge wa Tanzania ni china, Saudi Arabia , India, Uhispania, Ujerumani, Uingereza, Kenya, Uganda na Nigeria.

ZAO LA MKONGE

Kutokana na mabadiliko makubwa ya hali ya hewa kwa sasa wakulima wengi wamekuwa wakikosa mavuno kutokana na kutegemea mvua ambazo kwa sasa mtiririko wake siyo mzuri ivyo wataafiti wa mkonge wanahamasisha kilimo cha mkonge kwa wakulima wadogo nchi nzima ili zao litumike katika kuwaongezea wananchi kipato kutokana na sifa za mkonge kama zifuatazo;
- Zao la mkonge linavumilia sana ukame
- Ni zao ambalo halina msimu maalumu wa kupanda hivyo kupelekea kuweza kupandwa wakati wowote na pia halina wakati maalumu wa kuvunwa pale linapokuwa tayari kuvunwa
- Zao la mkonge linaweza kuchanganywa na mazao mengine ya msimu kama kunde, mahindi, maharage , alizeti, njegere na karanga.
- Ni zao ambalo halina uhaba wa vipando.
- Bidhaa zitokanazo na mkonge zinaweza kutumika katika tasnia ya kilimo, nishati, ujenzi, famasia, magari, meli, majumbani,ofisini na mazingira
- Mmea wa mkonge unaweza kuishi kwa kipindi cha miaka 10-25 hivyo kumuhakikishia mkulima kipato cha uhakika
- Mkonge ni zao linalo staimil magonjwa, wadudu na maguu na hata upungufu wa rutuba kwenye udongo.

UZALISHAJI WA MKONGE
Mambo yafuatayo ni yakuzingatia katika uzalishaji wa mkonge;
- Maandalizi ya miche bora ya mkonge
- Utunzaji wa vitalu vya mkonge
- Upandaji wa mkonge shambani
- Utunzaji wa mkonge shambani
- Kilimo mseto cha mkonge na mazao mengine yachakula

i) MAANDALIZI YA VITALU VYA MKONGE
Uchaguzi sahihi wa miche ya mkonge na maadalizi ya mazuri ya kitalu kwa ajili ya upandaji wa miche ya mkonge ni muhimu kwa ukuaji haraka na hatimaye utoaji wa mavuno bora na mengi ya zao la mkonge.
Kuna aina nne ya vipando vya mkonge;
• Vikonyo (bulbils) huota kwenye mlingoti baada ya maua ya mkonge kupukutika
• Machipukizi (suckers) huchipua kutoka kwenye mmea wa mkonge
• Miche inayozalishwe ndani ya maabara kwa njia ya tissue culture (mtc lab)
• Miche inayotokana na mizizi au tumba za mkonge huitwa rhizomes japo aina hii ya miche sasa hivi haitumiki sana hapa nchini.

II) UTUNZAJI WA VITALU VYA MKONGE
• Palizi – upaliliaji kwa jembe la mkono kwa kawaida palizi linaweza kufanyika mara 4-8 kutegemea na udongo.
- Upaliliaji kwa kutumia dawa za magugu mfano hy-varax hutumika sana kuzuia magugu katika bustani za mkonge huzuia uotaji wa magugu kwa muda wa miezi sita mfululizo ambayo utumika kwa kiasi cha kilo 4.5/ha nah ii dawa inashauriwa inyunyiziwe bustanini wakati udongo una unyevunyevu.
• Namna ya kurutubisha vitalu
- Taka za mkonge ( sisal waste)
- Mbolea ya chunvichunvi zenye kirutubisho cha nitrogen 30kg /ha kama CAN, SA, and UREA kwa kukuzia
- Mbolea aina ya potash kama MOP na DAP
- Wadudu na magonjwa ya mkonge kama tembo wa mkonge ( sisal weevil) na scale na magonjwa kama kuoza kwa mashina (bole rot) , ugonjwa wa pundamilia (zebra leaf rot) na ugonjwa wa mabaka kwenye majani (korogwe leaf sport)

iii) UPANDAJI WA MKONGE SHAMBANI
• Uchaguzi na upandaji wa miche ya kupanda (grading) ukubwa wa miche ya kupanda ni bora iwe na urefu kati ya sentimita 50 -70 na uzito kati ya kilo 2-4 miche ipangwe katika madaraja kufuatana na ukubwa
- Uchimbaji wa miche huchimbwa kwa kutumia jembe au sululu ili kitunguu (bole) kisikatwe ili kuepusha kushambuliwa na wadudu.
- Kutayarisha miche kwa kukata mizizi bila kuaribu shina na majani yaliyonyauka yaondolewe
- Upandaji wa kutumia machipukizi (suckers) ikusanywe kutoka katika mashamba yenye mkonge mdogo si zaidi ya mikato 2
- Kuligawa shamba katika maboma kwa ajili ya kupanda mkonge shambani

