Experience yangu kama baby moma

Experience yangu kama baby moma

Hakuna haja ya kulalamika wakati umechagua mwenyewe tena kwa vigezo ulivyoviweka ambavyo unaamini ni sahihi. Jambo lolote negative likitokea ujilaumu mwenyewe kabla ya kumlaumu mwingine kwani bila wewe hayo yasingetokea.
Sio kulalamika tatizo ni MTU kukwepa majukumu ya kulea hyo ya vigezo hailalishi kukwepa majukumu.
 
Yaani haya maneno ndio ya busara....

Sema wengine ni masikio ya kufa...




Afu nimeamini dhambi ya kutoka na mume/mke wa mtu itakutafuna tu,haijalishi inapita muda gani.Niliachana na mume wa mtu wala hata sikutubu nikaona nimemaliza,ila haikupita muda dhambi ile nimeilipia.Siwashauri mabinti kutoka na married guys,machozi ya mkewe utayalipia tu.
 
Hivi unaweza kupata mtoto ukawa depressed real? mmm im just thinking out loud ...like u have your own image yet u feel sad..cmon just enjoy being a mom no matter what..Jikubali mdada.
 
Hivi unaweza kupata mtoto ukawa depressed real? mmm im just thinking out loud ...like u have your own image yet u feel sad..cmon just enjoy being a mom no matter what..Jikubali mdada.

Ajikubali wapi wewe mtoto usiekuwa ukintaka lazima utapagawa tuu.
 
Sasa ushauri bure...usizae tena na mwanaume mwengine...tulizana tuu.
 
Wadada kuweni makini mijianaume ya sikuhizi ni zaidi ya ibilisi anakuzalisha then anakutema hapo unakuwa umrkongoroka yeye anaenda kuoa mwingine. Bora kusubiria ndoa tu ili mulee mtoto vizuri. Kwanza kuwa single parent Ku raise child ni issue. Wanawake kuweni makini

Alafu.....
Nimejikuta napenda sana wadada ambao tayari walikwisha zaa maana naamini ndio kwanza wamekomaa. Chaajabu sijui kwanini nikigundua kidada bado hakija zaa nakiona kana kwamba bado hakija pevuka akili aiseeee
 
Wala tu hamna mwanaume au mwanamke anayedharaulika wala kudharaulika haku determine future nzuri. Pia kiburi ni tabia tu ya MTU jinsi alivolelewa kuna wanaopendwa na yet wanajiheshimu hawadharau MTU. Pia life halina principles hao wazuri ukiona hawaolewi ujue hawajapata MTU sahihi wa kuwaoa.
Mbona hata wabaya huoa na kuolewa kuanzia wafupi ukiona HVO ujue walipata perfect choice na match ya real life. Ndo mana kila mtu ana criteria zake akiongeza na upendo basi kitu INA tick.

Haya maneno ya Mzuri/ M-baya, kiukweli nimekua nikichanganyikiwa sana kwa kutokujua vigezo na tofauti ya Mzuri na Mbaya.
Please help
 
Nikiri tu kuwa kabla ya kuwa baby mama about 2 years ago,nilikuwa mtu wa bata sana hapa mjini.By that time nishamaliza chuo na nimeajiriwa nikiwa na miaka 3 kazin kwenye ofisi flan hapa town,so kiaina flan nilikuwa nishajipanga,usafiri wa maana,plots kama tatu namiliki ,moja nikiwa nimefikisha nyumba kwenye linta,nimepanga full house maeneo flan jijini nikiishi na house girl tu.kimahusiano nilikuwa natoka na workmate ambaye ameoa akiwa na watoto 3 ambaye niliajiriwa nikamkuta kwenye hiyo ofisi.Akarusha ndoano mwanzoni nilimkataa ila alikomaa na kupitia mashosti nikajikuta nimeingia kwenye 18 zake.Hivyo kimtindo nilikuwa free kujirusha mwishoni mwa wiki manake jamaa wikendi alikuwa anaspend na familia yake.Alikuwa bize nami anzia j3 hadi ijumaa,ndo tulikuwa tunaspend some quality time together.

