Zitto Kabwe "draft agreement" sio mkataba

May 3, 2019
53
144
ZITTO KABWE "DRAFT AGREEMENT" SIO MKATABA.

Leo 13:15pm,21/07/2019.

Niliwahi kusema Zitto ndiye aliyehitimu na kupata Gentlemen katika degree yake,na hilo nalithibitisha kwa maandiko yake yanayopinga kwa kutoelewa lugha,kutoelewa uchumi,kwa kutoelewa mahesabu na kwa kutumia ujinga wa Watanzania kutokuwa na taarifa ya jambo basi yeye anatumia nafasi hiyo kuwapotosha.

Zitto aliwahi kutuambia 50/50 ya Economic Benefits ni 50/50 ya Net Profit,hii inadhihirisha kutokuelewa kwake na kuwapotosha sana watu ambao hawana taarifa,hii ni mbaya sana kuwa mpotoshaji ama kujifanya msemaji wa kila kitu hata husichovijua ama ambavyo ulifeli darasani.

-Ushindi Mkubwa wa Rais Magufuli kwa Mabeberu.

Hatimaye Acacia imenunuliwa rasmi na Barrick,Barrick imetangaza kuinunua Acacia,na Acacia wametangaza kununuliwa na Barrick,Tulisema sisi hatuongei na Acacia kwa kuwa ni mtoto kwa Barrick,sisi tunaongea na Barrick watulipe deni la kodi ya dola milioni 300 ama kishika uchumba na sasa yametimia,Acacia aliyepinga hayupo tena kabaki Barrick tuliyekubaliana nae.

-Sasa mgogoro wa Acacia na serikali yetu, umemalizika rasmi kwa sababu sasa Acacia haipo tena,Rais Magufuli kama aliota vile kuingia kwenye mazungumzo na Barrick.

Migodi yote mitatu iliyokuwa chini ya Acacia, sasa itakuwa chini ya Barrick,yale makubaliano na serikali yetu sasa yatatekelezwa.

-Kwa kuanzia tutalipwa dola milioni 300 zilizokuwa ni kishika uchumba, lakini sasa sio kishika uchumba tena bali ni kifuta machozi cha kusamehe lile deni kubwa la kodi la dola bilioni 190.

-Barrick ataunda kampuni mpya ya ubia na Tanzania kuchukuwa shughuli za Acacia
Kwenye hiyo kampuni mpya, serikali ya Tanzania itakuwa na shares asilimia 16%.

-Bodi ya hiyo kampuni mpya itakuwa na Watanzania.
Makao Makuu yatakuwa Tanzania
Menejiment itakuwa na Watanzania.

-Tutagawana manufaa ya kiuchumi pasu kwa pasu, yaani 50/50.(Manufaa ya kiuchumi ni economic benefits na sio faida profits kwa maana ya Net Profit)

-Huu ndio ushindi tuliousubiria,tuachane na maneno ya Wahuni wanaosema tutanunuliwa Noah kila mtanzania.

-Huu ni ushindi wa kwanza wa kishindo wa Rais Magufuli na awamu ya Tano dhidi ya Mabeberu toka tupate Uhuru.

-Hongera Mzalendo Namba mbili Profesa Paramagamba Kabudi.

Tunaanza rasmi utekelezaji wa kwanza wa sheria mpya ya madini,ni mazungumzo yaliyochuku miaka mitatu na sasa tumepata tokeo chanya la kusainiwa makubaliano yenyewe,Mabeberu yamesaini mkataba ambao Watanzania tutapata manufaa y kiuchumi nusu kwa nusu.

-Acacia imekufa na tunafanya na Maziko.

Leo ndo ilikuwa ni siku amabyo Acacia walikubaliana na Barrick juu ya offer waliotoa either kukubali au kukataa. Hatimaye leo Acacia wamekubali kununuliwa na Acacia,Ilikuwa angekataa Offer Watanzania tungechukua mgodi wetu,na kisingetoka kitu iwe dhahabu,Almasi na Tanzanite hadi manufaa ya kiuchumi yawe nusu kwa nusu kati yao wawekezaji na Sisi Watanzania,kwa kweli najivunia kumpata Rais Magufuli na sasa natembea kifua mbele na sitomuogopa mnyonyaji,kupe, beberu wala bepari,Sisi ni Tanzania Mpya.

-Niguse Ninuke

Zitto nakusihi uache ulongo na upotoshaji, Sema kweli hakutakuondolea sifa ya kuwa mpinzani,itakuongezea sifa ya kuwa Mzalendo, sii kweli kuwa mkataba wa makubaliano ya Barrick,Acacia na Tanzania umeisha sainiwa!, hilo neno (initiated) sio kuonyesha kuwa umesainiwa, bali katika mikataba, kunatakiwa signatories watie initials zao kwenye kila page ya draft kuonyesha wameelewa, lakini draft ni draft na mkataba ni mkataba!, ku initiated sio kusaini.

Kwa wapenzi wa Zito kama ndugu yangu George naomba kuwahakikishia, lengo la bandiko hili sio kumuita Zitto Mshamba au kumbagaza Mhe. Zitto, bali ni kumuelimisha tuu na kumtaka awe mkweli kwa kuacha upotoshaji, akiacha upotoshaji Zitto ni kati ya wanasiasa makini na mahiri kabisa na anaweza kula shavu kamba mwanasiasa mwingine mahiri kabisa ndugu Bashe.

Nikiishia hapa,Mimi ni,
Msemakweli Chakubanga.
Dar es Salaam.
 
Zitto anachuja kila uchao,ndagu zinamwisho wake,full kukurupuka,mbaya zaidi kuna kundi la vijana kawaambukiza kukurupuka,ni hatari kwa taifa
 
mnahangaika sana. Ile draft mmeweka mpaka sahihi zenu.

Hiyo ni makubaliano zaidi hata ya kile kilichosemwa pale Ikulu.
 
Chafya imepigwa huko Ccm, Taifa linaumwa

Tuachaneni na mambo ya sijui Acacia sijui Madini, tumalize kwanza hili
 
Hii mijamaa mijinga sana inaonesha haijasoma hata doc yenyewe.
Imetumwa humu kupotosha
 
Umechelewa kijana, ukweli tumeishaujua, nyaraka tumezipata tumezisoma, kawadanganye Lumumba wenzio wavivu was kusoma, pia wasioijua lugha adhimu ya malikia
 
Ngoja nikupe shule dogo, mkataba mpya itakuwa hivi

1. 50 /50 economic benefit ni pamoja na ajira, Kodi, mrahaba, siyo annual profit

2. 16% shares za daraja B, hazina madhara

3. Ushuluhishi wa migogoro ni mahakama za nje kinyume na sheria mpya ya hati ya dharula.

4. $ mil 300 zitalipwa kwa miaka 7

5. VAT refund $ mil.200 itakuwa deducted kwenye kishika uchumba cha $ mil 300
6. Jiwe kasamehe capital gain 20% ya $ bill
458

7. Hakuna mtambo wa kujenjulia makinikia

8. Makinikia yatasafirishwa nje kama kawa

9.bunge haruhusiwa kutunga sheria itakayoathiri uwekezaji kwa muda wote

10..30% shares stock exchange no. Kinyume na sheria ya madini 2010
 
Sentence yako ya kwanza "leo 13:15 pm....."inakatisha tamaa
Nadhani utakuwa umenielewa.
 
Ngoja nikupe shule dogo, mkataba mpya itakuwa hivi

1. 50 /50 economic benefit ni pamoja na ajira, Kodi, mrahaba, siyo annual profit

2. 16% shares za daraja B, hazina madhara

3. Ushuluhishi wa migogoro ni mahakama za nje kinyume na sheria mpya ya hati ya dharula.

4. $ mil 300 zitalipwa kwa miaka 7

5. VAT refund $ mil.200 itakuwa deducted kwenye kishika uchumba cha $ mil 300
6. Jiwe kasamehe capital gain 20% ya $ bill
458

7. Hakuna mtambo wa kujenjulia makinikia

8. Makinikia yatasafirishwa nje kama kawa

9.bunge haruhusiwa kutunga sheria itakayoathiri uwekezaji kwa muda wote

10..30% shares stock exchange no. Kinyume na sheria ya madini 2010

Hiyo namba 9 inaonyesha namna ambavyo jamaa ni mamafia na wanaweza mbele sana.

Nahisi kwenye hayo mazungumzo kuna mahala walitublackmail ikabidi watu wetu wawe wanyonge...
 
haya malizia na haya

30% ya shares kuwa listed DSE ??
tax returns??
arbitration clause n law applicable??

maana ya uzalendo Tanzania ipo tofauti na maeneo mengine duniani.
 
Shenzi, tangu lini draft ikatiwa sahihi? Haya mambo ya kipuuzi mnayatoaga wapi?
 
Hawezi akawa ana dis inform public intentionally halafu uendelee kumuita mwanasiasa MAKINI.
 
Back
Top Bottom