Uchaguzi 2020 Upinzani na Membe 2020, mtaji au kurejea makosa?

Jamhuri ya Zanzibar

Senior Member
Jul 17, 2012
126
195
Wakati umoja wa vya vyama vya upinzani (UKAWA) vikiwa katika mchakato wa kutafuta mgombea watakaemuunga mkono wote kwa pamoja ili awawakilishe katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, ghafla palizuka agenda ya mtu aitwae Edward Lowassa. Suala la Lowassa kuibukia upinzani ni jambo ambalo halikutarajiwa mapema bali lilizuka ghafla ikiwa ni matokeo ya kudhulumiana ndani ya CCM. Suala la Lowassa kwenda upinzani haukuwa mkakakati uliopangwa na CCM. Maana CCM ya sasa si Chama cha mikakati ya akili kubwa bali ni Chama cha nguvu kubwa za vyombo na taasisi za Dola, vikiwemo vyimbo vya ulinzi na usalama.

Lowassa alikuwa mkweli katika agenda yake (ya kuutaka urais), yaani kutafuta haki yake ya kuwania urais aliodhulumia ndani ya CCM. Inawezekana hakufarahia sana kufanya hivyo kupitia upinzani. Hii iko wazi kwani alitumia kila uwezo na fursa alizokuwa nazo kuimarisha na kuunganisha upinzani katika kipindi cha Uchaguzi tu ili kuleta umoja wa upinzani utakaotoa matokeo aliyoyatarajia katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 nayo ni kutimia safari yake aliyoiitwa 'safari ya matumaini'.

Mikakati wa CCM ya kuusambaratisha upinzani kupitia hoja ya ujio wa Lowassa katika upinzani ilianzia baada ya Lowassa kutua upinzani sio kabla ya hapo. Mkakati huo ulikuwa ni kuhakikisha wapinzani wanasambaratika kufuatia hoja ya Lowassa kuwa mgombea urais mpya wa UKAWA, badala ya Lipumba au Slaa. Hata hivyo umadhubuti wa upinzani, ukweli wa Lowassa kwa wakati ule na namna alivyosimamia umoja wa UKAWA na uelewa mzuri wa Watanzania katika siasa za kipindi kile ni mambo ambayo yalipelekea UKAWA kubaki imara na hivyo mkakati wa CCM wa kuusambaratisha kufeli. Ambacho CCMilivuna kutokana na mkakati wake huo kilikuwa ni kumpata Prof. Lipumba kutoka CUF na Dr. Wilbroad Slaa kutoka CHADEMA wakiwa peke yao bila hata mfuasi mmoja nyuma yao.

UKAWA kwa kuwakilishwa na Lowassa katika urais wa Jamhuri ya Muungano ulifanya vizuri sana kama ambavyo wataalamu walivyozikokotoa mapema hesabu hizo. UKAWA ulifanikiwa kushinda majimbo mengi kuliko ilivyowahi kuwa katika historia ya vyama vingi Tanzania. CUF kwa mfano ambayo chini ya Lipumba mara zote tokea Uchaguzi wa mwanzo wa vyama vingi wa 1995 imekuwa ikishinda jimbo 1 au 2 au bila jimbo lolote lakini katika Uchaguzi wa 2015 kwa mwavuli wa UKAWA iliweza kuvuna majimbo 10. Upo ushahidi wa wazi wa hesabu za matokeo ya Uchaguzi wa 2015 zinazothibisha kwamba UKAWA ungevuna majimbo mengi zaidi kama sio ubinafsi na uroho wa vyama vyenyewe vya UKAWA wa kushindwa kukubaliana kuachiana baadhi ya majimbo na hivyo kupelekea kuzigawa kura za UKAWA katika majimbo hayo na hivyo kuangukia mikononi mwa CCM.

Matokea ya urais wa Jamhuri ya Muungano katika Uchaguzi wa 2015 yalikuwa nayo ni ya kihistoria. Kwa upande wa Zanzibar, Lowassa, mgombea urais wa UKAWA alipata ushindi mkubwa kumpita Magufuli wa CCM kwa tofauti ambayo haijawahi kutokea katika chaguzi za nyuma. Kwa upande wa Bara nako, asilimia ya ushindi wa urais kupitia UKAWA ulikuwa mkubwa sana kulinganisha na chaguzi zote zilizotangulia. Hili la Uchaguzi wa urais wa Muungano kwa upande wa Bara kutotoka na ushindi kwa UKAWA limeambatana na changamoto nyingi. Moja ni udhaifu wa siasa za eneo la msingi (grassroot level) kwa vyama vya upinzani. Ni ukweli usiopingika kwamba mpaka tunaingia katika Uchaguzi Mkuu, Oktoba 2015, vyama vya UKAWA vilikuwa bado vina misingi (grassroot machineries) dhaifu. Ikumbukwe kwamba msingi ni chombo muhimu sana katika sayansi ya uchaguzi.

Halkadhalika nguvu ya Dola haikuacha kushughulishwa na hofu ya uwezekano mkubwa wa Lowassa kushinda urais wa Muungano. Hivyo Dola iliratibu hujuma nyingi za kimkakati na za mabavu ili kuusambaratisha ushindi wa UKAWA katika urais wa Muungano. Moja ya hujuma iliyokuwa wazi ni kuvamiwa vituo vya ukusanyaji na ujumuishaji wa matokea vilivyokuwa vikisimamiwa na CHADEMA katika maeneo mbali mbali ya nchi.

