Exclusive Live updates:Simba Fc vs Mbeya City

Exclusive Live updates:Simba Fc vs Mbeya City

zubedayo_mchuzi

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2011
Posts
4,873
Reaction score
1,221
Leo leo wale wakare wapya kwenye mchuano huu unaoendelea,na walomtoa jASHO BINGWA mtetezi Dar Yanga leo wanatupa tena upinde wao kuona je wanaweza kumchezea sharubu Simba...

utwalubunju...

Stay alert...Simba fc vs Mbeya City
 
Leo leo wale wakare wapya kwenye mchuano huu unaoendelea,na walomtoa jASHO BINGWA mtetezi Dar Yanga leo wanatupa tena upinde wao kuona je wanaweza kumchezea sharubu Simba...

utwalubunju...

Stay alert...Simba fc vs Mbeya City

Ila usije ukalala mbele kwenye kutupasha habari kiongozi wengine tupo mikoani.
 
Ila usije ukalala mbele kwenye kutupasha habari kiongozi wengine tupo mikoani.
Hahahahahaha.
Nadhani umesahau kale kamsemo ka zamani kwamba ukianzisha ugomvi na nyuki basi uwe na speed ya kukimbia.
 
mechi inayosubiriwA KWA hamu ni ya hawa jamaa MBEYA CITY.....wakiwa kwao walipata sare,sasa je na simba watasimama......

Leo tutamlipia mtani wetu, ukiona kijana anataka kumuadhiri mzee mwenzako inabidi uingilie kati kumtetea mzee mwenzako, kwa hiyo leo tunajipanga kumlipia mzee mwenzetu, Mbeya City lazima wajue tofauti ya ligi kuu na ligi daraja la kwanza, kwa kifupi leo ndo kipimo chao kwenye ligi kuu, wakipona leo basi watang'aa kama dhahabu maana Simba hii ni tanuru tosha.
 
...kwa upande wa TEMEKE hali ya hewa ni nzuri kama tupo ARUSHA vile...jua hakuna na sasa hivi kuna ka mvua kana pita ni ishara ya ushindi kwa timu fulani...
 
kwani leo kuna mechi moja tu ya ligi kuu?

...Leo ni kama ifuatavyo, pia kesho na...

Wakati vinara Simba wakiwakaribisha Mbeya City kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Uwanja wa Mkwakwani, Tanga utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Mgambo Shooting Stars na Rhino Rangers ya Tabora. Mtibwa Sugar itakuwa mgeni wa Tanzania Prisons katika pambano litakalochezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
Nayo Kagera Sugar itakuwa nyumbani kwenye uwanja wake wa Kaitaba mjini Bukoba kuvaana na Ashanti United ya Dar es Salaam katika mechi itakayochezeshwa na mwamuzi Jacob Adongo kutoka Mara.
Ligi hiyo itakamilisha mzunguko wa tano kesho (Septemba 22, 2013) kwa mechi tatu ambapo Azam na Yanga zitacheza Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam huku JKT Ruvu ikikwaruzana na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Azam Complex.
Ruvu Shooting inayokamata nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi itakuwa mgeni wa Coastal Union katika mechi itakayopigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
===
Wakati huo huo, Ligi Daraja la Kwanza (FDL) inaendelea wikiendi hii kwa mechi kumi na moja. Kundi A leo (Septemba 21, 2013) kutakuwa na mechi kati ya Transit Camp na Green Warriors (Uwanja wa Karume, Dar es Salaam), Tessema na African Lyon (Uwanja wa Mabatini, Mlandizi).
Ndanda itacheza na Villa Squad kwenye Nangwanda Sijaona mjini Mtwara wakati kesho (Septembe 22, 2013) kutakuwa na mechi kati ya Polisi Dar es Salaam na Friends Rangers katika Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Kundi B leo (Septemba 21, 2013) ni Mkamba Rangers dhidi ya Burkina Faso kwenye Uwanja wa CCM Mkamba, na Mlale JKT itakuwa mwenyeji wa Kurugenzi Mafinga kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea. Kesho (Septemba 22, 2013) ni Majimaji na Kimondo katika Uwanja wa Majimaji.
Mechi za kundi C leo (Septemba 21, 2013) ni Pamba dhidi ya Polisi Dodoma (Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza), Stand United na Polisi Tabora (Uwanja wa Kambarage, Shinyanga) na Kanembwa JKT itacheza na Mwadui kwenye Uwanja wa Kawawa ulioko Ujiji. Kesho (Septemba 22, 2013) Polisi Mara na Toto Africans zitacheza Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma.

