Fahamu jinsi magonjwa yanavyotengenezwa maabara na kuua watu (bioterrorism)

DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
40,495
99,292
Hii ni njia ya kuachia virusi, bacteria au fangasi kwenye jamii ya watu, mazao au mifugo ili kuweza kuwaambukiza kwa makusudi ugonjwa fulani na kuua kila kitu chenye uhai kwenye sura ya ardhi.

Hii inawezekana kwa kutumia mabomu maalumu, chakula, maji, dawa za kupuliza na kuchoma sindano.

Silaha hizi ni moja ya silaha hatari zaidi duniani kwani zikitupwa sehemu zinahakikisha hakuna uhai unaobaki, hata samaki na wadudu wa kwenye maji hufariki.

Kumekua na tetesi nyingi sana kwamba huenda ugonjwa wa corona virus umetengenezwa makusudi kuua watu au umewaponyoka maabara lakini hakuna ushahidi wa kutosha japokua hatuwezi kupinga kwani hilo linawezekana kwa asilimia mia moja na historia ya dunia imeonyesha mataifa yalioyofanya hivyo wakati wa vita Fulani Fulani.

magonjwa haya yanatengenezwa vipi?
Gene therapy ni teknolojia ambayo ililetwa mahususi kwa ajili ya kutumika kusaidia kutibu magonjwa kama siko seli, saratani, kisukari, magonjwa ya moyo, magonjwa ya kuvuja damu na hata ukimwi kwa kubadilisha vimelea au gene ambazo zinachochea magonjwa hayo na kuweka gene mpya ambazo zinazuia magonjwa hayo.

Mpaka sasa hivi wagonjwa wengi wamefaidika na teknolojia hiyo lakini ka upande wa pili teknolojia hiyo inatumika vibaya kutengeneza magonjwa hatari na ya kutisha.

Wanasayansi huchukua vimelea au DNA ya bacteria, virusi au fangasi kisha hutengeneza wadudu wengine wengi wa aina hiyo hiyo kitaalamu kama cloning kisha huwabadilisha maumbile wadudu hao na kuwafanya wasiweze kutibika na dawa zilizopo.

mfano kama bacteria Fulani alikua na uwezo wa kutibiwa kwa kuharibu gamba lake la nje kitaalamu kama cell wall basi gamba lile huondolewa kwa teknolojia ya gene therapy na kumfanya bacteria yule kushindwa kutibika.

kwanini corona virusi haitibiki sasa hivi?
Ugonjwa wa corona ulikuepo tangu mwaka 1960, na ulikua sio ugonjwa hatari lakini ghafla ulibadilika mwaka 2019 na kua ugonjwa tishio kitu ambacho kinaleta mashaka kwamba huenda virusi hao wamebadilishwa na kuongezewa nguvu maabara.

Mpaka sasa hivi hakuna mtu aliyekubali kuhusika na ugonjwa huo japokua kuna mashaka kwamba ugonjwa huu umetengenezwa.

Nchi ambazo zilitengeneza magonjwa kwenye historia ya dunia.
Mwaka 1944 wakati ya vita kuu ya pili ya dunia nchi za marekani, uingereza, urusi, china na wenzake walitengeneza maabara kubwa za kutengeneza bacteria wa anthrax, brucellosis, na sumu botulism kwa ajili ya kupambana na wapinzani wake wa japan, ujeruman na italia lakini bahati nzuri vita iliisha kabla ya silaha hizo za kibiologia hazijatumika.

Wakati wa vita ya pili ya dunia japan iliweka bacteria wa kupindupindu kwenye mito 1000 ya maji nchini china na kuua Zaidi ya watu 30000, ugonjwa huo uliendelea kuua watu hata baada ya kuisha kwa vita kuu ya pili ya dunia.

Mwaka 1979 maabara moja nchini urusi iliachia virusi vya anthrax bahati mbaya na kuua watu 66, serikali ya nchi hiyo ilipinga swala hilo lakini baadae ilikubali.

Mwaka 2001 barua ilitumwa nchini marekani ikiwa na bacteria wa anthrax ndani yake na kuua watu watano, haikufahamika barua ile ilitoka wapi.

Wakati wa vita ya mungolia, askari wake walitupa maiti zilizouawa na ugonjwa wa plague kwa wapinzani ili kusambaza ugonjwa huo sehemu mpya, hii ni moja ya sababu ya kuchelewa sana kuisha wa ugonjwa huo.

Tutarajie nini miaka ijayo?
kuna uwezekano mkubwa silaha hizi kutumika sana dunia hii ya sasa sababu ya kukua sana kwa teknolojia ya kutengeneza magonjwa haya na mbinu za kupambana kiuchumi kwa mataifa mbalimbali kwani vita ya silaha za kawaida zina athiri sana miundombinu, nyumba za kuishi, viwanda na miji mikubwa iliyojengwa kwa miaka mingi.

Source: Phoenix
 
Hakuna binadamu mwenye uwezo wa kuumba kiumbe chochote hata kama huyo kiumbe awe mdogo kiasi gani, hakuna na haitakaa itokee mpaka mwisho wa dunia, ni uongo wa mchana kweupe kabisa, kwa mujibu wa biblia yangu

Mungu alimashaliza kuumba, na baada ya kumaliza kuumba hiyo kazi hakuachiwa kiumbe yoyote yule, yaani hata shetani hana huo uwezo,
 
Kwa Afrika na waafrica, silaha hii ni maarufu sana japokuwa imekuwa ikitumika kati ya mtu na mtu au kaya na kaya.

Magonjwa kama ukoma na mengineyo yaliaminika kutumika kama adhabu kwa wahalifu wa makosa mbalimbali katika jamii.

Ukitaka kujua madhara na athari ya silaha ya magonjwa, angalia jinsi watu waliofanikiwa katika maisha wanavyorudi nyuma mara tu wapatwapo na maradhi ya muda mrefu
 
Kwa Africa na waafrica, silaha hii ni maarufu sana japokuwa imekuwa ikitumika kati ya mtu na mtu au kaya na kaya. Magonjwa kama ukoma na mengineyo yaliaminika kutumika kama adhabu kwa wahalifu wa makosa mbalimbali katika jamii. Ukitaka kujua madhara na athari ya silaha ya magonjwa, angalia jinsi watu waliofanikiwa katika maisha wanavyorudi nyuma mara tu wapatwapo na maradhi ya muda mrefu.
Ni changamoto Sana mkuu
 
Hii ni njia ya kuachia virusi, bacteria au fangasi kwenye jamii ya watu, mazao au mifugo ili kuweza kuwaambukiza kwa makusudi ugonjwa fulani na kuua kila kitu chenye uhai kwenye sura ya ardhi.

Hii inawezekana kwa kutumia mabomu maalumu, chakula, maji, dawa za kupuliza na kuchoma sindano.

Silaha hizi ni moja ya silaha hatari zaidi duniani kwani zikitupwa sehemu zinahakikisha hakuna uhai unaobaki, hata samaki na wadudu wa kwenye maji hufariki.

Kumekua na tetesi nyingi sana kwamba huenda ugonjwa wa corona virus umetengenezwa makusudi kuua watu au umewaponyoka maabara lakini hakuna ushahidi wa kutosha japokua hatuwezi kupinga kwani hilo linawezekana kwa asilimia mia moja na historia ya dunia imeonyesha mataifa yalioyofanya hivyo wakati wa vita Fulani Fulani.

magonjwa haya yanatengenezwa vipi?
Gene therapy ni teknolojia ambayo ililetwa mahususi kwa ajili ya kutumika kusaidia kutibu magonjwa kama siko seli, saratani, kisukari, magonjwa ya moyo, magonjwa ya kuvuja damu na hata ukimwi kwa kubadilisha vimelea au gene ambazo zinachochea magonjwa hayo na kuweka gene mpya ambazo zinazuia magonjwa hayo.

Mpaka sasa hivi wagonjwa wengi wamefaidika na teknolojia hiyo lakini ka upande wa pili teknolojia hiyo inatumika vibaya kutengeneza magonjwa hatari na ya kutisha.

