Fahamu kisa cha huyu binti kujinyonga

Fahamu kisa cha huyu binti kujinyonga

kuna wakati yakikuelemea unajikuta ujinga ndio suluhisho pekee. Kila mmoja anapenda kuishi, mpaka mtu akichukua uhai wake elewa yalomsibu ni makubwa. Cha kuomba Mungu ni kukupa ujasiri wa kukabiliana na chochote kitakachokusibu.
Ni kweli mkuu yaani kuna watu wakimwona mtu amejinyonga wanamwona kama mjinga flani wanasahau pamoja na kwamba tuna akili lakini tukivurugwa na kama tukikosa watu wa kutuweka sawa akili zinahama na kufanya mambo ya ajabu..kwa ambayo nyoyo zao ni za kukata tamaa na bahati mbaya wakakosa watu wa kuwatia moyo ndio hao "wanajinyonga", na kuna ambao wenye ujasiri uliopitiliza atamtafuta mwanaume na kulipa kisasi either kufanya mauaji ama fujo n.k...na wengine (kimsingi ndio wengi) watatoa maneno mabaya na matusi ya kila aina kwa yule mwanamume (haya yote ni kuvurugwa tu sema vitendo vinavyotokea vinakuwa vina uzito tofauti lakini mwisho wa siku wote wamevurugwa)
 
Hapa tuzungumzie mtu kuvua pichu kwa hiari yake halafu baadae kusema aasahhh bahati mbaya n.k mengine ni matokeo
 
Asante kwa ujumbe mzito. Pamoja na hayo mimi ni Baba wa mabinti sina mtoto wa kiume. Hii dhana ya mimba za bahati mbaya naona inaanza kutumika vibaya.
Tuwe wakweli kwa pande zote.
Ungefafanua labda ningekuelewa, maana ninavyojua mimi neno bahati mbaya ni kitu kutokea bila kupanga hata kama unafanya kitendo chenye mazingira hatarishi.
 
Ungefafanua labda ningekuelewa, maana ninavyojua mimi neno bahati mbaya ni kitu kutokea bila kupanga hata kama unafanya kitendo chenye mazingira hatarishi.
Angefafanua mtoa mada maana neno bahati mbaya kwa kisa hiki kalileta yeye
 
Ha ha usinichekeshe sasa kujamiana tuuingize katiks "mazingira hatarishi"
 
Mapenzi acha yaitwe mapenzi ni tatizo kubwa..lakini pia hii huenda ikawa siri ya mtungi....
 
Nadhani mnakumbuka kisa cha huyu binti ambaye kwa sasa ni marehemu RIP aliyejinyonga akiwa chuoni Iringa?
Huyu binti ni mmojawapo wa wahanga wa mimba za bahati mbaya? Mimba kabla ya ndoa... Lakini aliweza kuhimili kwa kupitia magumu yote mpaka kujifungua na hatimaye baada ya muda kuweza kuendelea na masomo yake ngazi ya chuo...
Kwa jinsi inavyosemwa mahusiano yaliyozaa mimba na hatimaye mtoto hayakuwa endelevu... Lakini binti akawa ana faraja kwa kuwa na mtoto mzuri wa kiume asiye na tatizo lolote....
Matendo ya Mungu si ya mwanadamu.... Mtoto yule mzuri akatwaliwa na Bwana mwezi March mwaka huu akiwa na miaka 3... Jiweke kwenye nafasi ya huyu binti... Uyaone maumivu yake... Lakini mbaya zaidi, baba mtoto kwa sababu zisizojulikana hakufika msibani wala hakuhudhuria mazishi ya mwanae... Ikawa ni maumivu juu ya maumivu kwa mama wa mtoto.... Ila akafarijiwa na kufarijika kuwa hili nalo litapita!

Ikiwa ni chini ya siku 40 tangu msiba... Likatokea lingine kubwa zaidi na lililomuongezea maumivu mama mtoto marehemu..... Mzazi mwenzie yule aliyeshindwa hata kufika kaburini kwa mwanae akaoa / akafunga ndoa na mwanamke mwingine tena kwa sherehe!
Kumbuka mtoto alifariki March kwahiyo kwa vyovyote baba alioa mwezi April..... Compressed inner pains were too heavy to bear.... Mama mtoto marehemu akaamua kuchukua uamuzi aliochukua
Wote hawa sasa ni marehemu.... My apology kama picha zinakwaza ama kwa namna yoyote zitaleta maumivu kwa wengine View attachment 772106View attachment 772117
We are all part n parcel of great thinking.... In this case great thinkers.... Penye kasoro lazima parekebishwe huku msingi wa kasoro ukibaki vile vile ile kuweza kuleta uhalisia na ulinganifu wa masahihisho husika....

Mlengwa katika mada hii alikuwa ni mwanachuo Arusha... Sio Iringa na alikuwa yatima... Background yake ya kuwa yatima sio muhimu sana hapa
Tangu baada ya kifo cha mwanae alishafanya majaribio mawili ya kujiua akiwa nyumbani Moro... Yote mawili yalifeli ama kwa kuokolewa ama vinginevyo... Jaribio la tatu lililofanikiwa ni hili la kujinyonga chuoni
Mimba iliyozaa mtoto aliyekuja kufariki ilikuwa ya mume wa mtu ambaye hata hivyo aliikana na hata mazishi hakuhudhuria... Walikuwa wanaishi mtaa mmoja.... Na hili la baba mtoto allilifanya siri mpaka mtoto alipofariki....
Nimeona ni vema kuweka ufafanuzi huu kwa nia njema na kutenda haki
 
Ukimya ni mbaya sana
Wapiga kelele huishi tu
Hupata muda kujadili
Hupata ufumbuzi wake
Hujikomboa na mabaya
Mawazo kukata tamaa
Naamini ukimya mbaya

Bazazi
Kabisa Mkuu, Kuficha Ni Kubaya Sana
 
Nakumbuka Nililetaga Uzi wa Kutamani Kujiua Humu, Wapo Walionikebehi, Ila Kuna Waliosaidia Mno, Watu Wanahisi Hivi Vitu ni Kama Filamu, Ila Ni Halisi, Yanatokea, "MUNGU AWABARIKI All GREAT THINKERS'
 
Ukimya ni mbaya sana
Wapiga kelele huishi tu
Hupata muda kujadili
Hupata ufumbuzi wake
Hujikomboa na mabaya
Mawazo kukata tamaa
Naamini ukimya mbaya

Bazazi
Kwel kabisa mkuu kukaa kimya ni sumu kubwa inayoua taratibu
 
Mapenzi ya ujanani hayana tafakuri ya matokeo na yajayo.... Na wengine hudanganywa ama kudanganyika... Dhana ya bahati mbaya ni matokeo ya kufanya kitu bila kupanga
So sad
Nini kilisababisha kifo cha mtoto?
Bwana harusi na Bibi harusi mpya yanayokuja mbele yao ni magumu
Roho ya mtu hunena kama ulimi unenavyo
 
Kujinyonga iwe ni kwa sababu yeyote ile ni ujinga na upumbavu wa kupitiliza. Kila Mwanadamu anapaswa kutambua kuwa hakujileta hapa duniani kwa hiari yake mwenyewe na hivyo pia hawezi kujiondoa hapa duniani kwa hiari yake mwenyewe.

Hata kama mambo ni magumu kiasi gani, unakomaa nayo hivyo hivyo na siku ya kuondoka ikifika, basi unaondoka, lakini siyo kwa kujiua.
 
So sad
Nini kilisababisha kifo cha mtoto?
Bwana harusi na Bibi harusi mpya yanayokuja mbele yao ni magumu
Roho ya mtu hunena kama ulimi unenavyo
Hakuna kitu kama hicho. Bwana harusi na bibi harusi wao wana kosa gani?? Huyu kajinyonga kwa upumbavu wake mwenyewe, na kama kosa ni kuachwa na huyo bwana wake, na yeye angeendelea kusoma, kisha atafute wa kumuoa na kuanza maisha yake upya, na siyo kujinyonga na kuacha laana za kipumbavu kwa watu waliochagua kuishi.

Hata siku moja laana ya mpumbavu haimpati mtu.
 
Back
Top Bottom