Fahamu Kodi ya zuio ni nini?

AmbaB

Member
Sep 1, 2016
51
27
KODI YA ZUIO NI NINI?

(Withholding Tax) Ni kiasi kinachokatwa wakati malipo yanapofanyika kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.

"Eng Evans amepanga nyumba kwa Bw. Noah kwa ajiri ya kufungua ofisi ya BIASHARA ya mambo ya ujenzi (Civil). Wamekubaliana kulipa Tsh. 1200,000 (kodi ya zuio) kwa mwaka, Evans atalipa siku ya 02/03/2020. Eng Evans(Withholding agent) atamlipa Bwana Noah, Landlord( Withholdee) Tsh. 1,080,000 na kisha kutakiwa kuhold Tsh 120,000 ambayo atailipa TRA kabla ya au tar 07/04/2020. Na kisha kutakiwa kufaili malipo yote yanayohusiana na zuio kabla ya au tar 30/07/2020. (Zaidi, Eng Evans atalipia 1% ya Tsh 1200,000 kama kodi ya stamp (Stamp duty) ndani ya mwaka mzima.)"

Hiki ni kiasi ambacho hukatwa wakati mlipaji anamlipa mlipwaji. Kiasi hiki kinachokatwa hulipwa serikalini kwa muda maalumu baada ya kukatwa kwenye malipo ya mlipwaji.

Kodi ya zuio hutegemea inatoka kwa nani, kama inatoka kwa mwajiri(P.A.Y.E) hukatwa kwenye malipo ya mwezi ya mwajiriwa kulingana na kiwango kilichoainishwa kwenye sheria ya mapato, shejo ya kwanza (first schedule) na mwajiriwa hupata kiasi kinachobaki (Net salary) baada ya makato na inategemeana pia anamakato mengine kama NSSF,PSSSF nakadharika.

Halikadharika kwa upande wa mfanyabiashara wakati wa ulipaji malipo ya pango ya nyumba, hutakiwa kuzuia kiasi fulani,(10%), kutoka kwenye jumla ya malipo ya kodi, na kukiwasilisha kwenye mamlaka ya mapato(TRA), kiasi kinachobaki ndicho hupewa mwenye nyumba.

Mamlaka imeona ni vema kodi ya zuio izuiwe na mlipaji(withholding agent) kabla ya mlipwaji(withholdee)hajapata malipo yake, maana yake ni kuwa mlipwaji akipata pesa yote anaweza asiwasilishe malipo serikali kwa muda husika,akashikwa na tamaa akala.

Sheria inatutaka kulipa kodi hii ndani ya siku saba za kazi baada ya kufunga mwezi wa malipo, kama malipo yalifanyika tar 12 mwezi Agost, basi kabla ya au tar 7 sept kiasi hiki kiwe kimelipwa TRA. Na kufaili ndani ya siku 30 baada ya kuisha kwa miezi sita ya mwaka wa mapato.

Hivyo basi kiwango cha malipo hutegemea kinatoka(kinakatwa)kwenye malipo ya nani? Ama malipo ya nini?Tazama Jedwali pichani.

Kodi ya zuio HAIKATWI kwenye malipo ya mtu ambaye hafanyi biashara(Shall not apply to payment made by individual Unless made in conducting business).Na kwa malipo yaliyopewa msamaha(Tazama jedwari). ITA 2004 as at 1/7/2020.

Pande zote zinawajibika kisheria endapo kodi ya zuio haijalipwa kwenye malipo yalifanyika baina ya pande husika. Na mlipaji atawajibika kama hajaweza kufaili ndani ya siku 30 baada ya miezi sita kuisha.(active self assessment)

NB: Ni muhimu pande zote mbili mkakubaliana mapema namna na kiwango cha kulipa, maana mnaweza shikana mashati pale ambapo mwenye mali anataka isiyokatwa.

Na Ambangile.

IMG_20200814_140129_093.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vitu hivi lissu anakufundisha unaelewa vizurii sana kuliko wengine wasiojua sheria
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom