ACT-Wazalendo na CHADEMA ni "Back up Parties" kwa Makada wa CCM

X-bar

JF-Expert Member
Mar 20, 2019
1,002
1,146
Nani kakuambia ACT-Wazalendo ni ya Zitto Kabwe? Na nani anasema CHADEMA iko pale kuipinga CCM? Kwa taarifa yako vyama hivi ni “back up” za makada wa ccm wanaokosa nafasi au wasioridhishwa na siasa za ndani ya chama hicho. Sikiliza nikwambie.

Tukianza na CDM, hiki ni chama cha upinzani kilichopoteza muelekeo baada ya kutekwa na makada wa CCM mwaka 2010. Ikumbukwe kuwa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, CCM ilikumbwa na mpasuko uliochagizwa na wakristo ambao hawakupenda Mh. Kikwete aendelee na urais kutokana na sababu tatu.

Kwanza kabisa, Rais Kikwete alikuwa anataka kutimiza ahadi iliyotokana na ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2005 ambayo ni kuanzisha mahakama ya kadhi hapa nchini. Chama cha Mapinduzi kilisukumwa na kuamua kuingiza sera hii kwenye ilani yake kutokana na ukweli kwamba waislam enzi hizo walipamba moto katika harakati dhidi ya serikali. Ikumbukwe kuwa Augustin Mrema alijipatia umaarufu hadi kuwa mbunge wa Temeke kutokana na kuungwa mkono na waislamu kutokana na kuwaonesha kuwaunga mkono katika harakati zao za kuitaka serikali ianzishe mahakama ya kadhi. Kwahiyo mahakama ya kadhi enzi hizo ilikuwa ni “critical policy” kwa chama cha siasa ili kuungwa mkono na waislamu.

Pili, serikali ya awamu ya nne ilitaka kutekeleza matakwa ya waislam ya kuingiza nchi hii katika jumuia ya nchi za kiislam (OIC). Ikumbukwe Benard Membe akiwa ndo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa alifikisha Bungeni ripoti ya serikali iliyopendekeza umuhimu/faida kwa Tanzania kujiunga na OIC. Wakristo walikuja juu dhidi ya serikali na bila shaka hiki ndo chanzo cha Membe kuchukiwa na wakristo hata na kuanza kuwa na mashaka nae kama ni mkristo kweli au ni muislam. Wakristo wakaanza kumtuhumu Membe kuwa ni muislam bali ana undugu wa damu na Kikwete (muislam) na kwahiyo hata angeshinda urais bado angetekeleza agenda ya ndugu zake waislam.

Kubali au kataa, suala la mahakama ya kadhi hata kama hukumu zake haziwahusu wakristo na OIC hata kama inafaida kwa Tanzania, wakristo wa nchi hii hawako tayari kusikia. Na ukitaka hasira zao zikushukie basi jaribu ku-ipromote agenda hizi. Sasa kwakuwa CCM ilibeba agenda kwa faida ya waislam, hii ndio sababu ya wakristo kuanza kuchukia na kupanga mikakati ili kumkwamisha Rais Kikwete na CCM yake katika uchaguzi wa 2010. Viongozi wa makanisa wakawashawishi waumini wao walioshika hatam ndani ya CCM wajitenge na chama CCM ya Kikwete. Wengi walioitikia wito huu wakajiunga na CHADEMA na baadhi wakaanzisha CCJ na CCK.

Tatu, mamuzi ya CCM kupitia Katibu Mkuu Makamba ya kukata majina ya baadhi ya washindi wa kura za maoni za ubunge uliwakisirisha makada na wafuasi wa chama hicho hadi wakaamua kuunga mkono wagombea wa upinzani hasa CDM.

Sababu hizi tatu ndio msingi wa CHADEMA kutekwa na makada walioihama CCM ya Kikwete ambao walikiwezesha chama hiki kutoa upinzani wa nguvu dhidi ya CCM na kukiwezesha kuipiku CUF na kuwa chama kikuu cha upinzani. Kwa misingi hii ndipo tunasema CDM ni “back up” (kimbilio) la makada wa CCM ambao kwa sababu moja au nyingine hawaridhishwi na mienendo au maamuzi ya ndani ya CCM. Lakini inapotokea CCM inafanya mambo Fulani ambayo yanawapendeza, makada hawa ni wepesi wa kuachana na upinzani na kurejea kwenye “chama mama”. Kiufupi makada wa CDM na CCM wako kwenye “equilibrium” inayoathirika na hali ya kisasa ya ndani ya vyama hivyo. Kwahiyo tusishingae tunapoona kada wa leo wa CDM kesho anakuwa wa CCM na kinyuma chake. Kwa kuwa kuna “continuity” kati ya CDM na CCM ni vigumu kuona makada wa vyama hivi wanakimbilia vyama vingine kama NCCR, TLP, CHAUMA au CUF.

Kwa upande wa ACT, tofauti ya chama hiki na CDM ni kwamba, CDM ni mateka na ACT ni “hybrid” ya CCM na CDM. Wajinga wanadhani ACT ni ya Zitto Kabwe. Ukweli ni kwamba chama hiki kilianzishwa na Team Lowassa kutoka CCM ili iwe kimbilio lao endapo Lowassa angekosa nafasi ya kugombea urais kupitia CCM. Ni muhimu kukumbuka kwamba ACT kiliweza kusimamisha wagombea ubunge katika 80% ya majimbo yote. Chama hiki kikiwa bado kichanga kisingiweza kuwa na nguvu hiyo bila sapoti ya “watu wakubwa” ambao walikiandaa chama hicho kufanya harakati zao za kuelekea ikulu. Sasa mtu anaweza kuhoji kulikuwa na haja gani kwa Timu Lowassa kuanzisha ACT kama kimbilio lao wakati tayari kuna CDM ambayo ni mateka wa CCM? Nitafafanua.

Timu Lowassa hawakufikiria wangeweza kukubalika na kushika hatam ndani ya CDM tukizingatia ukweli kwamba chama hicho kilimuandama sana Lowassa kwa ufisadi wa Richmond. CHADEMA ndio chama kilichomuorodhesha Lowassa kwenye “List of Shame”. Lakini sababu nyingine ni kwamba Timu Lowassa wasingekuwa na nafasi ndani ya CDM kwasababu chama hiko kilikuwa katika muungano na vyama vingine vya upinzani, UKAWA, ambao tayari walishakuwa na wagombea wao makini na waliodhamiria kuchukua dola, yaani Slaa na Lipumba.

Hata hivyo,” gia ya angani” ya Mbowe ambayo ilitoa “offer” kwa Lowassa ilibadilisha njia kwa “safari ya matumaini” ya Lowassa na kupitia ya “anga” (CDM) badala ya reli (ACT). Lakini baada ya kushindwa kwa safari ya matumaini, makada wengi wa ACT na CDM ambao walihamia wakitokea CCM kwa kumfuata Lowassa (wazee wa ulipo tupo) wamerejea CCM.

Kutokana na continuity iliyopo kati ya vyama vya ACT, CDM na CCM, tusishangae tunapoona CDM na ACT wanaguswa sana na migogoro ya ndani ya CCM na kuomba imalizwe na wakati inapotokea hali kama hiyo kwa CUF wanashabikia.
 
Back
Top Bottom