kakuruvi
JF-Expert Member
- Sep 2, 2009
- 770
- 256
Enzi zile za Mzee Mwinyi alipewa nguvu iliyoitwa Fagio la Chuma iliyopelekea Marehemu Brg.Moses Nnauye kutunga wimbo 'usipowajibika ole wako utakumbwa na fagio la chuma' sikumbuki uliimbwa na bendi gani, nguvu hii Rais aliitumia kufagia na kusafisha serikali kwa maana ya kutumia madaraka aliyonayo kwa mujibu wa katiba kuwawajibisha watendaji wabovu serikalini.
Hivi lile fagio liko wapi? Ninachoomba kama Mzee Mwinyi aliondoka nalo liko Museum basi ampe Mwenzake Mh.Rais Kikwete naye alitumie kwani sasa hivi watendaji wabovu ni wengi zaidi ya wakati ule, nauliza tena ''fagio liko wapi?''