Elections 2010 Fact: Church, the Force Behind CHADEMA's Popularity; will the holy union last longer?

Status
Not open for further replies.

Shinto

JF-Expert Member
Dec 6, 2010
1,781
0
Bila kuuma uma maneno, ni ukweli usiopingika kuwa kanisa limetoa mchango mkubwa katika kuifikisha CHADEMA hapa ilipo leo hii.
Umaarufu wa CHADEMA uliongezeka mara dufu kufuatia kanisa kutoa 'waraka' ambao jamii ya kikristo iliutafsiri vema.
Najua kuna watu watabisha kwa nguvu zote hili lakini ukweli utabaki kuwa huo. Kisingizio kuwa CHADEMA kina viongozi imara sasa hakina ukweli kwani ni viongozi hawa hawa waliokuwepo 2005 na mwenyekiti Mbowe aligombea urais.
Pia hoja ya ufisadi ndani ya CCM haina nguvu sana kwani ufisadi mwingi ulifanyika kwenye awamu zilizopita mbona CDM haikupata umaarufu huo?
Nadhani directly au indirectly kanisa liliamua kuiadhibu serikali ya awamu ya nne kwa kuvunja 'memorundum of understanding'

Mimi hofu yangu ni come 2015 elections, CCM wana turufu ambayo kama wataitumia na wameiweka kimkakati, political landscape in TZ will not be the same. Turufu yenyewe ni CCM kumsimamisha mgombea wa urais mkristo.
  1. Kanisa litaacha 'holy union' na CDM ili kufufua memorundum of understanding na serikali ya huyo mgombea?
  2. Waislamu ambao sasa wanaunga mkono CCM wataendelea kukiunga mkono ili kulinda maslahi yao?
  3. Wale walioenda CDM kwa wito wa kanisa watabaki huko, au watarudi kutetea maslahi serikalini?
 

PakaJimmy

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
16,213
2,000
Thi is a bit better than crap!

Mi ni mpenzi wa CHADEMA, sijawahi kushawishiwa na mtu kanisani or wherever juu ya kuichagua CDM..
oNGEA VITU VYENYE USHAHIDI!
Huo waraka unaoudai kuwepo, ulifika as far as wapi?...vijijini mashambani mpaka wapi?...na msambazaji alikuwa nani na je kwanini haukuripotiwa kuwa ni kinyume na matakwa ya tume ya uchaguzi?
Kama Dr Slaa alipata support ya kanisa na akawa tishio vile, basi ulipaswa kuandika habari hii kwa maana ya ku'admire ukubwa wa nguvu ya kanisa na vile inavyotakiwa kutumika POSITIVELY kwa maendeleo ya nchi, not this stupidity, a potential to unrests in the country!...

Nakushauri usifanye UTABIRI na ndoto zisizo na majibu kwa sasa, unajenga chuki unnecessarily!...Uchaguzi umepita, na maisha yako palepale!
 

LAT

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
4,403
0
MS .... DSM... Y.Y ndio wale wale ......wanauotuchangaya na hoja zao zisizo na root ... please potezea thread hii.... with incrustation... mods seal this thread with silicon agent...
 

mfarisayo

JF-Expert Member
Nov 23, 2010
5,152
2,000
Kabla ya kanisa kutoa waraka, Waislam si nao walitoa waraka wao?
Mbona husemi effect yake kwenye uchaguzi?
 

Mwanajamii

JF-Expert Member
Mar 5, 2008
7,064
0
Wewe ni mdini na unatoboa mtumbwi tena katika ya bahari kuu ambao na wewe umepanda na bila kujua kwamba mtumbwi huo ukizama na wewe ni mmoja wa wataozama na kufa.

Ndani ya CCM kuna wakristo na waislamu na vivyo hivyo ndani ya chadema. Ndani ya CUF kuna waislamu wengi kuliko wakristo pengine ni kwa sababu kina asili ya zanzibar lakini kusema ni chama cha msikiti itakuwa ni fikra mgando. Unachotaka kupandikiza katika akili zetu ni kwamba chama kikiongozwa na mkristo basi ni cha wakristo na kikiongozwa na mwislamu ni chama cha waislamu. Na zaidi waislamu walio ndani ya chadema ni wengi kuliko wakristo walioko ndani ya CUF.

Mimi nafikiri kama una hoja ya kuipinga chadema ni haki yako ya kikatiba ya kuchagua chama cha siasa ukipendacho lakini ni bora usitumie mwamvuli wa kidini. Mwamvuli wa kidini ni hatari lakini pia unaweza kusababisha washiriki wengine watoe maoni yao kwa kuchambua vyama vyote vya siasa kwa misingi ya dini jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa nchi yetu.
 

Mwanajamii

JF-Expert Member
Mar 5, 2008
7,064
0
Waraka wa waislamu na wakristo ulitoka hata hapa JF upo ni vema tukakemea mambo hayo kwa pande zote badala ya kujifanya hukuona waraka wa upande mmoja ambao pengine ni wa upande wa dini yako wakati zilisambaa sehemu nyingi nchini na nyingine zikaletwa hapa Jf kwa mjadala.
 

