Face to Face with Zitto Kabwe: Kuhusu Kupika Data, "Namheshimu Sana Rais Magufuli ila Sio Mkweli!. Uchumi Umesinyaa!.

News Alert: - Serikali yamjibu Zitto Kabwe, yasema anapotosha kuhusu takwimu za pato la Taifa

Baada ya serikali kukanusha taarifa hii ya Zitto, hii I namaanisha Zitto amepika data, na kupika data ni kosa la jinai, hivyo sasa tunaisubiria serikali impandishe kizimbani Mhe. Zitto, malumbano haya yakafungwe rasmi.

Paskali
Mkuu kama kila anaeikosoa serikali apelekwe mahakamani sasa nini maana ya kuwa na vyama vya upinzania Tanzania,siasa ni kurumbana,Zitto kaileta hoja kisiasa serikali inapaswa kuijibu hoja kisiasa....,usitupeleke Zimbabwe Mkuu
 
Baada ya serikali kukanusha taarifa hii ya Zitto, hii I namaanisha Zitto amepika data, na kupika data ni kosa la jinai, hivyo sasa tunaisubiria serikali impandishe kizimbani Mhe. Zitto, malumbano haya yakafungwe rasmi.
Afadhali hata wampeleke mahakamani na wavumilie hata kama wakishindwa kumkuta na hatia maana sasa umeibuka umafia wa kutaka kuwaangamiza wakosoaji kwa mitutu ya bunduki kubwa kubwa za kivita baada ya kuwashindwa mahakamani.

[HASHTAG]#HATUTAKI[/HASHTAG] MAFIA STATE
 
Sijaelewa hoja yako hii inahusiana vp na nilichoandika na kwahiyo nimeshindwa hata jinsi ya kujibu!!
Mimi nilielewa ulivyofananisha na kujichanganya kuhusu aliyoyachambua Zitto na kutoa mfano wa kidini, kwamba anakubali baadhi ya data na kuzikataa nyenginezo. Ni wazi hukuelewa kile alichokisema.

Vizuri umekiri kwamba hukuelewa hoja yangu. Ni wazi pia kwamba hukuelewa hoja ya Zitto. Nakushauri uendelee na uamuzi kama huu uliouchukua hapa. Usipoelewa usijibu au omba ufafanuzi. Nakushauri umsikilize Zitto uone kama kulikuwa na ulazima wa kutolea mfano wa ulinganisho wa kidini.

Nimesoma Zitto amekamatwa na Polisi. Hiyo ndio aina ya siri-kali inavyojibu hoja.

Link News Alert: - TEMEKE, DAR: Zitto Kabwe akamatwa na kupelekwa kituo cha Polisi Chang'ombe

Link2. Serikali yamjibu Zitto Kabwe, yasema anapotosha kuhusu takwimu za pato la Taifa
 
Wewe ndio hukunielewa!! Hakuna popote niliposema wala kuashiria kwamba Zitto amejichanganya! Nilianza hoja yangu kwa lugha nyepesi kabisa kwamba:
Halafu upande wa serikali wala sijaona mtu anaeweza kujibu hoja za Zitto kwa kutumia facts and figures!!!
Kwamba, kama hoja ya Zitto ni data zimepikwa basi huwezi kumjibu kwa kutumia data ambazo tayari ana mashaka nazo. Na hapo nikatoa mfano wa ukuaji wa uchumi!

Nikaendelea kusema kwamba, kama unataka kumjibu kwa kutumia data ambazo anaamini zimepikwa basi unatakiwa kwanza kuonesha kwamba data zilizopo ni genuine ili kutengeneza uhalali wa hoja itakayotumia data hizo!!!

Na hapo ndpo nikatumia mfano wa dini kwamba, Mkristo haamini katika Quran! Sasa huwezi kumthibitishia Mkristo kwamba Yesu ni Mungu kwa kutumia reference ya Quran ambayo yeye haiamini!!!

Ukitaka kumthibitishia Yesu ni Mungu wakati reference yako ni Quran unatakiwa kwanza kumwanisha uhalali wa Quran yenyewe or else, tafuta namna nyingine!!

Ukiyatafakari hayo niliyosema ndipo utafahamu ni nani kati yetu anatakiwa kuzingatia kwenye ushauri wako hapo kwenye RED!!!
 
Back
Top Bottom