• Mifumo ya kupanda mkonge shambani
- Mstari mmoja (single row) kwa nafasi ya 3.5 x 0.75 mita
- Upandaji wa mistari miwili (double row ) upandaji huu miraba miwili huwekwa karibu ili kutoa nafasi pana kati ya miraba hiyo. Nafasi ya upandaji utegemea aina ya mkonge

  • Mkonge aina ya sisalana nafasi pana ni mita 3.5 na nafasi kati ya mistari miwili iliyo karibu ni mita 1 wakati nafasi kati ya mmea mmoja na mwingine ni setimita 90 (3.5 +1 x 0.9) mita. Hutoa mimea 5,000 kwa hekta.
  • Mkonge chotara (H.11648) nafasi pana ni mita 4 na nafasi kati ya mistari iliyo karibu ni 1 pia nafasi kati ya mmea mmoja na mwingine ni mita 1 (4 +1 x 1) mita. Upandaji huu utoa mimea 4,000 kwa hekta.
• Muda wa kupanda inashauriwa kupanda mkonge kabla mvua hazijaanza na mkonge upandwe kina cha sentimita 8 ardhini na kushindiliwa

iv) UTUNZAJI WA MKONGE SHAMBANI
Ili kupata mavuno mengi ni vyema kuzingatia yafuatayo
- Matumizi ya taka za mkonge (sisal waste) ili kuifadhi unyevunyevu na kurutubisha udongo.
- Matumizi ya chokaa (agriculture lime) ili kuongeza chachu pH mpaka 5.5-5.8 inayotakiwa na mkonge.
- Kuweka mbolea za chunvichunvi zenye kirutubisha cha nitrogeni mfano CAN UREA, potasiam na phosphorus kama MOP, TSP NA DAP.
- Udhibiti wa magugu ili kuepusha kutumia maji na virutubisho vinavyotakiwa kutumiwa na mmea. Kwakutumia njia zifuatazo;- kutumia jembe au nyengo, kutumia madawa mfano bromacil, kutumia jamii ya mikunde (cover crop) mfano tropical kudzu.

v) KILIMO MSETO CHA MKONGE NA MAZAO MENGINE YA CHAKULA
Eneo linalotumiwa kwa mkonge ni asilimia 60 na kiasi kilichosalia asilimia 40 hubaki tupu ivyo ni bora Kulima na mazao mengine faida za Kilimo mseto
- Kutumia ardhi kwa ufanisi
- Kuzalisha mazao Zaidi ya moja katika eneo hilo na kwa Gharama ndogo.
- Kwa kupanda mazao jamii ya kunde husaidia kuongeza rutuba ya udongo.
- Kupata Chakula hasa kwa wakulima wadogo na kwa mazao yanayofunika ardhi na kupunguza mmomonyoko wa ardhi kwa njia ya upepo na maji.

• Mazao yanayofaa kuchanganywa na mkonge maharage, kunde, karanga, soya, choroko alizeti, ufuta, mahindi nk
• Mazao yasiyofaa kuchanganywa na mkonge ni mazao ya kudumu kama migomba, minazi, mikorosho na michungwa mtama uwele viazi vitamu na mihogo

2. UVUNAJI WA MKONGE
i) Ukataji wa mkonge ili kupata singe mkonge uvunwa majani kwa kuzingatia yafuatayo
- Jani linalovunwa ni lazima liwe na urefu unaozidi sentimeta 90
- Ni lazima jani liwe na mwanguko usiozidi digrii 45%
- Ni lazima likatwe kwenye shingo yake
- Ni marufuku kukata kitunguu au mape
ii) Usombaji wa majani yaliyokatwa
iii) Usindikaji
iv) Kulainisha singa (brushing)
v) Kufunga mizingo kwenye press (pressing machine)
vi) Kupanga madaraja ya singa (grading) kwa kuangalia urefu wa singa narangi ya singa

Shukrani ka muandaaji MR. MBARAKA BATARE, MTAFITI WA MKONGE, ARI-MLINGANO TANGA TANZANI
==================

Tanzania ni miongoni mwa zenye hali ya hewa na mazingira bora, kwa uzalishaji wa mkonge ambao ni zao la biashara.

