Nikiri tu kuwa kabla ya kuwa baby mama about 2 years ago, nilikuwa mtu wa bata sana hapa mjini. By that time nishamaliza chuo na nimeajiriwa nikiwa na miaka 3 kazin kwenye ofisi flan hapa town, so kiaina flan nilikuwa nishajipanga, usafiri wa maana, plots kama tatu namiliki, moja nikiwa nimefikisha nyumba kwenye linta, nimepanga full house maeneo flan jijini nikiishi na house girl tu.
Kimahusiano nilikuwa natoka na workmate ambaye ameoa akiwa na watoto 3 ambaye niliajiriwa nikamkuta kwenye hiyo ofisi. Akarusha ndoano mwanzoni nilimkataa ila alikomaa na kupitia mashosti nikajikuta nimeingia kwenye 18 zake.
Hivyo kimtindo nilikuwa free kujirusha mwishoni mwa wiki manake jamaa wikendi alikuwa anaspend na familia yake. Alikuwa bize nami anzia j3 hadi ijumaa, ndo tulikuwa tunaspend some quality time together.
Niliendelea na maisha hayo, ila baadaye yakaanza niboa kutokana na kelele za mashosti, again kuhusu kumzalia jamaa(mume wa mtu) mtoto. Sikuliafiki hilo suala isitoshe jamaa alikuwa nami kuenjoi maisha, nami sikuwa tayari kuzaa na mume wa mtu.
Kutoka naye ni dhambi ya kwanza, sikuwa tayari kuongeza dhambi nyingine ya uzao, so nilikuwa makini sana. Na nikiri jamaa alinispoil sana kiasi kwamba nilijua nikibeba mimba tu nitaharibu.
Katika kutoka huko na mashosti sometimes na workmates, siku moja workmate akaja na rafiki yake, kijana flan amazing, black kaenda hewani, akamuintroduce. Binafsi nilivutiwa naye katika kumdadis nikagundua jamaa ndo kagraduate bado yuko kitaa anatafuta kutoka. Tukabadilishana mawasiliano.
Wikend kama mbili tukatoka nao, workmate pamoja na jamaa. Nikamdadis kuhusiana na mahusiano akanambia alikuwa girl ila washaachana kila mtu na maisha yake,na huyo girl kwasasa yuko mkoa. Kiukwel niliona ndo chance ya mimi kuanza mahusiano na kijana mwenzangu aliye free na kuachana na mume wa mtu.
Sikuwa na haraka ya kujuana na kijana, niliazimia kumsoma kwanza kabla ya kuanzisha lolote. Hivyo ilikuwa kampani ya gambe na mziki tu wikendi. Katika mitoko hiyo nikagundua jamaa anapiga maji sana afu anaishi Sinza, akitoka kwenye mihangaiko ye ni baa baa na yeye. Basi nikapunguza mawasiliano kimtindo, manake niliona hatutofika mbali.
Ikapita mwezi kila akinitafuta nampiga kalenda, siku moja akaniibukia kwangu kwani niliwahi mkaribisha .Akawa analalamika kama nimeonyesha interest afu nikapotezea, sikuona sababu ya kumficha nikamweleza nimekusoma nikaona ka hatutaendana. Mwenzangu mtu wa starehe sana, huna wikendi afu mie nataka kutulia nijenge family.A kanambia hamna hisia zako tu, mie nakaa bar daily kwakuwa sijapata mtu wa kueleweka kufanya naye life. Kama huamini ntabadilika kukuonyesha niko serious.
Nikamwambia kama kweli kwanza hama sinza, ndani ya mwezi hilo akalikamilisha. Yule mume wa mtu nikakata mawasiliano naye mdogomdogo, kwani nilikuwa serious kustart afresh. Ila sikuwahi kumwambia kama nilikuwa natoka na married guy. Afu nimeamini dhambi ya kutoka na mume/mke wa mtu itakutafuna tu, haijalishi inapita muda gani.
Niliachana na mume wa mtu wala hata sikutubu nikaona nimemaliza, ila haikupita muda dhambi ile nimeilipia.S iwashauri mabinti kutoka na married guys, machozi ya mkewe utayalipia tu.
Basi mapenzi motomoto yakaanza na kijana, mwanzoni niliinjio sana, kujali, kampani na attention ya mpenzi niliipata kwa asilimia 100.
Nikawa mtu wa furaha sana kila kiwanja na marafiki zake wakanijua ,akawa ananitambulisha kama wife wake. Ilikuwa haraka sana kwa kweli, kutahamaki ndani ya miezi 2 nikajigundua ni mjamzito. Lahaula! Nilichanganyikiwa kwani haikuwa plan yangu. Plan ilikuwa nikatambulishwe kwao na kwetu wamjue, uchumba then ndoa.
Ila kabla ya kugundua ni mjamzito, jamaa akaanza kama kuadimika hivi, wakati huo na yeye ashapata kazi mambo yamemnyookea. Nikawa mpole nasikilizia ni mimba kweli ama mabadiliko tu ya mwili. Vipimo vya mimba vya pharmacy vinasema mimba, nikaenda hospital kuconfirm wakanambia sina mimba, mwezi wa 3 huo toka tufahamiane. Ila nikiangalia 'mechi za simba sipati tena na si kawaida.
Nikaongea na shosti akanipeleka kwa dokta wake bingwa, kupiga ultrasound, majibu yakatoka ni mjamzito. Nikamwita jamaa nikamweleza, akaniuliza unaamuaje? Nikamwambia nipe wiki nifikirie, ila kabla sijakujibu mipango ya kwenda kwenu vipi? Akanambia bado sana ndo kwanza ameanza maisha.
Baada ya wiki tukakutana nikamjibu kuwa nitazaa. Akaniuliza una uhakika? Nikamjibu ndiyo, huyu mtoto hana hatia nitazaa. Akasema poa, uzuri una kazi na unajimudu.