Wanasayansi huchukua vimelea au DNA ya bacteria, virusi au fangasi kisha hutengeneza wadudu wengine wengi wa aina hiyo hiyo kitaalamu kama cloning kisha huwabadilisha maumbile wadudu hao na kuwafanya wasiweze kutibika na dawa zilizopo.

mfano kama bacteria Fulani alikua na uwezo wa kutibiwa kwa kuharibu gamba lake la nje kitaalamu kama cell wall basi gamba lile huondolewa kwa teknolojia ya gene therapy na kumfanya bacteria yule kushindwa kutibika.

kwanini corona virusi haitibiki sasa hivi?
Ugonjwa wa corona ulikuepo tangu mwaka 1960, na ulikua sio ugonjwa hatari lakini ghafla ulibadilika mwaka 2019 na kua ugonjwa tishio kitu ambacho kinaleta mashaka kwamba huenda virusi hao wamebadilishwa na kuongezewa nguvu maabara.

Mpaka sasa hivi hakuna mtu aliyekubali kuhusika na ugonjwa huo japokua kuna mashaka kwamba ugonjwa huu umetengenezwa.

Nchi ambazo zilitengeneza magonjwa kwenye historia ya dunia.
Mwaka 1944 wakati ya vita kuu ya pili ya dunia nchi za marekani, uingereza, urusi, china na wenzake walitengeneza maabara kubwa za kutengeneza bacteria wa anthrax, brucellosis, na sumu botulism kwa ajili ya kupambana na wapinzani wake wa japan, ujeruman na italia lakini bahati nzuri vita iliisha kabla ya silaha hizo za kibiologia hazijatumika.

Wakati wa vita ya pili ya dunia japan iliweka bacteria wa kupindupindu kwenye mito 1000 ya maji nchini china na kuua Zaidi ya watu 30000, ugonjwa huo uliendelea kuua watu hata baada ya kuisha kwa vita kuu ya pili ya dunia.

Mwaka 1979 maabara moja nchini urusi iliachia virusi vya anthrax bahati mbaya na kuua watu 66, serikali ya nchi hiyo ilipinga swala hilo lakini baadae ilikubali.

Mwaka 2001 barua ilitumwa nchini marekani ikiwa na bacteria wa anthrax ndani yake na kuua watu watano, haikufahamika barua ile ilitoka wapi.

Wakati wa vita ya mungolia, askari wake walitupa maiti zilizouawa na ugonjwa wa plague kwa wapinzani ili kusambaza ugonjwa huo sehemu mpya, hii ni moja ya sababu ya kuchelewa sana kuisha wa ugonjwa huo.

Tutarajie nini miaka ijayo?
kuna uwezekano mkubwa silaha hizi kutumika sana dunia hii ya sasa sababu ya kukua sana kwa teknolojia ya kutengeneza magonjwa haya na mbinu za kupambana kiuchumi kwa mataifa mbalimbali kwani vita ya silaha za kawaida zina athiri sana miundombinu, nyumba za kuishi, viwanda na miji mikubwa iliyojengwa kwa miaka mingi.

Source: Phoenix
Tena cha ajabu... wanayofanya ni watu waliyo Shiba na wenye utajiri .... Lakini undani wao ni masikini na njaa tupu!! Heartless pippo!!
 
Hakuna binadamu mwenye uwezo wa kuumba kiumbe chochote hata kama huyo kiumbe awe mdogo kiasi gani, hakuna na haitakaa itokee mpaka mwisho wa dunia, ni uongo wa mchana kweupe kabisa, kwa mujibu wa biblia yangu

Mungu alimashaliza kuumba, na baada ya kumaliza kuumba hiyo kazi hakuachiwa kiumbe yoyote yule, yaani hata shetani hana huo uwezo,
soma kitu uelewe kwanza. hawaumbi bali wanamodify tu
 
Ahsante sana kwa somo
Nalog off
haka ka neno kanakufurahisha nini? Uki log off hayo ni yako hayatuhusu. unasumbua akili zetu na kuangalia upuuzi, saver za Jf zinajaa. Tunataka mambo mapya, km huna nyamaza pita huko! acha mara moja hii abia.
 
soma kitu uelewe kwanza. hawaumbi bali wanamodify tu
wanaumba kabisa siyo ku modify.

