Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 58,636
- 220,438
Dada mmoja anatoka katika familia ya watoto watano wote wanawake, yeye akiwa wa katikati kuzaliwa. Katika watoto wote watano wa familia yao wameweza kufika chuo kikuu,wote wanaajira na wote wameolewa na wanakaa katika mikoa tofauti.
Dada huyu na mume wake wote wanaajira za kueleweka namaisha standard.
Wana watoto watatu wadogo, wakiume wawili na wakike mmoja.Mtoto wa mwisho yuko nursery, wawili wako primary lakini ndiyo kwanza madarasa ya awali. Wanasoma hizo shule za Academy sijui English Medium mambo yenu ya sikuhizi.
Hii ni familia walifanikiwa kupangisha nyumba, nakama zilivyo nyumba nyingi za mjini, wamefanikiwa kupata nyumba ya vyumba vitatu vya kulala, ikiwa na master bedroom. Kwahiyo vile watoto wa kiume wawili walikua na chumba chao, wakike wakawa wanashare chumba na dada wa kazi.
Dada wa pili kuzaliwa aliolewa na mume mlevi ile mbaya, jamaa kakolea kageuka Tyson ndani ya nyumba haikuwa big deal. Mama alikuwa anapigwa sana.Wao walikua na watoto wawili,wakike na wakiume, watoto wenyewe walikuwa wakubwa na wanasoma secondary.
Siku ya siku dada alipigwa mpaka majirani wakaingilia,ilibidi wamchukue yule baba, mmoja wao akasema nitakaa nae kwangu mpaka pombe zimtoke. Kuona hali ile, mama akakusanya vitu alivyoweza kukusanya, haraka akaondoka na wanae, walifanikiwa kukimbiliakwa mdogo wake.
Dada anatoka kazini anakuta wageni na masanduku, anamwambia mdogo wake kule kwa yule mwanaume sirudi. Dada huwezi kumtupa, ikabidi wafanye maandalizi ya kuishi. Mipangoikawa dada apate uhamisho afanyie kazi mkoa ule, na watoto wapelekwe kwa afisa elimu, wapate kibali cha muda waanze shule wakati mipango ya uhamisho ikifanyika
.
Dada na mwanae ikabidi walale na binti wa mwenye nyumba nadada wa kazi, kijana akalala na watoto wa kiume. Kijana alikua amesha fikia balehe, basi akawa akitoka shule ananunua vipipi, akirudi nyumbani usiku anavipa vile vitoto pipi, anaviingilia kinyume cha maumbile, tena anaviambia mkisema kesho siwaletei pipi nyingine.
Mchezo uliendelea kwa muda mrefu, ila za mwizi ni arobaini, siku moja alizidisha mchezo, kitoto kikawa kinashindwa kutembea. Kimeshindwa kuamka kwenda shule, ndiyo siku wazazi walipojua.
Dada na mume wake walitaka kuita polisi, lakini ndugu waliwasihi sana wasipeleke kesi polisi, yaishe ki familia. Bi dada na mume wake walipata kidonda kikubwa sana, baada ya hapo walitafuta kazi katika moja ya nchi za Kusini mwa Africa. Mpaka sasa hivi hata likizohawaji, hawataki hata kuonana na ndugu.