Kwa wastani, mkonge unaweza kuishi wastani wa kati ya miaka 13 hadi 14, majani yake yanaweza kufikia urefu wa futi 200 hadi 300 hutumika kutengeneza bidhaa mbalimbali kama vile kamba nene, magunia, heleni na mazuria.

Kadri miaka inavyosonga mbele, ndivyo zao hilo linakuwa linavyozidi kuongezeka thamani, kutokana na mahitaji yake kuongezeka kadri siku zinavyoongezeka, kulingana na maendeleo ya sayansi na teknolojia. Linazidi kuwa na thamani katika soko la kimataifa. Historia ya nchi inaonyesha kuwa mkonge umekuwa ukimwa kwa sehemu kubwa ta mikoa ya Morogoro na Tanga.

Wakati bado haijatoweka kabisa katika mikoa hiyo miwili, imeanza kuibuka tena kwa kasi katika wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, ambako kuna kilimo kilichopamba moto.
Kasi yake imefika hatua ya kuchukua sura ya kuchuana na pamba inayolimwa kwa wingi huko kama zao la biashara.

KUTOKA KWA WAKULIMA
Suzan Jinyange (53), ni mkulima wa katani na msindikaji wa zao hilo kutoka wilayani Kishapu.
Anasema mkonge umewaongezea mafanikio wakulima wilayani humo na anatoa mfano binafsi kwamba akiwa mama aliyeolewa na mwenye watoto sita, amejikita katika kilimo hicho tangu mwaka 2013.
“Nilikuwa nalima mazao ya kawaida, lakini nilipoanza kulima zao la mkonge na kusindika, nimepata mafanikio makubwa,” anasema.

Jinyange anasema kuwa amepanda robo tatu ya ekari za zao hilo na ananunua mkonge kwa wakulima wengine kiasi cha ekari mbili kwa ajili ya kusindika.

Anasema kwa mwaka ana uwezo wa kusindika tani 10 anazoziuza kwa kampuni za mkonge na bei yake kwa kilo ni kati ya Sh. 800 hadi Sh. 1,000 na uliosindikwa unafikia bei zaidi ya Sh. 1,200 hadi Sh. 1,300.
“Nalishukuru shirika la Oxfam kupitia miradi yao, kwani limetupatia elimu juu ya zao hili, kwa sababu ardhi yetu ni kame mno. Tulikuwa tunapata hasara na kujikuta maendeleo ya kiuchumi yanarudi nyuma kila siku,” anasema.

Mkulima huyo anasema utaratibu wa sasa, wanapopanda mikonge kati eneo la kati, huchanganya na mazao mengine kama vile mahindi, choroko na karanga. Jinyange anasema shirika hilo kupitia wataalamu wake, imembadilisha maisha kwa kumpatia mashine ya kusindika mkonge na elimu kuhusu kilimo hicho.

“Nimefanikiwa kununua mashamba, kusomesha watoto pamoja na kumuuguza mtoto wangu anayesumbuliwa na saratani ya mguu. “Nilikuwa sina meno yaling’oka, ila nilipata fedha za kununua meno bandia. Pia nimewaajiri vijana ambao wananisaidia shughuli zangu za kusindika mkonge,” anasema Jinyange.

Mshauri wa Mradi wa Mnyororo wa Zao la Mkonge kutoka shirika la Oxfam, Azimio Mbegu, anasema wamefanya uchambuzi wa chanzo cha mabadiliko ya tabianchi na zao la biashara litakalohimili hali hiyo.
Wakulima kwa kushirikiana na shirika hilo, wamekubaliana zao pekee linalohimili ukame ni mkonge, kwani halishambuliwi na magonjwa.

Kaimu Ofisa Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika wilayani Kishapu,Godwin Evarist, anasema Oxfam lilianza kazi katika wilaya hiyo mwaka 2009. Anasema ilianza shughuli zake katika vijiji 10 na baadaye ikavifikia vijiji 30, kwa lengo la kuelimisha jamii matumizi ya mkonge.

Evarist anasema mwanzoni walitumia mmea wa mkonge kuweka mpaka baina ya mashamba na sasa imepiga hatua na kuwa na hadhi ya zao la biashara. Hivi sasa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, imehamasika na imelichukua kuwa sehemu ya uchumi wa wilaya.

