Experience yangu mbaya na gari za Toyota

JituMirabaMinne

JF-Expert Member
May 4, 2020
3,327
9,321
Katika kufanya diagnosis na kurekebisha matatizo mbali mbali kwenye magari. Asilimia kubwa ya gari nilizokutana nazo ni gari za japan mathalani gari za toyota japo nishakutana pia na gari za ulaya kama BMW, Land Rover na VW na gari za US kama Jeep na Ford.

Experience yangu mbaya kwenye kufanya Diagnosis nmekutana nayo kwenye gari za toyota. Gari za toyota zinachelewa sana kutrigger code (Diagnistic Trouble Code) linapotokea tatizo. Kwa lugha rahisi gari za toyota hasa before 2012 huwa si rahisi sana kuwasha taa ya tahadhari kwenye dashboard au kutrigger code ili ukipima uone.

Kuna case mbili.

Case ya kwanza, Gari inaweza kuwa na shida na haijawasha warning light yoyote ila ukapima ukakutana na code. Hii huwa ina uafadhali.

Case ya pili, Hii ndio mbaya zaidi na ndio mara nyingi huwa inatokea. Gari inakuwa na shida, Haijawasha taa yoyote ya tahadhari na ukipima hukutani na code yoyote.

Nina mifano miwili mikubwa.

Mfano wa kwanza Gari iliyosumbua system ya Immobilizer. Hii gari ni Toyota Avensis ambayo jamaa alikuwa anaiendesha ikaanza kumisi then mwisho wa siku ikazima yenyewe.

Kwenda kuiangalia ikawa inawaka kwa shida sana halafu ikiwaka inakuwa na misi kubwa kana kwamba katika cylinder 4 ni mbili tu ndo kama zinachoma maana misi ya cylinder moja huwa haiwi kubwa vile.

Hiyo siku sikwenda mashine hivyo niliangalia tu kama plug zinachoma ikawa inaonekana zinachoma japo zilikuwa zimechoka. Ile siku kazi ikawa pending tukaamkia siku inayofuata.

Hiyo siku nikaenda na mashine. Ile kupima tu ikaja code moja B2799 - Immobilizer system circuit malfunction. Imagine ECU ilikuwa imetrigger hiyo code lakini taa ya Immobilizer haiwaki kuashiria kwamba kuna tatizo.

Kwa jinsi ile ilivyokuwa inabehave mtu angeweza kubadili kila kitu kwenye engine na bado tatizo likaendelea kuwepo kama kawaida. Kwa maana gari ilikuwa inawaka inakaa hata sekunde 20 halafu inazima yenyewe. Tofauti baadhi ya gari ambazo immobilizer ikileta shida, ukiwasha starter hata haishtuki na taa ya immobilizer inakuwa inablink.

Nilireprogram immobilizer na upya gari ikawa bado inawaka kwa misi ila baada ya kuiendesha umbali fulani kama 8km ikakaa sawa. Na tatizo likawa limeisha.

Mfano wa pili.

Mfano wa pili huu ndio ulikuwa mbaya zaidi kwa maana nmeshakutana na tatizo la aina hii kwenye IST na Rav 4 ( Engine za 2NZ FE, 1ZZ FE na 1AZ FSE)

Simply kuna muda ukikanyaga accelerator kwa nguvu gari inamisi na inakuwa haina nguvu. Na inaweza kuzima kabisa. Au ukiwa unaendesha utaenda umbali fulani ikishapata moto inaanza kumisi halafu inazima.

Case tatu zote ambazo nmekutana nazo za mtindo huo gari haikuwasha check engine wala hakukuwa na code yoyote. Kwenye kucheza na Fuel trim kwenye live Data pamoja na mode 6 data nikaja kugundua misi inasababishwa na mfumo wa Ignition. Ambapo shida ilikuwa kwenye Crankshaft position sensor na nilikuja kujua baada ya kupima resistance yake na kukuta iko out of range.

Ni rahisi gari ya toyota kutrigger code kama waya umekatika lakini kama sensor inafanya kazi ila inatoa info ambazo zipo nje ya range ni mara chache sana toyota inaweza kutrigger code.

Mfano wa mwisho. Ukiikuta Suzuki au Subaru ambayo inachelewa kubadili gear ukipima mara nyingi inakutelea code inayohusiana na incorect gear ration ya gear fulani. Hiki kitu kitu sijawahi kutana nacho kwenye toyota japo katika list ya code za toyota ipo.

Si kama nazikandia Toyota, Hapana. Ninejaribu tu kueleza kile nilichokutana nacho.

Ni tatizo gani gani linakusumbua kwenye gari yako kwa muda mrefu?

View attachment 1784843
 
Swali nje ya mada.

Sababu ya gari kuchelewa kuchanganya ni nini hasa?

Mfano. Ukiwa unataka ku-overtake, ukikanyaga moto mpaka mwisho inasubiri kama sekunde 1 au 2?

Nini sababu?