Kuna imani (myth) inayopikiwa uzoefu wa 2015 kwamba kumueka tena mtu kutoka CCM kama vile Benard Kamillius Membe kuwa mgombea wa urais kupitia umoja wa vyama makini vya upinzani ni sawa na kurejea makosa. Sikusudii kusema kwamba wenye madai hayo hawana hoja. Laa hasha! Bila shaka wanayo hoja lakini msingi wa hoja hii zaidi umejikita katika hofu na woga, kwa kuangalia zaidi ule msemo mashuhuri wa Kiswahili usemao 'Muungwana haumwi na nyoka katika shimo hilo kwa hilo'.

Makala hii inajaribu kufanya uchambuzi kwamba pamoja na suala la Lowassa la kuukimbia upinzani na kurejea CCM, bado upinzani haupaswi kujijaza woga. Kwanza tuiangalie staili ya uondokaji wa Lowassa katika upinzani na kurudi CCM. Jambo moja ambalo lilimsukuma Lowassa kurejea CCM kwa mujibu wa baadhi ya wachambuzi ni umri na afya yake. Wanadai kwamba Lowassa amehisi safari yake ya kusaka urais haina wakati tena wa kutosha kulinganisha na umri na afya yake. Hivyo amehisi kupumzikia CCM ni usalama zaidi kwake.

Kufuatia Tundu Lissu, mwiba wa Magufuli kutangaza nia ya kuwania urais, Lowassa amedhani ule umaarufu wake wa 2015 umeshuka sana na hivyo jina la Tundu Lissu na umaarufu wake lina nafasi kubwa ndani ya CHDEMA kwa wakati wa sasa hivyo hivyo safari yake ya urais kupitia upinzani imeshafikia mwisho. Kama ni hivyo na kama agenda yake ilikuwa ni urais pekee, hakuona umuhimu wa kubaki upinzani kuadhibiwa na Dola. Washauri wake wamemshauri apumzikie CCM badala ya kubaki upinzani kujitatiza.

Lowassa hakufukuzwa katika CCM alitoka kwa hiari yake ili kuweza kupata fursa ya kugombea urais kupitia vyama vya upinzani. Kwa upande wa Membe ni tofauti, yeye amefukuzwa CCM, bila sababu ya kikatiba, kikanuni wala kimaadili kwa mujibu wa maelezo yake mwenyewe. Amefukuzwa kiuonevu akiwa hayuko tayari hata kidogo kuondoka. Amejaribu Mara nyingi kupambana ili pamoja na mgogoro wake huo na Chama chake, aweze kubakia lakini juhudi zake hazikufua dafu. Zisingefua dafu kwa sababu Mwenyekiti wa CCM ni Rais Magufuli ambae takriban sio tu WanaCCM bali watanzania wote wanafahamu busara yake inakuwaje pale panapohusika na jaribio la kumpinga au kumkabili. Hivyo kwa mtazamo huu wa kufukuzwa katika Chama kiuonevu hasira za Membe ni zaidi ya zile za Lowassa.

Lowassa alipendwa sana lakini hakuwa mtu wa mikakati ya kisiasa wala ya kisayansi ya Uchaguzi. CHADEMA na ukawa walikuwa ndio muongozo wake wa kila jambo katika safari yake ya kugombea urais ndani ya UKAWA. Membe ni mtu wa mikakati (strategic person). Anaweza kupika mikakati yote ya kushambulia na kudifendi hivyo anaweza kuwa turufu muhimu katika science ya mikakati ya Uchaguzi Mkuu wa kumng'oa Magufuli Oktoba 2020.

Lowassa alikuwa mtu mpole sana kwa kauli na vitendo. Alikuwa mwepesi, mwenye kuonesha unyonge na kuhitaji kuhurumiwa. Membe ni mtu tofauti. Anaonesha Yuko tayari kupigania haki yake. Ni mkali (aggressive), hivyo anaweza kupambana zaidi badala ya kubaki mgombea tu wa kusubiri huruma na hisani ya Dola kama ilivyokuwa kwa Lowassa.

Bado CCM inahitaji silaha nzito ili kuishambulia. Silaha nzito zaidi kuliko ya mwaka 2015. Silaha ambayo itawaunganisha CCM, upinzani, wanaharakati dhidi ya udikteta wetu tulioishi nao kwa miaka mitano sasa, wasio na vyama na Watanzania kwa jumla waliochoshwa na unyonge ulioletwa na Awamu hii ya utawala wa Magufuli. Kwa maoni yangu, Membe ndio mgombea anaekidhi matakwa ya zama, nyakati, mazingira na hali ya kiasa ya sasa.

Mara hii hatunae Lipumba wala Slaa hivyo yale makosa ya ubinafsi wa kugombea urais hatutarajii yatarejewa na watu makini wanaoongoza upinzani kwa sasa. Wakati wa ubinafsi wa kichama kwa kambi ya upinzani kugombea urais bado haujafika. Let's kill the beast first!

Twende na Membe 2020

Ahmed Omar
Zanzibar

Makala hii ni maoni yangu binafsi, hayahusiani na maoni au fikra za taasisi yeyote niliyo na mahusiano nayo
 
Nimesoma nikashindwa kufika mwisho lakini ukweli ni kwamba Membe hafai kugombea urais!

Mgombea anayefaa CHADEMA ni Tundu Lissu. Bora tukapotee tukiwa na mwenzetu sio hao wa kuletwa na mfumo kwa makubaliano.

Sent from my VFD 301 using JamiiForums mobile app
 
Ccm acheni hofu kwa CHADEMA mnatia aibu kabisa. Kwanini hamjiamini kama mnafanya mazuri?
 
s
hebu summarizebasi duh!
 
Back
Top Bottom