EXCLUSIVE: Ushirikiano wa Makampuni ya Mafuta na CCM

EXCLUSIVE: Ushirikiano wa Makampuni ya Mafuta na CCM

Kama ni cha moto sasa watanzania tunakipata sawia. Ccm na kikwete wake ni janga. Dr. Slaa alituasa tukampuuza.

Acheni mijungu,
Badala ya kuconcentrate kutafuta vitegauchumi na kuimarisha chama, mnaangaika na maandamano kila siku.
CDM hawajui wanachokifanya.

Lakini watu wanashangaza; walipewa nafasi ya kuchagua 2010 wakaamua kuwarudisha; sasa kinachonishangaza kuwa hata watu waliowapigia kura nao wanaanza kujifanya wanashangaa kana kwamba hawakujua watakachokipata. Inashangaza.
inauma sana kukirudisha madarakani chama hiki licha ya wanaharakati na chadema kutuasa kati ya dhambi ambaya ambayo tunge ifanya ni kuirudisha ccm madarakani leo miezi tisa baadae tunajuta na bado..sijui mpaka 2015 itakuwaje

Gamba ni ccm yenyewe ambayo ni full suit toka mwenyekiti hadi mwananchama wa kawaida, akina RACHEL ilikuwa ni kiini macho tu. Alichokuwa anahangaikia(EPA,Kagoda etc) RA ni kutafuta pesa za kufanikisha issues za chama. Kama alikuwaanafaidika
basi ni mgao lakini pesa zilikuwa
zinatoka kwa directives za ccm. Ndiyo maana RA kakasirika na wanambembeleza kwa sababu wanajua hana kosa kwa vile alikuwa tu anatumika na chama lakini uchafu wote ni wa viongozi wakuu wa chama na serikali.

Mbaya zaidi kinachoonekana hapa ni pesa za chama lakini nyingi huishia kugawanwa na wakubwa. Pesa kidogo tu hutumika kufanikisha chaguzi za chama kama kununulia chumvi na kanga na Tshirt. Ndiyo maana kitu cha muhimu sana kwenye ccm ni mtu kuwa kwenye zile ngazi za maamuzi kama CC na NEC ili migao hii ikupitie lasivyo hupati kitu.

Kwa msingi huu EL na ACH hawataweza kuwatoa kwa nguvu ni lazi,a wawavumilie tu mpaka watakapokubali wenyewe maana wanajua hawana makosa wao kama wao ila wamechafuka vile kwa sababu walikuwa wanafanya kazi za chama na watu wengi wamenufaika na kazi yao.

Kama Tanzania inataka kujenga nchi ,pya ni lazima watanzania tujivue gamba lote ambalo ni ccm. Bila hivyo tutakwisha wote na vizazi vyetu sisi tulio masikini.

Kama kweli kuna watu wenye uchungu na hii nchi basi ni lazima tuwaunge mkono wapinzani wa kweli kwa nguvu zetu zote. Mungu ametupa kuyajua mambo mengi kwa muda huu mfupi ambao cdm wamekuwa kazini. CDM wanafanya kazi yao vizuri na sisi tuwaunge mkono kw maana CDM ikifa basi tunarudishwa square zero tena na watatutafuna mapaka mifupa yetu.

Tafakari, chukua hatua!

Wafanyabiashara waliichangia CCM saizi wanamake ndio maana wanaichimba mkwara serikali na inanywea ujinga mtupu halafu mtu anasimama bungeni na kuanza kuisifu serikali ya CCM this iz houliganism...........................................................

Imeandika kwa utulivu mkubwa sana, ni vigumu kwa wanafiki kukuelewa lakini binafsi nimekusoma sana na hivyo sina haja ya kuandika kwani hii post yako inatosha.

Gamba ni ccm yenyewe ambayo ni full suit toka mwenyekiti hadi mwananchama wa kawaida, akina RACHEL ilikuwa ni kiini macho tu. Alichokuwa anahangaikia(EPA,Kagoda etc) RA ni kutafuta pesa za kufanikisha issues za chama. Kama alikuwaanafaidika

basi ni mgao lakini pesa zilikuwa

zinatoka kwa directives za ccm. Ndiyo maana RA kakasirika na wanambembeleza kwa sababu wanajua hana kosa kwa vile alikuwa tu anatumika na chama lakini uchafu wote ni wa viongozi wakuu wa chama na serikali.

Mbaya zaidi kinachoonekana hapa ni pesa za chama lakini nyingi huishia kugawanwa na wakubwa. Pesa kidogo tu hutumika kufanikisha chaguzi za chama kama kununulia chumvi na kanga na Tshirt. Ndiyo maana kitu cha muhimu sana kwenye ccm ni mtu kuwa kwenye zile ngazi za maamuzi kama CC na NEC ili migao hii ikupitie lasivyo hupati kitu.

Kwa msingi huu EL na ACH hawataweza kuwatoa kwa nguvu ni lazi,a wawavumilie tu mpaka watakapokubali wenyewe maana wanajua hawana makosa wao kama wao ila wamechafuka vile kwa sababu walikuwa wanafanya kazi za chama na watu wengi wamenufaika na kazi yao.

Kama Tanzania inataka kujenga nchi ,pya ni lazima watanzania tujivue gamba lote ambalo ni ccm. Bila hivyo tutakwisha wote na vizazi vyetu sisi tulio masikini.

Kama kweli kuna watu wenye uchungu na hii nchi basi ni lazima tuwaunge mkono wapinzani wa kweli kwa nguvu zetu zote. Mungu ametupa kuyajua mambo mengi kwa muda huu mfupi ambao cdm wamekuwa kazini. CDM wanafanya kazi yao vizuri na sisi tuwaunge mkono kw maana CDM ikifa basi tunarudishwa square zero tena na watatutafuna mapaka mifupa yetu.

Tafakari, chukua hatua!

umeandika kwa utulivu mkubwa sana, ni vigumu kwa wanafiki kukuelewa, binafsi nimekusoma na hivyo sioni haja ya kuandika chochote kwani post yako inatosha mkuu.

KINACHOTUTAFUNA TANZANIA HADI HIVI SASA NCHINI NI UKOSEFU WA UONGOZI ADILIFU NA KUKOSEKANA UTAWALA BORA KIUTENDAJI

Ni ajabu na kweli kuona jinsi ambavyo watawala wanavyoenenda katika shughuli zao za kila siku. Kama mtu bado huamini tu basi hebu tu wewe mwenyewe tupe JIBU hapa jukwani.

Hebu jaribu kutufahamisha kama kweli hali halisi kama ilivyoainishwa hapo chini kweli itasaidia kukuza MASLAHI YA UMMA katika nchi hii au ni ukuta wa kuendeleza MASLAHI BINAFSI kwa kutupora sisi kama taifa:

Mpaka hapa mtu kweli unategemea WATUMISHI WETU huko serikalini kweli watawezaje kufanya kazi yao ipasavyo na kwa mujibu wa sheria zetu bila kupindapinda pale unapomkuta mkuu wa nchi tayari katamalaki kila upande kiasi cha kuona;

1. Kikwete Mwenyekiti wa CCM Taifa

2. Akitupa geresha za Kumuagiza Kikwete Rais na Kiongozi wa Serikali ili naye

3. Akumamrishe yule Kikwete Mfanyabiashara wa mafuta pale Lake Oil akapunguze bei ya mafuta.

Ewe Mzee Wassira, kwa nini hamkuliona hili na kumshauri mkuu wa nchi; DHANA YA UTAWALA BORA sasa uko wapi hapa??? Mbona kinyaa hivi!!!!!!!!!!!!

Mzee Simbeye, Wakuhenga, Warioba, Kubenea, Mjengwa na Jenerali Ulimwengu, nyinyi kama wakosoaji wa jamiiyetu hii hili hamkuliona???????

Kweli kabisa mtu ukijitwisha kofia hizi zote tatu na kujizivalia umaridi kabisa wewe mtu mmoja tu, Dr Hosea, kweli bado kunakosekana hali ya MGONGANO WA KIMASLAHI ambao hivi sasa inasababisha Watanzania tuliowengi kuwa WALAZWAHOI.

Hapana, Hapana na Hapana; hatutaki tena wala hutusikii cha mtu hapa - ulaghai na ufisadi sasa basi mwishoooo!!!! Mpaka hapa wala mtu huitaji kuwa na elimu ya hata sekondari kugundua kwa nini mambo kila siku hayaendi kwa njia nyoofu huko serikalini badala yake watu kuzunguka tu mbuyu; kumbe kuna Joka kuu katamalaki na kuenea kila kona!!!

Watanzania wenzangu, ni kati ya Kikwete yupi kati ya hao watatu atakayeweza kupata kweli ujasiri na uhalali wa kumdhibiti yule Kikwete mwingine?????

Mbona tunachezewa shere siku zote hivi nchini na bado tu watu hatuoni haya yote????????????? Je baada ya kusoma na kutafakari haya niliyoyaandika hapo juu:

1) Je, bado unayo imani na Hoja ya Dharura ya Januari Makamba kule bungeni Dodoma??

