Fahamu Jamii isiyo na wivu wa kimapenzi kanda ya ziwa

cutelove

JF-Expert Member
Oct 3, 2017
3,317
7,509
Kibinadamu tumeumbwa na wivu fulani hasa linapokuja suala la mapenzi

Katika hali ambayo si ya kawaida kabisa kuna jamii Fulani kanda ya ziwa huwa wana wivu kiduchu sana kwa waume au kwa wake zao au hawana kabisa

Angalia hapa

1,Mwanamke anaweza kumshawishi binti fulani aolewe na mume wake,lengo ili mwanamke na huyo binti wazidi kupendana wawapo uke wenza

2,Mwanaume anaweza akamshawishi mke wake atafute hawala ili huyo hawala awe anampa hela ya matumizi ili kupunguza hali ngumu ya maisha nyumbani lakini mwanamke anapewa tahadhari na mume wake asije akamfanyia dharau

3,Mwanamme anaweza kuwa na hawala na huyo hawala akawa rafiki wa mke wa mwanaume,urafiki haswa na mwanamke anajua kabisa huyu ni hawala wa mume wangu na cha ajabu wanawake hawa wakawa wanasaidiana vitu kadha wa kadha na wakashona sare kama kuna harusi mmoja wao alialikwa,wataenda wote wamevaa sare

4,Mwanaume hawezi kuchunguza mtoto aliyezaliwa anafanana na nani,na cha ajabu kama mtoto alizaliwa na mwanaume fulani na sura inaendana na huyo mwanaume,baba wa mtoto hupata taarifa hizo lakini hawezi kufanya fujo,au kumtenga huyo mtoto,Ukisikia kitanda hakizai haram basi hii jamii inatekeleza kwa asilimia 100

5,Mwanamke anaweza akawa anavaa nguo za bei,viatu na kula chakula bora ,na mwanaume akajua hivi vitu haviendani na kipato chao lakini mwanaume asihoji,hapa nikasikia kuna msemo wanautumia "Mwanaume tema mate chini mji ukue" wakimaanisha mwanaume usifuatilie hayo mambo ilimradi watoto wanakula na wanakua

6,Mwanamke ukiwa na wivu sana,mwanaume atafanya mbinu za kupunguza wivu wako,anaoa mke mwingine

7,Mwanamke anaweza akaenda zake,akatoka kwenye ndoa na akaenda zake kutafuta maisha,lakini huko alikoenda akakutana na wanaume wakamzalisha,kisha maisha yakagoma akirudi kwa Mme wake wa awali hupokelewa na watoto aliokuja nao huhesabiwa wa mume wake huyo wa ndoa na hakuna tatizo kabisa na maisha huendelea

8,Mwanaume huoa binti aliyezaa kabla ya kuolewa ,hata kama ana watoto watatu,na watoto huhesabiwa ni watoto wa muoaji.Mtoto huhesabiwa wa baba fulani kama alitoa mahari

9,Baba ni mkali zaidi kwa watoto wake wa kike, mfano unaruhusiwa kutembea na mke wa jamaa lakini si watoto wake wa kike au hawala,ni mchungu balaa

Ishi uone Mengi
 
Kuna dada mmoja aliolewa na muuza genge lakini dada mzuri amenyooka sema kwa miezi genge alifika.

Maisha ya chumba kimoja wakapata watoto wawili. Hali ilizidi kuwa mbaya. Dada aliamua kufanga Ferry. Alipata mzungu, mzungu alifika bei anatakawkuchukua jumla. Walikaawna mume wake wakaamua heri aolewe.

Aliolewa na waligawana watoto na mume wake. Alikwenda Ulaya na mtoto wa kike, wa kiume alibaki na baba yake.

Kule hakupata watoto wengine, lakini alimudu kumjengea nyumba mtoto wa kiume.
 
Kuna dada mmoja aliolewa na muuza genge lakini dada mzuri amenyooka sema kwa miezi genge alifika.

Maisha ya chumba kimoja wakapata watoto wawili. Hali ilizidi kuwa mbaya. Dada aliamua kufanga Ferry. Alipata mzungu, mzungu alifika bei anatakawkuchukua jumla. Walikaawna mume wake wakaamua heri aolewe.

Aliolewa na waligawana watoto na mume wake. Alikwenda Ulayawna mtoto wa kike, wa kiume alibaki na baba yake.

Kule hakupata watoto wengine, lakini alimuduwkumjengea nyumba mtoto wa kiume.
Hatari
 
Hebu tulia basi uandike vizuri
 
Leo sijui umekula makopa yawapi, embu soma ulichokiandika
 
Hiyo inaitwa ku control hasira tu maana mengine yanaumiza utajikuta umeua bure tu.
 
Back
Top Bottom