FarLeftist

JF-Expert Member
Oct 20, 2010
363
0
upupu huu,
kama waraka uliotolewa na kanisa ndio sababu ya mafanikio makubwa ya chadema, vipi kuhusu waraka uliotolewa na waislamu umepelekea mafanikio kwa chama gani? hakuna logic kwenye hoja yako, nadhani umekua subjective zaidi....
 

Mwanajamii

JF-Expert Member
Mar 5, 2008
7,064
0
Je mwaka 2005 jamii ya wakristo haikuwepo nchini kuisadia chadema hadi wasubiri 2010?
 

Jackbauer

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
5,930
2,000
How do you explain the victory of other opposition parties namely NCCR(kigoma),CUF(rufiji) and TLP(Vunjo)??? Is it the church or mosque?
Are you RETARDED?
 

Gerad2008

JF-Expert Member
Jun 9, 2009
561
500
Awe Mkristo au Mwislamu ;Hivi kwani lazima CCM iongoze jamani? Tumewachoka na hawana kipya tunataka mageuzi uongozi wa kimazoea hatutaki
 

Kibaraka

JF-Expert Member
Dec 14, 2010
249
195
Ukitaka kugombana na watu humu Jf basi sema kitu chohote kibaya kuhusu CHADEMA hata kama ni ukweli lakini watu watakupinga na kukushutumu mara 'umetumwa wewe' na maneno ya kashfa kibao.
 

Nzi

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
13,932
2,000
Malaria Sugu a.k.a yaya a.k.a Dar es Salaam a.k.a Jeykei a.k.a JeyKeiWaUkweli at his/her best. Yani hiki KIRUSI hata kikitumia ID ya 'JF moderator x',lazima nitakigundua.
 

Mwanajamii

JF-Expert Member
Mar 5, 2008
7,064
0
Waraka wa wakristo haukuanza kutoka mwaka 2010 hata katika uchaguzi wa 2005 ulitoka kama ungekuwa na impact katika siasa za chadema basi kuanzia mwaka 1995 ambao kanisa lilianza kutoa waraka wa uchaguzi. Ninavyoona mimi ni kwamba waraka wa wakristo wa 1995, 2000 haukuonekana tishio kwa sababu uongozi wa nchi ulikuwa chini ya mkristo lakini ulikuwepo na kumbukumbu zinaonyesha hivyo. Wadini wamegeuza kete ya waraka kuwa agenda yao ya kuibomoa nchi na kuacha agenda za msingi.

kanisa limesema litaendelea kutoa waraka kila uchaguzi bila kujali Rais atakuwa mkristo au mwislamu kama lilivyofanya huko nyuma, sasa na hapo baadaye.

Binafsi siungi mkono waraka hizi na zinachangia sana kuwachanganya wananchi.
 

LAT

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
4,403
0
Ukitaka kugombana na watu humu Jf basi sema kitu chohote kibaya kuhusu CHADEMA hata kama ni ukweli lakini watu watakupinga na kukushutumu mara 'umetumwa wewe' na maneno ya kashfa kibao.

if you can justify that what you say is legitimate.... jf hawatakupinga..... lakini ukikurupuka .... ndio madhara yake

haya...bwana kibaraka... justify this thread topic tukusifie
 

Prisoner 46664

JF-Expert Member
Dec 18, 2010
1,948
2,000
Sielewewi watu wengine huwa wanafikiri vipi..inanishinda kusema.
Kwani hilo 'kanisa' ambalo sijui hata ni lipi kati hizi denominations zaidi ya 200 tulizonazo,lilipoamua kukiunga mkono CDM kilifanyia
kampeni wapi za kushawishi wananchi kujiunga nacho.?makanisani?kwanini tusisikie..??
embu tuache kupanda mbegu za udini, mimi ni mkristo halisi, ila hakuna ninachopata nikiongozwa na rais mkristo aliye mpumbavu..
wananchi wanatambua sasa, zaidi ya wakati mwingine wowote,mabaya yanayofanywa na serikali...hii ndiyo sababu ya msingi ya
CDM kupata huu umaarufu hasa...tufikirie kimaendeleo zaidi tafadhali.
 

Mwanajamii

JF-Expert Member
Mar 5, 2008
7,064
0
wewe ni aina ya watu wanaofikiri kwamba Rais aliopo madarakani kachaguliwa na watu wa dini moja ni uendawazimu uliojaa ukale wa zama za watu wasotambua usasa unakokwenda.

Napenda kikwete kuwa Rais wangu lakini nachukizwa na watu wanaotaka tuamini kwamba kushuka kwa asilimia 20 mwaka huu kulisababishwa na kanisa kuinga mkono chadema. Kujenga hoja dhaifu kama hizi ni kutaka kupandikiza mbegu za sumu za udini kwamba watu wa imani nyingie wajenge imani kwamba Rais alichaguliwa na watu wa dini moja jambo ambalo si la kweli.
 
Status
Not open for further replies.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom