External yangu imekataa kusoma ghafla: MSAADA

Michael Ngusa

JF-Expert Member
Aug 4, 2014
1,637
458
Wadau,
External yangu ya Toshiba (500GB) ilikuwa inafunction vizuri tu kama kawaida, leo baada ya kuichomoa na kuiweka kwenye Port ikawa haisomi hadi saivi, nimegoogle nikaambulia ujumbe wa ku uninstall na kuinstall tena driver za USB2.0-CRW lakini hamna ufumbuzi. Nikiweka flash inasoma, ila hii External inaishia kuwaka taa tu kama kawaida yake lakini kwenye Computer haionekani? Msaada tafadhali.
 
Mdau kama umeinunua zaidi ya mwaka mmoja basi iweke ndani ya mfuko laini wa Rambo ifunge vizuri kisha iweke ndani ya friji kwa dakika 2 hadi 3 itoe kisha ijaribu tena. Hakikisha haipati unyevu na iweke mbali na upande ilipo compressor ya friji. Nimefanikiwa mara nyingi njia hii. :mvutaji:
 
are you serious. .?
 
Mkuu mimi niliwahi kupata tatizo linaloelekea kufanana na hili la kwako. Ilinipa taharuki kwani nilikuwa nimehifadhi vitu vingi sana na muhimu kwenye hiyo EHD ya 2 TB. Nilipoulizia wazoefu wakanishauri nibadilishe cable yake. Nilifanya hivyo na mambo yakaenda vizuri.
 
Back
Top Bottom