Huu ni mkataba ambao Uvccm waliupeleka kwenye baraza kuu lililofanyika Dodoma na wamekubaliana kuusaini na uliosainiwa utawekwa hapa baadae kwani wanatukwamisha na mtajua ni kwanini mafuta hayashuki bei.
IDARA YA UTAWALA, UCHUMI NA FEDHA.
2. (II) MCHAKATO WA UBIA WA KIWANJA NA. 2 "AA"MCHIKICHINI ILALA – DAR ES SALAAM.IDARA YA UTAWALA, UCHUMI NA FEDHA.
Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam ulikaribisha Maombi kwa Wawekezaji wenye nia ya kuendeleza kiwanja chao kilichopo Ilala – Mchikichini chenye Hati namba 24 ‘AA' Dar es Salaam.
Katika kikao cha Baraza Kuu la UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam lililokutana tarehe 13/01/2010 kilipokea taarifa kwamba wawekezaji watatu wameomba kuwekeza ambao ni;
(a) Camel Oil Ltd
(b) World Oil
l(c) Lake Oil
Baada ya kupitia maombi ya wawekezaji Baraza Kuu la UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam lilimpitisha Camel Oil kuingia naye Ubia, na hivyo kuyawasilisha mapendekezo katika vikao vya UVCCM Taifa na Baraza la Wadhamini wa UVCCM kwa uamuizi wa mwisho.
Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la UVCCM Taifa ilipokea pendekezo la UVCCM Mkoa wa DSM la kuingia Ubia na Camel Oil na kuelekeza kwamba Mwekezaji alete michoro na gharama za ujenzi. Pia aonyeshe faida itakayopata UVCCM na makubaliano haya yatadumu muda gani. Pia ilielekeza Mwekezaji ajenge si chini ya ghorofa sita badala ya tatu alizoomba mwanzo na kwa kufuata taratibu na Sheria za Mipango Miji.
UVCCM umepokea kukubali kwa Mwekezaji kuingia Ubia na UVCCM na kuleta mapendekezo ya aina mbili.
(i) Camel Oil ameomba kujenga kituo cha Mafuta (Petrol Station) katika nusu ya eneo la kiwanja, na nusu nyingine atajenga Jengo la apartments lenye ghorofa sita kwa ajili ya biashara kama mchoro unavyojionyesha katika alternative one. Eneo la kiwanja hiki ni mita za mraba 3,595.
Gharama yote ya mradi huu katika pendekezo hili ni Tshs. 3,064,300,000 kama mchanganuo wake unavyosomeka katika kiambatanisho chake.
Ø Katika pendekezo hili la Mradi, Ujenzi wake utakamilika katika kipindi cha miezi 36 mara tu baada ya kupata vibali vyote vya Ujenzi toka katika mamlaka husika. UVCCM utanufaika kwa kupata……………………….na Mbia tapata ……………… katika sehemu ya………………… na katika sehemu ya kituo cha mafuta, UVCCM atafaidika kwa………………. Na Mwekezaji atapata faida ya…………….. Mkataba huu utadumu kwa kipindi cha miaka 30.
Ø Mbia (Camel Oil) ataupatia UVCCM Mkoa wa DSM jumla ya Shs. 78,000,000/= ambazo zitatumika kufidia gharama za mpangaji wa sasa ili eneo liweze kuwa wazi tayari kwa kujenga. Mara baada ya kukamilika ujenzi, UVCCM utaweka utaratibu wa kumrudishia kiasi cha Tshs. 39,000,000/= na zinazobaki katika Tshs. 78,000,000/= yaani 39,000,000/= utakuwa ni mchango wake wa kufanikisha eneo kuwa wazi.
Ø Mbia atakuwa anaulipa UVCCM kiasi cha Tshs. 1,300,000/= kama kodi kwa kipindi chote cha ujenzi hadi hapo Ujenzi utakapokamilika. Fedha hizi hazitarudishwa.
Ø Mbia atalipia gharama zote za kubadili matumizi ya ardhi na kufanya kuwa kituo cha Mafuta
Ø Hatatumia Hati ya UVCCM kukopea Benki ili kupata mtaji wa kujengea
Ø Mara baada ya miaka 30 Mkataba utafikia ukomo na Camel Oil ataomba kupangishwa.
(ii) Hoja ya aina ya pili ya Uwekezaji inatokana na ukweli kwamba ili aweze kujenga kituo cha Mafuta lazima aombe kubadili matumizi ya ardhi katika Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi. Hivyo basi Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la UVCCM Taifa ilimtaka Mbia alete pendekezo la pili endapo ombi la kujenga kituo cha mafuta halitakubaliwa.
Ø Katika kuwasilisha pendekezo la mradi wa Ubia na UVCCM, Camel Oil amependekeza ajenge majengo mawili yenye ghorofa sita kila moja. (Two Twin Towers). Gharama ya Ujenzi katika Mradi huu ni Tshs. 3,054,460,000/= na kwamba ujenzi utakamilika katika kipindi cha miezi 36 kuanzia tarehe ya kupata kibali cha ujenzi toka mamlaka zinazohusika. Majengo haya yote yatakuwa na ukubwa unaofanana.
UVCCM utapata mapato yake katika Jengo moja na Mwekezaji atapata mapato yake katika Jengo moja. Yaani UVCCM utamiliki 50% na Mbia atamiliki 50% na Mkataba utadumu kwa kipindi cha miaka 30.
Ø Mbia (Camel Oil) ataupatia UVCCM Mkoa wa DSM jumla ya Shs. 78,000,000/= ambazo zitatumika kufidia gharama za mpangaji wa sasa ili eneo liweze kuwa wazi tayari kwa kujenga. Mara baada ya kukamilika ujenzi, UVCCM utaweka utaratibu wa kumrudishia kiasi cha Tshs. 39,000,000/= na zinazobaki katika Tshs. 78,000,000/= yaani 39,000,000/= utakuwa ni mchango wake wa kufanikisha eneo kuwa wazi.
Ø Mbia atakuwa anaulipa UVCCM kiasi cha Tshs. 1,300,000/= kama kodi kwa kipindi chote cha ujenzi hadi hapo Ujenzi utakapokamilika. Fedha hizi hazitarudishwa.
Ø Mbia atalipia gharama zote zinazohusiana na mchakato wa Ujenzi, ikiwa ni pamoja na kupata vibali vya Ujenzi.
Ø Mbia hatatumia Hati ya UVCCM kukopea Benki ili apate mtaji wa kujengea mradi huo.
Ø Mara baada ya miaka 30 Mkataba kati ya UVCCM na Mbia utakoma na Mbia ataomba kupangishwa.