2) Je, bado unategemea kusikia kutolewa kwa agizo lolote na serikali yetu na ikazingatiwa???

3) Je, mpaka hapo bado unaamini kuwa EWURA ni chombo cha kulinda maslahi yetu Umma wa Tanzania????

4) Je, kwa hiyo hali hapo juu na ukipiga picha na kwingineko kama eneo la matatizo sugu ya maji, maliasili na umeme nchini bado tu utakua unaamini kweli kwamba Dr Hosea bado anayo meno ya kuweza kutafuna mtu au kampuni yoyote hapa nchi kwa madai ya UFISADI???????????????????

Tafakari zaidi na zaidi na mwisho ujishauri mwenyewe jinsi UTAKAVYOTUMIA HAKI YAKO YA KUPIGA KURA siku za usoni!!!!!!!!!!

Salute Mkuu.

Lakini watu wanashangaza; walipewa nafasi ya kuchagua 2010 wakaamua kuwarudisha; sasa kinachonishangaza kuwa hata watu waliowapigia kura nao wanaanza kujifanya wanashangaa kana kwamba hawakujua watakachokipata. Inashangaza.

Mwanakijiji naomba niwatetee watanzania uchaguzi uliopita. They voted out CCM. Wakabaka demokrasia. Labda kama tuwalaumu kwa kuface mabomu kulazimisha matokeo halali yatangazwe. Lakini kura walipiga vizuri.

jamani watanzania tunasubiri nini? twendeni tahirr square kwa kishindo kikubwa ili kuyatoa haya majangili hayafai hata kuwa tanzania.

TAIFA LITAJENGWA NA WENYE MOYO!!!!

Acheni mijungu,
Badala ya kuconcentrate kutafuta vitegauchumi na kuimarisha chama, mnaangaika na maandamano kila siku.
CDM hawajui wanachokifanya.

UVCCM walitafuta lini vitega uchumi zaidi ya kuendelea kufaidika na ule mfumo wa chama kimoja ambapo assets zote ilizonanzo zilichangwa na watanzania wote bila yakujali itikadi ya vyama?, kama ni usawa; mali zote zilizopatikana kipindi hicho aidha zirudi serikalini au zigawiwe kwa vyama vyote vya siasa...heri Chama tawala kinachojua kinachofanya kwa kuvimbishiwa na wauza mafuta leo ikiwa ni siku ya 8...

Ndio maana wana jeuri hawa watu.
Ila hayo ndio mavuno ya tulichokipanda.

RA sawa na paa lililoezuka. Sasa inyeshe mvua, liwake jua, utoke ukungu, kila kwetu kitajulikana.

mkuu ungeiscani kama JPG ili saini za hao mafirauni zionekane. Wengine humu ndani ni wanachama wa jumuiya hii na pengine viongozi umkini safari ya kwenda Tahrir squire ya Bongo ianzie kwenye issue kama hizi. Ki ufupi haturiziki na yanayoendelea ndani ya kijiwe hiki cha CCmagambazazi

Wabongo tumezoea kulalamika, kunung'unika na kusikitika hata ukiwekewa
kidole machoni, am sure wengi wetu tumepitia JKT, tunajua kutumia zana mbali mbali,
tunajua mbinu za medani nk.Twendeni front kama wenzetu wanavyofanya, it is very easy to get rid of these stupid
Fisadis, ni waoga mno hawa jamaa. Let us mobilize ourselves and others, huu ndio wakati
muafaka, hawawezi kuondoka wenyewe hata kama itawashinda kabisa.

Acheni mijungu,
Badala ya kuconcentrate kutafuta vitegauchumi na kuimarisha chama, mnaangaika na maandamano kila siku.
CDM hawajui wanachokifanya.
we kipara ngoto sikuelewagi!!sometimes unatetea magamba,sometimes unajipendekeza CDM,mbona uko kama mwanamke ma**y*??kuwa baridi au chumvi,ukiwa vuguvugu utatapikwa!!....bloody f**l

Kuna haja ya upinzani kuanza kuclaim back hizi mali za CCM maana hizi mali zilipatikana enzi ya mfumo wa chama kimoja ambapo hata wapinzani walichangia katika kuzipata. Kwa maana hiyo ofisi zote za CCM, viwanja, stadium na kumbi zote wanazoziita za CCM zinatakiwa zitaifishwe ili kuweza kupata mgao sawa wa rasilimali yetu. Haiwezekani, mali tutafute wote, lakini CCM ndo waendelee kuneemeka nayo.

yes ccm ni TRA,ni wizara zote,ni migodi,ni vitalu,ni mbuga,ni wajeshi nk nk...

Back
Top Bottom