Facebook waanza kushughulikia akaunti za bandia.

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,939
20,399
Mtandao wa jamii maarufu duniani kwa jina la FACEBOOK wameanza mchakato wa kufuta kaunti zote ambazo uhalisia wake haujulikani yaani ni za bandia.

Baada ya uchunguzi wa muda kufanyika kwenye mtandao huo na hasa baada ya kujiorodhesha kwenye soko la mitaji la NewYork, imegundulika kuwepo kwa akaunti za uongo za watu zipatazo milioni 83.

Baadhi ya watumiaji maarufu wa mtandao huo kama Justin Timberlake, Rihanna na Lady Gaga na wengine wamejikuta wakiwa na upungufu wa wafuasi wao kwenye mtandao huo.

article-1348425787380-1529CF1C000005DC-23937_636x491.jpg

Lady Gaga ana wafuasi wapatao milioni 53,238,735

Hatua hiyo ya FACEBOOK imekuja katika wakati ambao mtandao huo unatafuta pesa zaidi kupitia matangazo ambapo ni wale watumiaji halisi ndio wataweza kulengwa na makampuni ambayo yanatangaza kwenye mtandao huo. Pia imeaminika kuwa asilimia 8.7 ya watumiaji wake wapatao 845 hawatumii majina ya kweli, hivyo kufanya nasafi yake kwenye soko la mitaji kuwa ndogo.

article-1348329862722-1523E4F2000005DC-683476_636x431.jpg

Rihanna nae anavutia wafuasi wanaofikia milioni 60,370,797 sasa.

Moja ya tatizo kubwa la watumiaji wa majina ya uongo ni kuweza kutengeneza pongezi au "likes" kwa kutumia software maalum za Malware ambazo huingilia kazi za computer husika na kuharibu utendaji wa program zake, kwa kufanya hivyo jina la FACEBOOK linakuwa linakuuzwa lakini katika hali isiyo rasmi.

Pia kwa mtindo huo wale watumiaji maarufu wanakuwa hawajui uhalisi wa wafuasi wao. FACEBOOK siku ya Alhamisi walitoa taarifa kwenye blog yao wakieleza hatua hiyo wanayochukua na kwamba wanaamini itasaidia kupunguza hizo "likes" kwa asilimia 1.

Utumiaji wa majina yasiyo rasmi umeleta matatizo kwa mitandao mingi ya kijamii na umekuwa shughuli nyingi za kihalifu pia zimekuwa zikifanika kwa kutumuia majina bandia kwenye mitandao hiyo.
img_4126-300x225.jpg

Nembo ya mtandao wa FACEBOOK nje ya jengo la makao yake makuu mjini California kwenye kitongoji cha Palo Alto.

Mtandao wa JamiiForums tayari ulikwishajiandaa na yote haya na ndio maana tumefika hapa tulipo.

Idumu JF.
 
kutokana na sheria za jf nafikiri swali ulilotakiwa kuuliza ni "jf imejikinga vipi na majina halisi?

kwanini unasema hivyo? Au unamaanisha usalama mtandaoni? Facebook wanaondoa account feki na zenye majina ya uongo, sasa JF Wanaotumia majina halisi ni asilimia kama 20 tu! Hapo inakuwa sielewi
 
kwanini unasema hivyo? Au unamaanisha usalama mtandaoni? Facebook wanaondoa account feki na zenye majina ya uongo, sasa JF Wanaotumia majina halisi ni asilimia kama 20 tu! Hapo inakuwa sielewi
ao u

Ungesoma rules zao ungeelewa kwamba kutumia jina halisi hata kwenye mail sio moja ya sheria zao bali the opposite is true?
 
Wakulu mbona mambo mengi yanaeleweaka wazi?

Facebook ni mtandao wa jamii unaounganisha watu mbalimbali kwenye urafiki , masomo na maisha kwa ujumla. Mtumiaji wa Facebook ni lazima aweke anuani pepe ambayo si bandia na atumie jina lolote analopenda.

JamiiForums ni mtandao unaounganisha watu mbalimbali (online discussion site) kwenye kujadili mijadala mbalimbali na mtumiaji ana uchaguzi wa ama kutumia jina halisi au la bandia.

Kwahio basi kule Facebook kama mtu alijisajili kwa kutumia majina bandia na hajulikani kwa wale ambao wanadhani wana wafuasi, Facebook wameamua kufanya usafi.
 
Back
Top Bottom