MIKAKATI YA MABORESHO
Katika bajeti ya mwaka wa fedha 2016/17, Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu imeingiza mkonge kwenye mpango mkakati wake, ikiwa ni hanzo cha ndani na imetenga bajeti ya Sh. milioni 200 kwa ajili ya kuendeleza zao hilo.

Kiasi hicho cha fedha kimedhamiriwa kuviwezesha vikundi vya kinamama kupata pembejeo na mitaji ya kuendeleza biashara zao. Changamoto inayotajwa kuwapo ni ubaba wa miche ya m ikonge na hivyo, imeanzishwa kitalu chenye miche 25 ya zao hilo.

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Hawa Ng’umbi anasema wilaya itahakikisha zao hilo linapewa kipaumbele, baada ya wakulima kubaini umuhimu wake katika kuwaongezea kipato.
Hawa anasema kupitia mikutano ya hadhara, wamekuwa wakihamasisha kulima mazao mengine, bila ya kusahau mkonge kwa kuwa linastahimili ukame.

“Kampeni ya uhamasishaji imeanza katika shule, kaya na kata kupanda mikonge ekari mbili. Lakini nilishukuru shirika la Oxfam, kwa kutoa elimu kwa wakulima ambao hivi sasa wamepata mafanikio ,”anasema.
 

Attachments

  • KILIMO CHA MKONGE 3.doc
    71.5 KB · Views: 546
NAPENDA KUWAKUMBUSHA WALE WADAU WA MKONGE NA WALE WANAOITAJI KUWEKEZA KWENYE MKONGE KUWA MSIMU WA MAANDALIZI YA SHAMBA KWA AJIRI YA KUPANDA MKONGE NI SASA NA KAMA UKUBAHATI KUPATA DARASA LETU LA KILIMO CHA MKONGE NA FAIDA ZAKE TAFADHARI WASILIANA NASI WATAFITI KUTOKA KITUO CHA UTAFITI MLINGANO IDARA YA MKONGE NA PIA TUNATOA HUDUMA YA KUPIMA VIRUTUBISHO KATIKA UDONGO KWA BEI NAFUU. WASILIANA NA;
BATARE 0717698998/0769323117
 
Hailipi hyo biashara
Bro hii biashara kwa sasa inalipa,mkonge unahitajika sana mashariki ya mbali na ya kati.Wachina wanausaka sana mkonge,ndio hutumika kutengenezea hata haya mabodi ya mabas,mfano mibas ya mwendo kasi ile ni mikonge tu ile ndo maana hata likikwaruzana na Bodaboda linaparaganyika,issue ni kujua soko ila Mkonge ni deal for now
 
UTAKUWA HUIJUI BUT WATU WENYE MAENDELEO TANGA NI WALE WANAJIUSISHA NA KILIMO CHA MKONGE
Ya nikweli inalipa jirani yangu amepanda huo mkonge yupo vizuri. Ananishauri namimi nipande mkonge tumepakana mipaka shambani NGOMENI UMBA tanga.
pia wanunuzi wahuo mkonge nawafahamu mpaka bei zao kulingana na ubora kama ni OG ipojuu kidogo.
 
Kanda ya ziwa hakuna wanunuz,je nikipanda nitauzia wapi hasa mvuno wa kwanza ambao mavuno mi machache?
 