Source: Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
 
mechi inayosubiriwA
KWA hamu ni ya hawa jamaa MBEYA CITY.....wakiwa kwao walipata sare,sasa
je na simba watasimama......

sawa, ila ili jukwaa ni la sport, timu sio YANGA na simba tu, watu wanataka updates za timu nyingine pia kwan kwa ujumla wao ndio zinafanya uwepo wa ligi kuu ya tanzania, ni vizuri kuweka mechi zote na kuzi update pia.
 
...Leo ni kama ifuatavyo, pia
kesho na...

Wakati vinara Simba wakiwakaribisha Mbeya City kwenye Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam.
Uwanja wa Mkwakwani, Tanga utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Mgambo
Shooting Stars na Rhino Rangers ya Tabora. Mtibwa Sugar itakuwa mgeni wa
Tanzania Prisons katika pambano litakalochezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya
Sokoine jijini Mbeya.
Nayo Kagera Sugar itakuwa nyumbani kwenye uwanja wake wa Kaitaba mjini
Bukoba kuvaana na Ashanti United ya Dar es Salaam katika mechi
itakayochezeshwa na mwamuzi Jacob Adongo kutoka Mara.
Ligi hiyo itakamilisha mzunguko wa tano kesho (Septemba 22, 2013) kwa
mechi tatu ambapo Azam na Yanga zitacheza Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
huku JKT Ruvu ikikwaruzana na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Azam Complex.
Ruvu Shooting inayokamata nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi itakuwa
mgeni wa Coastal Union katika mechi itakayopigwa kwenye Uwanja wa
Mkwakwani jijini Tanga.
===
Wakati huo huo, Ligi Daraja la Kwanza (FDL) inaendelea wikiendi hii kwa
mechi kumi na moja. Kundi A leo (Septemba 21, 2013) kutakuwa na mechi
kati ya Transit Camp na Green Warriors (Uwanja wa Karume, Dar es
Salaam), Tessema na African Lyon (Uwanja wa Mabatini, Mlandizi).
Ndanda itacheza na Villa Squad kwenye Nangwanda Sijaona mjini Mtwara
wakati kesho (Septembe 22, 2013) kutakuwa na mechi kati ya Polisi Dar es
Salaam na Friends Rangers katika Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Kundi B leo (Septemba 21, 2013) ni Mkamba Rangers dhidi ya Burkina Faso
kwenye Uwanja wa CCM Mkamba, na Mlale JKT itakuwa mwenyeji wa Kurugenzi
Mafinga kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea. Kesho (Septemba 22,
2013) ni Majimaji na Kimondo katika Uwanja wa Majimaji.
Mechi za kundi C leo (Septemba 21, 2013) ni Pamba dhidi ya Polisi Dodoma
(Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza), Stand United na Polisi Tabora (Uwanja
wa Kambarage, Shinyanga) na Kanembwa JKT itacheza na Mwadui kwenye
Uwanja wa Kawawa ulioko Ujiji. Kesho (Septemba 22, 2013) Polisi Mara na
Toto Africans zitacheza Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma.

Source: Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Asante mkuu'
 
Waambieni hao MGAMBO wa Jiji la Mbeya kua, Uwanja wa Taifa hawauzi Viroba!

Salam wameshazipata toka kwa kaka zao Mgambo wa Tanga!
 
... Ofisa Habari wa Simba anena!

MCL leo... "Mbeya City yapiga hodi Simba"

mbeya.jpg

Wachezaji wa Mbeya City wakipasha kabla ya mechi.