Hapo shida inaweza kuwa kwenye engine au gearbox.

Mfano hiyo case ninayosema nimekutana nayo kwenye Gari tat, gari mojawapo ndio mtu alikuwa ametoka tu kubadili engine. Ikawa akitaka kuovertake faster gari unakuwa haina nguvu halafu inaweka na misi.

Kwenye Gearbox mara nyingi ni kama gari haibadili gear kwa wakati. Lazima itachelewa kuchanganya. Kuna gari ilikuwa mpaka unafika speed 20 ishaingiza gear namba 3. Hapo gari inakuwa nzito sana kuchanganya mpaka ukifika speed 60 hivi ambapo ndio gear namba 4 ilikuwa inaingia.
 
Incorrect gear ratio ni shida ipo gari zinazotumia CVT.

Kingine hii injini ambazo ukikanyaga accelerator mpaka chini gari ina miss(tatizo hili lilikua kwanye spacio nilio nayo, nili change Mass airflow sensor tatizo likaondoka)
 
Una uhakika kwamba code ya Incorrect gear ratio inatokea kwenye gari zenye CVT tu?

Screenshot_20201031-165630-1.jpg

Hiyo picha nmeattach hapo ilikuwa Suzuki Swift ya 2000 nilikuwa nairekebisha gearbox mwaka jana mwezi wa 10. Ilileta hizo code.

Nmeshapima Subaru mbili ambazo zina transmission ya 4EAT na zikaleta code za incorrect gear ratio. Hizo zote siyo CVT.

Hiyo MAF sensor ulibadilisha baada ya kupima au uliwaza tu itakuwa na shida? Maana matatizo ya maf sensor wala si kazi kutroubleshoot
 
Una uhakika kwamba code ya Incorrect gear ratio inatokea kwenye gari zenye CVT tu?

View attachment 1785903

Hiyo picha nmeattach hapo ilikuwa Suzuki Swift ya 2000 nilikuwa nairekebisha gearbox mwaka jana mwezi wa 10. Ilileta hizo code.

Nmeshapima Subaru mbili ambazo zina transmission ya 4EAT na zikaleta code za incorrect gear ratio. Hizo zote siyo CVT.

Hiyo MAF sensor ulibadilisha baada ya kupima au uliwaza tu itakuwa na shida? Maana matatizo ya maf sensor wala si kazi kutroubleshoot
Nilipima sikupata any DTC yoyote, so nkachomoa wire harness ya MAF of course ika trigger check engine light but engine hesitation ikawa gone uki press gas pedal instantly... Nkagundua nipo na fault MAF sensor.. (engine code ni 1NZ ipo kwenye spacio)

Kuhusu issue ya incorrect gear ratio nime experience kwenye gari iliyo na cvt gear box... Ambapo gearbox ilikufa baada ya muhuni mmoja kunichanganyia transmission fluid.. so ikawa inapata shida ya kupata correct gear ratio inayoendana na road conditions na engine rpm..

Note(sikuwa na jua kama gari ya normal/traditional ATF inaweza kua na trouble code ya gear ratio kwakua gear box zake zinakuja na fixed gear ratio.

But nashukuru kwa kuniongezea maarifa mkuu.
 
Katika kufanya diagnosis na kurekebisha matatizo mbali mbali kwenye magari. Asilimia kubwa ya gari nilizokutana nazo ni gari za japan mathalani gari za toyota japo nishakutana pia na gari za ulaya kama BMW, Land Rover na VW na gari za US kama Jeep na Ford.

Experience yangu mbaya kwenye kufanya Diagnosis nmekutana nayo kwenye gari za toyota. Gari za toyota zinachelewa sana kutrigger code (Diagnistic Trouble Code) linapotokea tatizo. Kwa lugha rahisi gari za toyota hasa before 2012 huwa si rahisi sana kuwasha taa ya tahadhari kwenye dashboard au kutrigger code ili ukipima uone.

Kuna case mbili.

Case ya kwanza, Gari inaweza kuwa na shida na haijawasha warning light yoyote ila ukapima ukakutana na code. Hii huwa ina uafadhali.

Case ya pili, Hii ndio mbaya zaidi na ndio mara nyingi huwa inatokea. Gari inakuwa na shida, Haijawasha taa yoyote ya tahadhari na ukipima hukutani na code yoyote.

Nina mifano miwili mikubwa.

Mfano wa kwanza Gari iliyosumbua system ya Immobilizer. Hii gari ni Toyota Avensis ambayo jamaa alikuwa anaiendesha ikaanza kumisi then mwisho wa siku ikazima yenyewe.

Kwenda kuiangalia ikawa inawaka kwa shida sana halafu ikiwaka inakuwa na misi kubwa kana kwamba katika cylinder 4 ni mbili tu ndo kama zinachoma maana misi ya cylinder moja huwa haiwi kubwa vile.

Hiyo siku sikwenda mashine hivyo niliangalia tu kama plug zinachoma ikawa inaonekana zinachoma japo zilikuwa zimechoka. Ile siku kazi ikawa pending tukaamkia siku inayofuata.

