Fahamu artificial intelligence (AI) Afya, Pt 3.

Swahili AI

JF-Expert Member
Mar 2, 2016
6,316
47,472
Habari Wana JF,
Leo tutaendelea na mada yetu ya akili bandia upande wa afya.
Tutaangazia nyanja mbalimbali za afya ambapo akili bandia AI hufaunya kazi na nini matazamio yake siku za mbeleni.
Kama tulivyoona awali kwamba AI hutegemea maelfu ya data kukusanywa na kujazwa kwenye kifaa kama vile kompyuta au apps (cumputer like machines) ili kutoa matokeo sahihi ya maswali kifaa au kompyuta itakapoulizwa kupitia alogarithm zake.

Tunapoongelea afya tunaamanisha vitu vikuu kama, vipimo na madawa. Vipimo/utambuzi (diagnosis) ndio msingi wa kupelekea mgonjwa kutumia dawa ipi kutokana na majibu ya kipimo husika. Kuna baadhi ya apps zimetengenezwa kwa ajili ya kufanya utambuzi wa dalili na kuleta matokeo karibu na magonjwa husika.

Kampuni kama Google wana Project iitwayo Euphonia, ambapo ina malengo makuu maili
1. Kuongeza utambuzi wa hotuba(Speech Recognition) kwa watu wenye matatizo ya kiafya yanayopelekea kutotamka matamshi vizuri kama Amyotrophic lateral sclerosis (ALS).
2.

Pia AI inategemewa kuwa msaada mkubwa sana kwa teknolojia ya kutengeneza ogani za mwili kwa kutumia stem cell. Stm cell ni cell ambazo zipo huru zenye uwezo wa kupewa virutubisho fulani na kuwa ogani ya mwili kama vile ini, kongono na kadhalika. AiI inategemewa kusaidia kutoa ishara mapema zaidi kwa ogani ambayo itafeli au kushindwa kufanya kazi zake kwa ufasaha kama inavyotakika.

Kwa upande wa viungo bandia, AI itawezesha kutengeneza viungo bandia ambavyo vitakuwa na muunganiko wa kimawasiliano moja kwa moja na ubongo wa mwanadamu, hivyo kiungo bandia kufanya kazi kama kiungo halisi cha mwanadamu. Inasemekana pia 2050 watu wataweza kubadilisha viungo vya halisi kama mikono na miguu na kuweka bandia kwa maana nishati ya umeme itakuwa ikitumika zaidi kuliko vyakula, yani umeme ni mwingi kuliko mashamba. Hii itakuza sana soko la biotechnology na kuathiri sana afya.
 
Hadi mbo0 halisi unaitoa unaweka bandia ??Sasa sijui itakuwa ya chuma au material gani
 
Back
Top Bottom