Niliendelea na maisha hayo,ila baadaye yakaanza niboa kutokana na kelele za mashosti,again kuhusu kumzalia jamaa(mume wa mtu) mtoto.sikuliafiki hilo suala isitoshe jamaa alikuwa nami kuenjoi maisha,nami sikuwa tayari kuzaa na mume wa mtu.kutoka naye ni dhambi ya kwanza,sikuwa tayari kuongeza dhambi nyingine ya uzao,so nilikuwa makini sana.Na nikiri jamaa alinispoil sana kiasi kwamba nilijua nikibeba mimba tu nitaharibu.

Katika kutoka huko na mashosti sometimes na workmates,siku moja workmate akaja na rafiki yake,kijana flan amazing,black kaenda hewani,akamuintroduce.binafsi nilivutiwa naye katika kumdadis nikagundua jamaa ndo kagraduate bado yuko kitaa anatafuta kutoka.Tukabadilishana mawasiliano.Wikend kama mbili tukatoka nao,workmate pamoja na jamaa.Nikamdadis kuhusiana na mahusiano akanambia alikuwa girl ila washaachana kila mtu na maisha yake,na huyo girl kwasasa yuko mkoa.Kiukwel niliona ndo chance ya mimi kuanza mahusiano na kijana mwenzangu aliye free na kuachana na mume wa mtu.

Sikuwa na haraka ya kujuana na kijana,niliazimia kumsoma kwanza kabla ya kuanzisha lolote.Hivyo ilikuwa kampani ya gambe na mziki tu wikendi.katika mitoko hiyo nikagundua jamaa anapiga maji sana afu anaishi sinza,akitoka kwenye mihangaiko ye ni baa baa na yeye.Basi nikapunguza mawasiliano kimtindo,manake niliona hatutofika mbali.

Ikapita mwezi kila akinitafuta nampiga kalenda,siku moja akaniibukia kwangu kwani niliwahi mkaribisha.Akawa analalamika kama nimeonyesha interest afu nikapotezea,sikuona sababu ya kumficha nikamweleza nimekusoma nikaona ka hatutaendana.Mwenzangu mtu wa starehe sana,huna wikendi afu mie nataka kutulia nijenge family.Akanambia hamna hisia zako tu,mie nakaa bar daily kwakuwa sijapata mtu wa kueleweka kufanya naye life.Kama huamini ntabadilika kukuonyesha niko serious.

Nikamwambia kama kweli kwanza hama sinza,ndani ya mwezi hilo akalikamilisha.Yule mume wa mtu nikakata mawasiliano naye mdogomdogo,kwani nilikuwa serious kustart afresh.Ila sikuwahi kumwambia kama nilikuwa natoka na married guy.Afu nimeamini dhambi ya kutoka na mume/mke wa mtu itakutafuna tu,haijalishi inapita muda gani.Niliachana na mume wa mtu wala hata sikutubu nikaona nimemaliza,ila haikupita muda dhambi ile nimeilipia.Siwashauri mabinti kutoka na married guys,machozi ya mkewe utayalipia tu.

Basi mapenzi motomoto yakaanza na kijana,mwanzoni niliinjio sana,kujali,kampani na attention ya mpenzi niliipata kwa asilimia 100.Nikawa mtu wa furaha sana kila kiwanja na marafiki zake wakanijua,akawa ananitambulisha kama wife wake.Ilikuwa haraka sana kwa kweli,kutahamaki ndani ya miezi 2 nikajigundua ni mjamzito.Lahaula nilichanganyikiwa kwani haikuwa plan yangu.Plan ilikuwa nikatambulishwe kwao na kwetu wamjue ,uchumba then ndoa.

Ila kabla ya kugundua ni mjamzito,jamaa akaanza kama kuadimika hivi,wakati huo na yeye ashapata kazi mambo yamemnyookea.Nikawa mpole nasikilizia ni mimba kweli ama mabadiliko tu ya mwili.Vipimo vya mimba vya pharmacy vinasema mimba,nikaenda hospital kuconfirm wakanambia sina mimba,mwezi wa 3 huo toka tufahamiane.Ila nikiangalia mechi za simba sipati tena na si kawaida.