KILIMO BORA CHA
KATANI AU MKONGE
KILIMO BORA CHA
KATANI AU MKONGE
:
UTANGULIZI
Katani ni moja kati ya
zao la biashara
Jina la kisanyansi
; Agave sisalana
Jina maalufu ; sisal au
katani
Asili ya zao hili
ni Mexico na baadae
likasambaa katika nchi
nyingine nyingi, kwa
mara ya kwanza
lilitambushwa katika
nchi za kitropikia na
subtropikia
India,Tanzania, Brazil,
Kenya south Africa,
Angola, Mozambique
Morocco Uganda,
Zimbabwe na
Mauritius na ni zao
ambalo hutumika sana
kutengenezea bidhaa
nyingi.
HALI YA HEWA
JOTO LIDI ; Katani
hukua vizuri katika
maeneo ya
kisubtropikia, yaani
hukua vizuri kwenye
maeneo ya joto yenye
joto kati ya 10-32 oC
na joto ya juu zaidi
inakua 30 hadi 40oC
na joto ya hali ya chini
zaidi ni 5oC.
MVUA ; Pia mvua
huchukua nafasi
muhimu katika kilimo
cha katani zao hili
huzaa vyema zaidi
katika maeneo yenye
mvua 500mm na zaidi
kwa mwaka na wastani
wa mvua 600mm hadi
1500mm na pia
huweza kukua kwenye
maeneo yenye mvua
chini ya hapo.
UDONGO ; Zao la
katani halibagui sana
udongo lakin hukua
vyema kweye maeneo
ambayo yana unyevu
wa kutosha na aina
nyingi za udongo isipo
kua udongo mfinyanzi
na pH 4.0 hadi 6.0 ni
muhimu.
MBEGU : Katani
hupandwa kwa
kutumia bulbils na
suckers
Suckers ; ni vile
ambavyo vinakua
karibu na mmea na
utokana na matokezi
(buds) na vinaweza
kuchukuliwa na
kupandwa moja kwa
moja shambani
Bulbils ; Pale katani
inapokua huzaa maua
katika mlingoti wake,
hivi huchukuliwa na
kupandwa katika kitalu
na watu wengi
hupenda kuaanda hivi
kwa kua hua na sifa
kamili kama ya mmea
ambao ni mzazi.
KUANDAA SHAMBA
Mfumo unao hitajika
ni ule wa mistari
miwili yaani double
rows.
Hivyo andaa shamba
kwa kulipalilia vizuri
na kuondo taka zote.
KUPANDA
Kama nilivyo sema
awali bulbils lazima
zipandwe kweye kitalu
kwanza vinapandwa
10cm x 10cm na
hukaa kwenye kitalu
kwa mda wa miezi 6
na baada ya hapo
huamishiwa tena
kwenye kitalu kikubwa
ambapo hupandwa
kwa 30cm x 30cm ,
Na baada ya miezi 12
hadi 18 mimea hua
tayari sasa
kwakupandwa katika
shamba kubwa na
nafasi kati ya mistari
hua ni 1 hadi 1.5 m
na 4 m na kina cha
kupanda mmea hua ni
3cm katika
kuhamishia shambani
mizizi midogo
pembeni ya mmea
hukatwa na majani ya
chini yanaweza
kuondolewa.
SISAL NURSERY
ESTABLISHMENT
MBOLEA
Mara nyingi katani hua
haiitaji sana mbolea
kwakua hua na urafiki
na mazingira pale
inapo pandwa kwenye
eneo jipya , lakini
inapo pandwa kwenye
eneo ambalo
limekwishatumika
mbolea huitajika ,
unaweza kutumia
UREA, lime ammonium
nitrate (LAN) na
superphosphate.
UMWAGILIAJI
Kilimo cha katani
hakihitaji umwagiliaji
kwa kua huhimili
ukame japo kua katika
kuprocess maji
hutumika sana.
UPALILIAJI
Kupalilia ni muhimu
sana ndani ya miaka
miwili ya mwanzo
yaani miaka 2 hadi 3
ni vyema sana
kupalilia baada ya
kuamishia katika
shamba kubwa
unaweza kutumia
jembe la mkono au
hata kemikali,
unaweza kuacha
magugu kukua wakati
wa mvua na ukaya
palilia wakati mvua
zimeisha
MAGONJWA NA
WADUDU WAALIBIFU
WADUDU
Weevil wa katani
nguruwe
nyani na sokwe
Unaweza kuuwa
wadudu kwa kutumia
viua dudu ambavyo
vimesajiliwa na
kwakulinda shamba ili
wanyama kama nyani
wasishambulie
shamba
MAGONJWA
Madoa ya majani
kuoza kwa mringoti
Unaweza kuzuia kwa
kuweka mbolea
ambazo zina calcium
na kwa kuweka
shamba safi na pia
tumia dawa za
kemikali
KUVUNA
Kuvunwa kwa mazao
inategemea na eneo,
kiasi cha mvua
udongo na hali ya
hewa, lakini kwa
kawaida katani
huvunwa kwa mara ya
kwanza kati ya miaka
3 hadi 4 baada ya
kupanda.
Mimea hua na majani
120 hadi 125 ambayo
hua na urefu wa 60
cm unatakiwa kuvuna
majani ambayo tu
yapo tayari .
Majani hua tayari pale
rangi inapo badilika
kutoka brown iliyo
koza hadi kua brown
iliyo pauka na majani
huvuna kwa interval
kwa maana hiyo
unaweza kuvuna
majani 25 kwa kila
mmea kwa mwaka.
 