...Simba inashuka leo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kukabiliana na Mbeya City , lakini inafahamu kwamba inahitaji pointi tatu ili iweze kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara.
Wekundu hao wa Msimbazi, wanakamata usukani wa ligi hiyo wakiwa na pointi 10, lakini wanasakamwa kwa karibu na JKT Ruvu iliyoko nafasi ya pili na pointi tisa, sawa na ndugu zao
Ruvu Shooting ambao pia wana pointi tisa lakini wakitofautiana kwa idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa.
Kama itafanikiwa kuvuna pointi tatu kwenye mchezo wa leo, Simba itafikisha pointi 13 huku mabingwa watetezi, Yanga watajiuliza upya mbele ya Azam kesho baada ya kuandamwa
na mdudu wa sare katika mecvhi tatu mfululizo.
Hata hivyo, ushindi wa pointi tatu haitakuwa rahisi kwa Simba bila jitihada za dhati, kwani Mbeya City nayo imethibitisha kwamba haitishiki kwa ukongwe hasa baada ya kuivimbia
Yanga kwa kutoka nayo sare ya bao 1-1.
Mbeya City ambayo imefuzu kucheza Ligi Kuu kwa mara ya kwanza msimu huu imeng¡¯ang¡¯ania katika nafasi ya saba ikiwa na pointi sita, huku ikiwa haijapoteza mchezo hata mmoja.
Kocha wa Simba, Abdallah Kibadeni¡±King¡± ambaye mchezo wa mwisho alichekelea ushindi mnono wa mabao 6-0 dhidi ya Mgambo JKT amejitapa kuifundisha soka Mbeya City kwa
kuibuka na ushindi kwenye kipute cha leo.
Naye Kocha wa Mbeya City, Juma Mwambusi amedai kutotishika na maneno ya mpinzani wake baada ya kusema yupo tayari kwa vita na kuibuka mbabe.
Katika hatua nyingine, Uongozi wa Simba umesema hauna matatizo na Mbeya City na kutaka timu hiyo iimarishiwe ulinzi zaidi.

Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema jana kuwa kuna kikundi cha watu ambao wamejipanga kuvaa jezi nyekundu na kufanya vurugu kwenye mchezo wao wa leo ili
kulipiza kisasa.
¡°Kuna mamluki wa Yanga ambao wamejipanga kuvaa jezi nyekundu na kuwafanyia vurugu Mbeya City, tungeomba jeshi la Polisi chini ya Kamanda Kova, kuimarisha zaidi ulinzi,¡±
alisema Kamwaga.

¡°Wasituchanganye sisi vyovyote, iwe tufungwe, tutoke sare kwetu ni matokeo na tutajipanga kwa mechi nyingine na kama kuna watu wanataka kulipiza kisasa wasubiri ikifika zamu yao,
tunaomba jeshi la Polisi liimarishe ulinzi hasa kwa Mbeya City.
Utamu wa ligi hiyo utakolezwa na mechi zingine tatu zitakazopigwa sehemu tofauti ikiwaemo Bukoba, ambako Kagera Sugar itakuwa nyumbani kwenye Uwanja wa Kaitaba kuumana na Ashanti, wakati Mgambo itakuwa nyumbani kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga kupimana ubavu na Rhino Rangers, hali kadhalika Prisons itakuwa mwenyeji wa Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Source: Mwananchi
 
kwa kuweka kumbukumbu sawa mwezi kama huu mwaka 1998 Yanga alikula 6-0 na Raja Casablanca.
 
Waambieni hao MGAMBO wa Jiji la Mbeya kua, Uwanja wa Taifa hawauzi Viroba!

Salam wameshazipata toka kwa kaka zao Mgambo wa Tanga!

huyu jamaa amekuja kuwashika
 

Attachments

  • simba katuni ya tambwe na hat trick.jpg
    simba katuni ya tambwe na hat trick.jpg
    81.7 KB · Views: 297
hapa tayari nishamaliza kusomaJF na kazi zingine kwenye PC, jezi nyekundu ipo kwenye kamba inakauka, naenda kuoga, kulana huyoo kuyoyoma uwanjani kushuhudia mnyama akiua watoto
 
sawa, ila ili jukwaa ni la sport, timu sio YANGA na simba tu, watu wanataka updates za timu nyingine pia kwan kwa ujumla wao ndio zinafanya uwepo wa ligi kuu ya tanzania, ni vizuri kuweka mechi zote na kuzi update pia.

Mleta thread yuko Dar atatoaje updates za mechi za Tanga, Kagera et el. Walio kwenye viwanja vingine waanzishe threads nyingine watu update.
 
Back
Top Bottom