Nikaongea na shosti akanipeleka kwa dokta wake bingwa,kupiga ultrasound,majibu yakatoka ni mjamzito.Nikamwita jamaa nikamweleza,akaniuliza,unaamuaje?Nikamwambia nipe wiki nifikirie,ila kabla sijakujibu mipango ya kwenda kwenu vipi?akanambia bado sana ndo kwanza ameanza maisha.Baada ya wiki tukakutana nikamjibu kuwa nitazaa.Akaniuliza una uhakika?nikamjibu ndiyo,huyu mtoto hana hatia nitazaa.Akasema poa,uzuri unakazi na unajimudu.
Basi jamaa baada ya kujua ni mjamzito,ikawa kama ndo nimemfukuza mazima.Nikimpigia simu zangu hata hapokei tena,sms hajibu,inshort akakata mawasiliano nami.Kuna wakati nilifikiria kuabort,nikaenda church nikalia sana na kusali.Nilipotoka nikaenda kwa school mate wangu kumwelezea uamuzi naotaka chukua.School mate akanisihi nisifanye hivyo,hapo mimba ina miezi 4.Basi nikarudi home na kuendelea lea mimba mwenyewe.Kumbe kipindi jamaa ananipotezea alisharudia na yule girl wake.Na vile mambo yake yalikuwa supa haikuwa shida kurudiana.
Mimba ilipotimiza miezi 7,nakumbuka ilikuwa dec 2014 ,jamaa akarudisha mawasiliano kwangu.Akasema anafanya kwaajili ya mwanae etc nikamwamini,akawa anakuja kwangu twice a week,napika tunakula tunalala.Nikajua Mungu kanisamehe dhambi yangu kamrudisha,kumbe wakati huo anajiandaa mpeleka yule girl wake kwao kumtambulisha.Kweli December 2014 akaenda kwao ila akaniomba nimwongezee hela zimempungukia.Nikampa nikijua we on the same page.Akaniahidi kurudi kabla sijajifungua.Lakin siku naumwa uchungu na majirani kunikimbiza hospital,yeye alikuwa anamtolea binti yule mahari.Nimekuja yajua haya yote baada ya mwaka kupita ,tena ndugu yake wa damu ndo alinipa huo ukweli mchungu.Ni mwaka wa pili sasa nalea mtoto peke yangu.Si rahisi kama watu wasemavyo.Kwanza nilipozaa tu kidogo nidate kwani nilipata depression.So being a single mom si rahisi hata kidogo.Haijalishi una pesa.
Pole sana shemeji, amini yatapita na furaha itachelewa lakini itarudi sehem yake.
Kuna scenario moja kama hiyo ila jamaa aliyeoa mkewe akawa hana uwezo wa kuzaa ikabidi aokoke na arudi kwa yule aliyemtelekeza na mtoto.
 
huwa nachukia sana kuona mwanamke anakupenda kweri kwa nia ya kutaka kufanya life na wewe araf mwanaume unamuongopea kwa kwenda kuoa mwingne mara nyingi hii hupelkea wanawake wengi kuwa sugu moyoni(roho mbaya katika mapenxi)7bu hapo babyboma jins ulipofikia mpk uruhusu kupenda kweri mwanaume inabidi boy afanya kazi ya ziada kwerikweri

araf mnaoponda kihusu kuchagua ooh mnapenda maboy wa zuri au magero wa zuri kusema ukweri huwezi kufanya maisha na mwanamke au mwanaume asiyekuvutia hata kama ni mzuri kiasi gan kila mtu ana vigezo vyake kwa mwenzi anayetaka kufanya naye maisha mfn mm demu hata uwe na figa nzuri kiasi gani yaan kitendo cha wewe kujichubua tu na mkorogo kwangu huwezi kupata nafasi hata ya kukumbatiana na pia haiwezekani mtoto mzuri wa mjini akatoka na mbugilambugila anayepiga pamba ka za kofi olomide bwana !