Bongo ni maumivu...mostly katani inalimwa na processors wenyewe...out growers wanaishia kulaliwa
 
Assalam wakuu,
naomba msada wenu Kwa anae fahamu vizuri biashara ya mkonge,au mwenye uzoefu wa biashara hii anisaidie, maana Nataka kuifanya

NB:(yaani kuanzia kununua mkonge Kwa meta,uzalishaji wa brush/singa Hadi mauzo)
 
Assalam wakuu,
naomba msada wenu Kwa anae fahamu vizuri biashara ya mkonge,au mwenye uzoefu wa biashara hii anisaidie, maana Nataka kuifanya

NB:(yaani kuanzia kununua mkonge Kwa meta,uzalishaji wa brush/singa Hadi mauzo)
Nimeicopy mahali Twitter(Sirjeff)
UTAJIRI MKUBWA ULIOJIFICHA KATIKA ZAO LA BIASHARA LA MKONGE

Uzi utakua mrefu kidogo lkn nitajitahidi niufupishe sana lkn at the same time nihakikishe umejifunza vitu vyote.

Mara ya kwanza nilikua interested na mkonge ilikua May 2019, nilitenga miezi miwili ya kujifunza kila kitu. Then nikaanza rasmi kuifanya July 2019.

Mpk sasa nina experience ya mwaka mmoja ktk hii biashara. Na naweza kusema kwa ujasiri sana, hiki ni kilimo chenye pesa nyingi sn

Mara zote ukimsikia @moodewji anazungumzia kilimo biashara, kwa % kubwa hua anamaanisha Mkonge na Korosho

Mo Dewji ni mzalishaji mkubwa zaidi wa katani Afrika, katani anayoizalisha kwa mwaka km ikinyooshwa inaweza kuifunika dunia mara 4. Yeye anaiita 'Dhahabu Nyeupe'
Mwaka 2019 nilinunua hekta 10 za shamba la mkonge wa miaka mi3 kwa mil 20. Nikaliweka vzr nikachukilia mkopo bank wa mil 25.

Nikanunua mashine 2 ndogo za kuchakata mkonge kwa mil 5.2. Nikapata eneo kwa ajili ya uzalishaji na kujenga kanyumba ka wafanyakazi kwa mil 2.7

Pesa yote iliyobaki nikaingiza kwenye uzalishaji. Nanunua katani kutoka kwa wakulima wa nje ya ushirika, nachakata kwenye mashine zangu, naAdd value kwa kupiga 'Kayamba' na 'kupress' then nauza kwa tani kwa faida tamu sana (sweet profit).

Na hapa ndo uzi wetu unapoanzia

Ili kuzalisha Tani 1 ya katani utahitaji kuchakata 'Meta' 20 hadi 25 za mkonge

Meta 1 ni sawa na vifundo 110 vya katani, kifundo kimoja kina matawi 30 ya katani. Ni sahihi kusema meta 1 ni sawa na majani 3,300 ya katani

Toyo inabeba meta 1 ya katani

Sasa kuna mikonge ya aina 2;
i) Fundisha- Mkonge usio na uzalishaji mzuri, kwa sababu ya uchanga. Utahitaji meta 40+ kutoa tani 1 ya katani. Gharama yake ni Sh 8k - 10k

ii) Komavu- Mkonge wenye uzalishaji bora, umekomaa utahitaji max meta 25 kutoa tani 1. Gharama yake ni Sh 22K
Mimi hua nanunua 'Komavu' tu. Katani za 550K zinanipa tani 1

Process zote za uzalishaji, kukata, kusafirisha site kwangu, kuchakata, kutoa 'kinyero', kuosha na kukausha inanigharimu Sh 510K.

Mpaka hapo ninakua na tani1 ya katani iliyochakatwa (processed). Tunaiita 'brashi'

Kuna grades 2 za brashi
i) SS - Grade ya kati. Mpk kufikia hiyo stage ya Tweet ya juu tuna SS, Thamani yake ni ndogo ukiuza ktk hiyo stage tani ni 1,500,000 - 1,600,000

ii) UG- Grade ya juu. Ukiongezea thamani SS unapata UG. MeTL ya Mo wananunua tani ya UG kwa 3.3 - 3.5 mil

So, baada ya kupata SS km ilivyo kwenye picha hapo juu, nafunga brashi yng na kuipeleka kiwandani kuingezea thamani. Kuna process 2

i) Kayamba- Kuinyoosha katani, km dada zetu wanavyochana nywele. Tani 1 ni 180K

ii) Kupress- kuibana na kuifunga ktk marobota. Tani 1 ni 180K

NB: Ili kupata UG lazima uhakikishe uzalishaji wa brashi yako ni wa kiwango kizuri.