Human cloning.
Kuku wa mayai wameumbwa hawana baba. Lkn wapo. Mayai mnayo kula dsm hayana baba. Mitrye haikupigwa mashine.
Monolith
 
Hakuna binadamu mwenye uwezo wa kuumba kiumbe chochote hata kama huyo kiumbe awe mdogo kiasi gani, hakuna na haitakaa itokee mpaka mwisho wa dunia, ni uongo wa mchana kweupe kabisa, kwa mujibu wa biblia yangu

Mungu alimashaliza kuumba, na baada ya kumaliza kuumba hiyo kazi hakuachiwa kiumbe yoyote yule, yaani hata shetani hana huo uwezo,
acha uzwazwa hujui kusoma biblia wee! Hata kuikariri umeshindwa?
 
haka ka neno kanakufurahisha nini? Uki log off hayo ni yako hayatuhusu. unasumbua akili zetu na kuangalia upuuzi, saver za Jf zinajaa. Tunataka mambo mapya, km huna nyamaza pita huko! acha mara moja hii abia.
Umemaliza?
Nalog off
 
wanaumba kabisa siyo ku modify.

Human cloning.
Kuku wa mayai wameumbwa hawana baba. Lkn wapo. Mayai mnayo kula dsm hayana baba. Mitrye haikupigwa mashine.
Monolith
Inawezekana una watoto au wadogo zako na unawafundisha kuwa kuku wa mayai wametengenezwa, naomba nikueleweshe mkuu, jambo la Kwanza unalotakiwa kujua ni kwamba kuku yoyote yule anaweza kutaga mayai Bila kuwa na JOGOO yani Bila kupandwa, awe kuku wa kichina, kisukuma, kihaya, kuzungu, hao kuku wa kizungu Wanazaliwa kutoka kwa mama na baba kama kuku wengine, baada ya hapo wanachambuliwa vifaranga wa kike ndio wanauzwa kama kuku wa mayai na vifaranga vya kiume vinauzwa kama kuku wa nyama

Hivo basi jua kwamba ata wewe kama una mtetea wako nyumbani na umemfungia ndani Bila ya kuwa na JOGOO utaokota tu mayai, tofauti yake ni kwamba yatakuwa hayajarutubishwa, na kwa lugha rahisi hayo ndio ambayo waga yanageuka na kuwa viza endapo yakilaliwa na kuku kwa lengo la kutotoa vifaranga, kuku akilalia mayai 15 kuna uwezekano yapo ambayo alitaga Bila kupandwa na hivo hayana baba na mwisho wake huaribika na kuwa viza

Tofauti ya mifugo ya nchi za ulaya ni kwamba wanatuzidi uzalishaji, kuku wa kienyeji hana uwezo wa kutaga mayai mengi ndani ya mwaka mmoja akiwa Bila JOGOO, ila kuku wa kuzungu anaweza kutaga mayai mengi ndani ya mwaka Bila kuwa na JOGOO, angalia pia kuhusu uwezo wa kutoa maziwa ng'ombe wa kienyeji na ng'ombe wa kisasa, ng'ombe wa kienyeji anaetoa maziwa mengi kabisa unakuta anatoa lita 10 kwa siku, ila wa kisasa anatoa hadi maziwa lita 40 kwa siku, mtu mwenye miaka 30 wa huku kwetu hawezi kulingana umbo na kijana wa miaka 20 wa kizungu, kama unafatilia mpira utajua, nguruwe wa miezi 12 wa kienyeji hana ata kilo 40 ila nguruwe wa kisasa mwenye kilo 40 ni mtoto wa miezi 2, hivo kuna tofauti kubwa sana kati yetu na nchi za magharibi

Kwahiyo kama ulikuwa unafundisha hivo watoto wako jua kuwa ulikuwa unakosea, kwa namna moja au ingine nitakuwa nimekusaidia kubadili uelewa wako
 
Mkuu mie ni mfugaji wa mifugo ya kienyeji kwa asili kabisaa halafu napenda wanyama mno km babu yangu yote nayajua.

All kind of animals species can be cloned na matunda pia kile chakula hkn madhara kwa binadamu.
Cloning haijaanza leo wala jana ilikuwepo.
Sema tukufundishe usikaze mikono tu kwa key board.
Maziwa ya ngombe wa kienyeji ni matamu. Kuliko hao unaosema wa kizungu hata kuku pia hata juice ya kienyeji.
wanakudanganya.
 
Back
Top Bottom