sasa nini cha kufanya kwa magero ukimpenda boy ukahisi ana sifa za kuwa mumeo usijilahisishe ukampa K ng'ang'ania ndoa kama kakupenda atakuoa tu ka kipindi kile wakati zamani na kauli za kishujaa (hatufanyi mpk tuoane)

maMEN je msikimbilie Kutaka K kwanza wala msimwage ahadi nyingi msizoweza kuzitekeleza kuwa NATURAL kwa hali ya maisha yako uliyo nayo tu yaan pia msionge sana MKE MWEMA ANUNULIWI

Babymoma Piga moyo konde lea mwenyewe mtoto hata kuja kukutunza UZEENI midhari unaweza kujimudu mshkuru MUNGU na muombe siku zote yeye na mtumaini yeye
wapo wanaume wengi tu wanahitaji mwamamke kama wewe naimani utapata huu mwaka hautaisha Trust Me dada !!


huyo boy alokutenda atapigwa na laana ya mapenzi atakujutia maisha yake yote

ila ni baba wa mtoto wako kamwe usimwombee mabayaa
Mkuu ndoa siyo vocha kuwa ukitaka unakwangua unaiweka sa hivi au baadaye itaingia... Mungu atusaidie
 
Baby moma weye si wa kwanza. Mwombe Mungu akusaidie na jitume zaidi kufanya kazi ili ulee mtoto katika maadili mema
 
.Ni mwaka wa pili sasa nalea mtoto peke yangu.Si rahisi kama watu wasemavyo.Kwanza nilipozaa tu kidogo nidate kwani nilipata depression.So being a single mom si rahisi hata kidogo.Haijalishi una pesa.
NI ukweli ambao kwa baadhi hawapendi kuusikia.

Bila shaka kuna kitu watajifunza.
 
Mimba ilipotimiza miezi 7,nakumbuka ilikuwa dec 2014 ,jamaa akarudisha mawasiliano kwangu.Akasema anafanya kwaajili ya mwanae etc nikamwamini,akawa anakuja kwangu twice a week,napika tunakula tunalala.Nikajua Mungu kanisamehe dhambi yangu kamrudisha,kumbe wakati huo anajiandaa mpeleka yule girl wake kwao kumtambulisha.Kweli December 2014 akaenda kwao ila akaniomba nimwongezee hela zimempungukia.Nikampa nikijua we on the same page.Akaniahidi kurudi kabla sijajifungua.Lakin siku naumwa uchungu na majirani kunikimbiza hospital,yeye alikuwa anamtolea binti yule mahari.Nimekuja yajua haya yote baada ya mwaka kupita ,tena ndugu yake wa damu ndo alinipa huo ukweli mchungu.Ni mwaka wa pili sasa nalea mtoto peke yangu.Si rahisi kama watu wasemavyo.Kwanza nilipozaa tu kidogo nidate kwani nilipata depression.So being a single mom si rahisi hata kidogo.Haijalishi una pesa.
Duuh pole sana Baby moma mathalani yashatokea huna budi kukubaliana na hali halisi. Lea mtoto wako kwa upendo na ujipende wewe mwenyewe pia... Maisha ndio kwanza yameanza usikate tamaa, kwa kuwa ushapitia magumu nadhani next time hutaacha makosa hayo yatokee tena kiurahisi..
Akupendaye yupo njiani anakuja na utapata suuziko la moyo maradufu.

Nakushauri usimfikirie yule mme wa mtu na wala usijilaumu sana kwa kilichotokea mathalani umekiri kuwa ulikosea basi jutio lako limepata msamaha hata kwenye mamlaka kuu..

Huyo baba wa mtoto naye potezeana naye usimuwaze na usimkaribishe karibu yako, kama atakua anajali atoe hela ya matunzo na maisha yaendelee...

Nikiri nimejisikia vibaya nilipo comment kwa mara ya kwanza kwa kukudhiaki maana uandishi wako umekaa kimachale...

Pole sana...
 
Sasa ushauri bure...usizae tena na mwanaume mwengine...tulizana tuu.
Hiyo ni shule tosha ya maisha, atubu kwa aliyofanya huko nyuma, atulia alee mtoto wake, yeye si wa kwanza kukumbana na mambo kama hayo na naamini Mwenyezi Mungu atampa mume "wake". Wale wengine walikuwa si wake, alidandia tu!
 
Back
Top Bottom