Brashi inabidi ioshwe mara 2 ili ipate kuwa nyeupe kabisa

Inabidi katani iwe ndefu na ikauke katika mazingira safi, bila kupata ukungu, au uvundo

Mpaka hapa ninakua na tani 1 ya UG ambayo gharama yake maximum baada ya kutoa kila kitu mpk usafiri ni 1.8 mil

Nikiiuza kwa mchina Mr. Chen ni 3.3mil, na nikiiuza kwa Mo Dewjo ni 3.5mil

NB. Mo Dewji ndani ya miaka hii miwili anaweza kuwa mzalishaji mkubwa zaidi duniani wa katan
Turudi kwenye production.

Mashine1 inazalisha tani 1 kwa wiki. Tuseme ni tani 4 kwa mwezi. Ukifanya vzr una uhakika wa 6mil kwa mashine 1

Mimi nilianza na mashine 2 miezi michache sn nyuma. Sasa hivi nina jumla ya mashine 5

Mkopo wa benki nimemaliza kuulipa mwezi uliopita
Sasa maybe ww hauna hela nyingi za kuanza km mimi nilivyoanza;

i) Si lazima uwe na shamba mkonge. Unaweza kununua kwa wakulima

ii) Si lazima uwe na mashine. Unaweza kuzikodi kwa watu

iii) Si lazima uwe na Toyo, unaweza kukodi

iv) Si lazima uwe na eneo la uzalishaji km mimi
So, probably faida yako inaweza kupungua kidogo bc utahitaji kulipia vitu vingi zaidi. Lkn ultimately faida utapata

Ni lazima ufanye research zako ujiridhishe vzr na numbers zako.

Sasa tuzungumze hbr ya changamoto
1. Hii biashara process zake ni NGUMU NGUMU mno. Yani ni labour intense
 
Nimeicopy mahali Twitter(Sirjeff)
UTAJIRI MKUBWA ULIOJIFICHA KATIKA ZAO LA BIASHARA LA MKONGE

Uzi utakua mrefu kidogo lkn nitajitahidi niufupishe sana lkn at the same time nihakikishe umejifunza vitu vyote.Mara ya kwanza nilikua interested na mkonge ilikua May 2019, nilitenga miezi miwili ya kujifunza kila kitu. Then nikaanza rasmi kuifanya July 2019.

Mpk sasa nina experience ya mwaka mmoja ktk hii biashara. Na naweza kusema kwa ujasiri sana, hiki ni kilimo chenye pesa nyingi sn

Mara zote ukimsikia @moodewji anazungumzia kilimo biashara, kwa % kubwa hua anamaanisha Mkonge na Korosho

Mo Dewji ni mzalishaji mkubwa zaidi wa katani Afrika, katani anayoizalisha kwa mwaka km ikinyooshwa inaweza kuifunika dunia mara 4. Yeye anaiita 'Dhahabu Nyeupe'
Mwaka 2019 nilinunua hekta 10 za shamba la mkonge wa miaka mi3 kwa mil 20. Nikaliweka vzr nikachukilia mkopo bank wa mil 25.

Nikanunua mashine 2 ndogo za kuchakata mkonge kwa mil 5.2. Nikapata eneo kwa ajili ya uzalishaji na kujenga kanyumba ka wafanyakazi kwa mil 2.7

Pesa yote iliyobaki nikaingiza kwenye uzalishaji. Nanunua katani kutoka kwa wakulima wa nje ya ushirika, nachakata kwenye mashine zangu, naAdd value kwa kupiga 'Kayamba' na 'kupress' then nauza kwa tani kwa faida tamu sana (sweet profit).

Na hapa ndo uzi wetu unapoanzia

Ili kuzalisha Tani 1 ya katani utahitaji kuchakata 'Meta' 20 hadi 25 za mkonge

Meta 1 ni sawa na vifundo 110 vya katani, kifundo kimoja kina matawi 30 ya katani. Ni sahihi kusema meta 1 ni sawa na majani 3,300 ya katani

Toyo inabeba meta 1 ya katani

Sasa kuna mikonge ya aina 2;
i) Fundisha- Mkonge usio na uzalishaji mzuri, kwa sababu ya uchanga. Utahitaji meta 40+ kutoa tani 1 ya katani. Gharama yake ni Sh 8k - 10k

ii) Komavu- Mkonge wenye uzalishaji bora, umekomaa utahitaji max meta 25 kutoa tani 1. Gharama yake ni Sh 22K
Mimi hua nanunua 'Komavu' tu. Katani za 550K zinanipa tani 1

Process zote za uzalishaji, kukata, kusafirisha site kwangu, kuchakata, kutoa 'kinyero', kuosha na kukausha inanigharimu Sh 510K.

