Fahamu kuhusu Biashara ya mkonge nchini Tanzania na Changamoto zake

Mwishoni mwa mwaka 2018 nilisoma andiko la Mr Mbaraka (Mtafiti wa Mkonge) ambalo liko kwenye uzi huu. Nilipendezewa nalo na kumpigia Simu. Akanielekeza sehemu ya kupata miche. Nikaenda Mlingano Tanga kupata picha ambayo nilipanda shambani kwangu Morogoro. Niliongezea na miche mingine kutoka katika shamba la Mkonge la Morogoro hapo Mkambalani (Mikese). Kwa kweli baada ya mwaka na miezi Kama 8 shamba langu linaonyesha matumaini na Nina nia ya kuongeza shamba. Lengo langu nikifishe walau hekita 40 kwa miaka 2 ijayo.

View attachment 1633420
hongera sana mkuu.. Na karibu sana kwenye kilimo cha mkonge
 
Vijana tuchangamkie hiki kilimo kinaweza kuwa mkombozi. Nasikia wakulima wa korosho wanalalamikia ukosefu wa magunia wakati mwingine. Tukiwa na Mkonge wa kutosha hili tatizo kitaisha maana tunaweza kuingia katika kutengeneza magunia zaidi kwa ajili ya korosho na mazao mengine.
Ni vijana wa mjini ambao hawawezi kuchangamkia furusa hii, je hao wengine wanaipataje aridhi?
 
Ni vijana wa mjini ambao hawawezi kuchangamkia furusa hii, je hao wengine wanaipataje aridhi?
Tanzania bado tuna ardhi kubwa sana sana. Tatizo la watu wengi wanapenda maeneo ambayo ni karibu na mijini. Kuna maeneo Tanzania ukienda hata hununui ardhi, serikali ya kijiji inakupatia ardhi, juhudi zako ni kusafisha hiyo ardhi na kuanza kulima.
Kukosa ardhi huwa siamini kama ni kikwazo.
 
Ni mkoa upi huo nije nilime miti ya matunda?
 
Naomba nijuwe mkonge ukishailima inaweza ikadumu kwa miaka mingapi ndo inakufa?

Miaka mingi. Mkonge ukifika ukomo hutoa mlingoti, ila pembeni kutakuwa na maotea hivyo basi like otea ambalo lipo karibu na mkonge ulioota lingoti litashika nafasi na lile la mlingoti unalikata. Unaweza kaa hata miaka mingi ni utunzaji tu.
 
lipo hekta 12 sawa na ekari 30..mill 48.
Huwa hayapatikani kama ulivyodai, mara nyingi watu hupanda wenyewe na maeneo kupata ckuiz ni ngumu...Ni kama bahati juzi kupata mtu anayeuza shamba lake maeneo ya korogwe ..ukitaka namba sema nikupatie
Inamaana hakuna mapori huko ya kununua na kufyeka mwenyewe? Mapori yote Tanga yamekwisha, sivyo?
 
Wilaya gani naweza kupata mashamba huko Tanga kwaajili ya kilimo cha mkonge? Bei ya shamba kwa ekari moja ikoje huko? Asante

kwa sasa kwa maeneo kongwe kama Korogwe inakuwa ngumu kidogo. Japo ukibahatisha wewaza kupata. Na ni kwa bei ambayo imechangamka.

Watu wengi kwa sasa wanaenda handeni mana bei iko chini, kwa ekari unaweza pata hata kwa laki moja (hii ilikuwa mwaka jana) huenda bei ikawa imepanda zaidi mana watu wengi wanakimbilia huko.
 
Mkuu,ni korogwe mpaka magoma huko kwa mandondo maeneo hayapatikani?
 
Mkuu,ni korogwe mpaka magoma huko kwa mandondo maeneo hayapatikani?

Mkuu,ni korogwe mpaka magoma huko kwa mandondo maeneo hayapatikani?

magoma ndo usiguse kabisa maana mkonge wenye singa nzuri Tanzania unatokea magoma na ni sehemu yenye mkonge mwingi mno ikifuatiwa na hale. Magoma, kwamandondo, mashewa mpaka mavovo, maramba yote wameshaamka. bora maeneo ya matarawanda, makorora, mahenge na kwamndolwa unaweza pata marneo. kwa magoma ni ngumu mno na ukipata bei itakuwa ya juu mno.
 
Vipi na biashara na kilimo cha viungo Tanga
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom