PAYE
JF-Expert Member
- Jun 19, 2025
- 354
- 395
Aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Victoria, Ezekiel Wenje, amesema suala la kwenda kupiga kura si la vyama vya siasa, bali ni la Mtanzania mmoja mmoja kama ilivyoainishwa kwenye Katiba ya Nchi.
Wenje ameyasema hayo leo, Oktoba 28, 2025, katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, wakati wa hitimisho la mikutano ya kampeni za Uchaguzi Mkuu wa 2025 ya mgombea wa urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan.
"Huu uchaguzi ni uchaguzi halali wa kikatiba, umefuata sheria na kuna waangalizi wa kimataifa na ndiyo maana mpaka kesho tutakapoenda kupiga kura hakuna chama chochote cha kisiasa ama mtu yoyote ambaye ameenda mahakamani kupinga kwamba huu uchaguzi ni batili. Tunaenda kwenye uchaguzi halali, wa kisheria na unaosimamiwa kikatiba, twendeni tukapige kura."