Mpaka hapo ninakua na tani1 ya katani iliyochakatwa (processed). Tunaiita 'brashi'

Kuna grades 2 za brashi
i) SS - Grade ya kati. Mpk kufikia hiyo stage ya Tweet ya juu tuna SS, Thamani yake ni ndogo ukiuza ktk hiyo stage tani ni 1,500,000 - 1,600,000

ii) UG- Grade ya juu. Ukiongezea thamani SS unapata UG. MeTL ya Mo wananunua tani ya UG kwa 3.3 - 3.5 mil

So, baada ya kupata SS km ilivyo kwenye picha hapo juu, nafunga brashi yng na kuipeleka kiwandani kuingezea thamani. Kuna process 2

i) Kayamba- Kuinyoosha katani, km dada zetu wanavyochana nywele. Tani 1 ni 180K

ii) Kupress- kuibana na kuifunga ktk marobota. Tani 1 ni 180KNB: Ili kupata UG lazima uhakikishe uzalishaji wa brashi yako ni wa kiwango kizuri.

Brashi inabidi ioshwe mara 2 ili ipate kuwa nyeupe kabisa

Inabidi katani iwe ndefu na ikauke katika mazingira safi, bila kupata ukungu, au uvundo

Mpaka hapa ninakua na tani 1 ya UG ambayo gharama yake maximum baada ya kutoa kila kitu mpk usafiri ni 1.8 mil

Nikiiuza kwa mchina Mr. Chen ni 3.3mil, na nikiiuza kwa Mo Dewjo ni 3.5mil

NB. Mo Dewji ndani ya miaka hii miwili anaweza kuwa mzalishaji mkubwa zaidi duniani wa katan
Turudi kwenye production.

Mashine1 inazalisha tani 1 kwa wiki. Tuseme ni tani 4 kwa mwezi. Ukifanya vzr una uhakika wa 6mil kwa mashine 1

Mimi nilianza na mashine 2 miezi michache sn nyuma. Sasa hivi nina jumla ya mashine 5

Mkopo wa benki nimemaliza kuulipa mwezi uliopita
Sasa maybe ww hauna hela nyingi za kuanza km mimi nilivyoanza;

i) Si lazima uwe na shamba mkonge. Unaweza kununua kwa wakulima

ii) Si lazima uwe na mashine. Unaweza kuzikodi kwa watu

iii) Si lazima uwe na Toyo, unaweza kukodi

iv) Si lazima uwe na eneo la uzalishaji km mimi
So, probably faida yako inaweza kupungua kidogo bc utahitaji kulipia vitu vingi zaidi. Lkn ultimately faida utapata

Ni lazima ufanye research zako ujiridhishe vzr na numbers zako.

Sasa tuzungumze hbr ya changamoto
1. Hii biashara process zake ni NGUMU NGUMU mno. Yani ni labour intense
. Hii biashara process zake ni NGUMU NGUMU mno. Yani ni labour intense sn, sijawahi kuona kilimo biashara kinachohitaji nguvu kubwa zaidi ya hii

2. Mashine moja tu inahitaji wafanyakazi 10 - 11. So machine 5 nahitaji kuSupervise watu 50.Na waTanga mnawajua, waPwani km waPwani
3. Kuna chances za kuibiwa km huna usimamizi mzuri. Km ilivyo biashara nyingine yyt, lazima uwe guru wa management & team building

4. Ukijichanganya ukauziwa mkonge wa mkulima wa ushirika, sheria ni unanyea debe mwaka m1

5. Changamoto zingine ni sawa na biashara zote
Faida 1 kubwa

Zalisha uzalishavyo hata ufanyaje huwezi kukosa mnunuzi yani kuna Mo, kuna Mr. Chen na Kuna Mnaijeria wote wanakupigia makoti uwauzie. Soko la dunia wao wanauza tani 1 kwa mil5

Mo akisema kilimo ni industry ya kuprint utajiri sasa nadhani unaelewa anachomaanisha
Sijui km nimegusia kila kitu, km kuna chochote nimesahau kuna watu humu pia wanaijua katani wataeleza, pia unaweza kuuliza swali, nikipata muda nitajibu au nitaongeza nyama kwenye YouTube video zinazopandishaga kwa channel yng.

Have a blessed week!
IMG_20200714_103610.jpg
 
Back
Top Bottom