Hiyo siku nikaenda na mashine. Ile kupima tu ikaja code moja B2799 - Immobilizer system circuit malfunction. Imagine ECU ilikuwa imetrigger hiyo code lakini taa ya Immobilizer haiwaki kuashiria kwamba kuna tatizo.

Kwa jinsi ile ilivyokuwa inabehave mtu angeweza kubadili kila kitu kwenye engine na bado tatizo likaendelea kuwepo kama kawaida. Kwa maana gari ilikuwa inawaka inakaa hata sekunde 20 halafu inazima yenyewe. Tofauti baadhi ya gari ambazo immobilizer ikileta shida, ukiwasha starter hata haishtuki na taa ya immobilizer inakuwa inablink.

Nilireprogram immobilizer na upya gari ikawa bado inawaka kwa misi ila baada ya kuiendesha umbali fulani kama 8km ikakaa sawa. Na tatizo likawa limeisha.

Mfano wa pili.

Mfano wa pili huu ndio ulikuwa mbaya zaidi kwa maana nmeshakutana na tatizo la aina hii kwenye IST na Rav 4 ( Engine za 2NZ FE, 1ZZ FE na 1AZ FSE)

Simply kuna muda ukikanyaga accelerator kwa nguvu gari inamisi na inakuwa haina nguvu. Na inaweza kuzima kabisa. Au ukiwa unaendesha utaenda umbali fulani ikishapata moto inaanza kumisi halafu inazima.

Case tatu zote ambazo nmekutana nazo za mtindo huo gari haikuwasha check engine wala hakukuwa na code yoyote. Kwenye kucheza na Fuel trim kwenye live Data pamoja na mode 6 data nikaja kugundua misi inasababishwa na mfumo wa Ignition. Ambapo shida ilikuwa kwenye Crankshaft position sensor na nilikuja kujua baada ya kupima resistance yake na kukuta iko out of range.

Ni rahisi gari ya toyota kutrigger code kama waya umekatika lakini kama sensor inafanya kazi ila inatoa info ambazo zipo nje ya range ni mara chache sana toyota inaweza kutrigger code.

Mfano wa mwisho. Ukiikuta Suzuki au Subaru ambayo inachelewa kubadili gear ukipima mara nyingi inakutelea code inayohusiana na incorect gear ration ya gear fulani. Hiki kitu kitu sijawahi kutana nacho kwenye toyota japo katika list ya code za toyota ipo.

Si kama nazikandia Toyota, Hapana. Ninejaribu tu kueleza kile nilichokutana nacho.

Ni tatizo gani gani linakusumbua kwenye gari yako kwa muda mrefu?

View attachment 1784843
Gari Aina ya Chevrolet Cruze Engine M13a nikipaki nikija kuwasha inakuwa Ina tetemeka hasa nikiweka Reverse Gear alaf baada ya mda inatulia Yani nikiiendesha,plug nimebadili,nozzel nmesafisha,sijui shda Nini mkuu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilipima sikupata any DTC yoyote, so nkachomoa wire harness ya MAF of course ika trigger check engine light but engine hesitation ikawa gone uki press gas pedal instantly... Nkagundua nipo na fault MAF sensor.. (engine code ni 1NZ ipo kwenye spacio)

Kuhusu issue ya incorrect gear ratio nime experience kwenye gari iliyo na cvt gear box... Ambapo gearbox ilikufa baada ya muhuni mmoja kunichanganyia transmission fluid.. so ikawa inapata shida ya kupata correct gear ratio inayoendana na road conditions na engine rpm..

Note(sikuwa na jua kama gari ya normal/traditional ATF inaweza kua na trouble code ya gear ratio kwakua gear box zake zinakuja na fixed gear ratio.

But nashukuru kwa kuniongezea maarifa mkuu.
Umetumia tatizo moja ulilokutana nalo la CVT kutoa hitimisho kuhusu CVT. Mitandaoni maelezo mengi inabidi mtu uyachuje.
 
Ni kwann gearbox za nissan zenye CVT zinaaminika kuwa hazidumu zaidi ya km 130? Hii nimekutana nayo sana mitandaoni.

Yes kuna malalamiko mengi sana kuhusu gearbox za CVT kwa nissan japo siyo gari zote lakini kuna matoleo kadhaa ambayo watu wengi wamekuwa wakilalamikia kwamba gearbox zinazumbua.

Mathalani gearbox za Nissan ambazo zimetengenezwa na Jatco ambaye ndio mzalishaji mkubwa wa gearbox nyingi za Nissan.
 
Garage yako ipo maeneo gani?
 
Asante.... Kwa experiense yako ni brand zipi za nissan za kuavoid.. maana kwa japan mm ni mpenzi wa nissan hizi pathfinder, navara, murano yenye engine q35 six cylinder si hizi 4 cylnder. Na kama ninayo nn cha kufanya iwe salama?
 
Back
Top Bottom