Facebook wazindua Verified accounts

Joeli

JF-Expert Member
Joined
Apr 25, 2011
Posts
4,941
Reaction score
3,417



Facebook imefuata mkondo Twitter kwa
kuanzisha akaunti na kurasa zilizothibitishwa (verified pages/
accounts) ili kuwawezesha watu mashuhuri kuthibitisha akaunti akaunti na fan page zao. Facebook wamesema wamefanya hivyo ili kusaidia watumiaji wa Facebook kuzitambua akaunti za kweli za mastaa na watu wengine mashuhuri
wanaotumia mtandao huo, pia ikiwemo
biashara zenye majina makubwa.
Kurasa zilizothibitishwa zitakua na alama ya blue ya pata “check-
mark” kama inavyoonekana kwenye
picha hapo juu. Watu
wataoruhusiwa kutumia huduma hiyo ni,
viongozi wa serikali, waandishi wa habari
maarufu, makampuni au bidhaa maarufu.
Hivyo kuanzia sasa, utaweza kufahamu
akaunti/pages zipi ni za kweli na zipi ni feki.

Ili mtu mashuhuri kupata akaunti
iliyohakikishwa, mhusika atahitaji kuwasilisha kitambulisho halali kinachotambuliwa kiserikali. Nadhani
celebrities (mastaa) Wengi wa Afrika
wataipenda hii. Kama mfano Wema, kuna
page zaidi ya kumi zinazodai kuwa ni
“Wema Sepetu”
 
Hamna kitachoshindikana hata hizo watu watazi-fake tu,watu wanaweza kuingia kwenye website ishindikane FB fan page? Tena hizo ndo mzuri mtu aki hake na kutumbukiza madudu yake itaonekana kweli ndo wewe muhusika hamna visingizio-uko kwenye reasonable dought

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Kwa facebook siyo rahisi sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…