Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
Rais Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuongoza mkutano wa nchi tano za Afrika ya Mashariki katika kile ambacho kinaaminiwa juhudi ya nchi hizo kukabiliana na mmonyoko wa kiuchumi duniani. Mkutano huo utakaozihusisha nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi unatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu au mapema mwezi wa tano.
Kwa mujibu wa habari za ndani toka Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje, Mkutano huu unatarajiwa kuwa ni wa kupanga mikakati na hatua za kukabiliana na matatizo yakiuchumi ambayo tayari yameanza kuonekana katika nchi hizo kufuatia kuporomoka kwa uchumi katika nchi wafadhili za Kimagharibi zikiongozwa na Marekani.
"Viongozi wametambua kuwa hawawezi kusubiri nchi wafadhili kuja na mipango ya kuokoa nchi za Kiafrika kiuchumi wakati wao viongozi wa Taifa wana uwezo wa kufanya mambo kadha wa kadha kwa juhudi zao wenyewe" amesema mdokezaji wetu kwa masharti ya kutotajwa jina kwani habari hizo hazijatangazwa rasmi.
Kwa mujibu wa msemaji huyo, wazo la kuzikutanisha nchi hizi ni la Rais Kikwete ambaye kutokana na mkutano wa IMF/WB uliofanyika nchini, mkutano wake na Waziri Mkuu wa Uingereza Bw. Gordon Brown na matokeo ya mkutano wa nchi 20 tajiri zaidi duniani ameona kuwa nchi za Afrika ya Mashariki zinaweza kabisa kupanga na kufadhili programu kubwa za maendeleo ambazo zitasisimua uchumi wa nchi hizo na kuongeza ulaji wa ndani, na uzalishaji wa bidhaa kwa soko la nje.
Naye afisa wa Mambo ya Nchi za Nje Charles Kimau toka Kenya amesema kuwa wazo hilo la mkutano huo tayari limefikishwa kwa Rais Kibaki na limepokewa na wao Kenya wako tayari kushiriki katika mkutano huo. Bw. Kimau alisema kuwa mkutano huo kwa kweli umechelewa na nchi yake iko tayari itashiriki ipasavyo katika kukamilisha.
Kutoka Uganda afisa mmoja toka Ikulu ya Nakasero Uganda aliyejitambulisha kwa jina moja tu la Ssemogerere amesema kuwa Uganda tayari wamepokea mwaliko na majibu yao ya awali ni kuwa wako tayari kushiriki katika mkutano huo. Toka Rwanda na Burundi majibu ni hayo hayo kwamba nchi hizo ziko tayari kufuata uongozi wa Rais Kikwete katika suala hili na watatoa ushirikiano wote.
Pamoja na kuwa mkutano huu unazihusu nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki nchi nyingine pia zimeonesha nia ya kutaka kuwa washiriki au waalikwa. Baadhi ya nchi hizo ni pamoja na Msumbiji, DRC, Visiwa vya Comoro na Ethiopia.
Kwa mujibu wa afia aliyetudokeza mkutano huo una lengo la kupanga mkakati wa kuinua uchumi wa nchi hizi hasa katika kipindi hiki ambacho kiukweli ni kipindi muafaka kwa kuanzisha miradi mikubwa ya kiuchumi ambayo itachochea ajira, kuboresha huduma mbalimbali, na kujenga nchi hizo kuelekea mataifa ya kisasa.
"Huu ni wakati wetu" alisema ofisa huyo kwa kujiamini. "Nchi za Kiafrika ni kweli hazijachangia sana katika mmomonyoko wa uchumi wa dunia lakini ukweli ni kuwa ni kwa sababu hazichangii sana katika uchumi wa dunia!" Kutokana na mchango huu kidogo wa Afrika ni wazi kuwa sauti ya bara hili haisikiki sana. "Fikiria kuwa GDP ya Bara zima la Afrika haifikii GDP ya jimbo la California huko kwenu Marekani" alisema afisa huyo. "Sasa kwanini watusikilize" alihoji kiudadisi.
Ni kutokana na ukweli huo, kwa upande wa Afrika nchi hizi ambazo zinaelekea kuwa shirikisho zinataka kuunganisha nguvu zake katika shughuli za uzalishaji mali, kuinua soko la ndani na kupanua bidhaa zao kwa soko la nje. Kwa mujibu wa mmoja wa waandaji wa mkutano huo, utakapofikia mwisho viongozi hao wanatarajia kutia sahihi makubaliano ambayo yanatazamiwa kuhusisha mambo makubwa yafuatayo:
a. Kuanzisha programu kubwa ya ujenzi wa miundombinu ya kisasa kwa kukusanya nguvu za mataifa hayo. Katika hili nchi hizi zinatarajiwa kuanzisha ujenzi wa barabara kubwa za kisasa za kuunganisha kila mkoa na mkoa katika nchi hizo katika mfano wa "Interstate Highways Project" wa Marekani chini ya Rais D. Eisenhower. "Tukiweza kuunganisha nchi zetu kwa mtandao wa barabara kubwa tutakuwa tumepiga hatua moja muhimu.
b. Kuanzisha mfuko maalum wa kuchochea uchumi ambapo fedha za ndani tu zitatumika. Mfuko huo unatarajiwa kukusanya dola bilioni moja. Tanzania imesema iko tayari kutoa dola milioni 400 kuanzisha mfuko huo ambao matumizi yake yataelekezwa katika kuinua na kuboresha kilimo cha umwagiliaji, kuchochea utafiti na ubunifu katika Sayansi na Teknolojia kupitia taasisi mbalimbali za kisomi, kuweka mitandao ya Internet bila nyaya kwenye miji mikubwa yote ya nchi hizo n.k.
c. Kuanzisha mabadiliko ya kisheria na uboreshaji wa taasisi za kiusalama ili kukabiliana na uhalifu wa fedha. Mojawapo ya mradi ambao unapendekezwa ni kujengwa kwa gereza jipya lenye kazi ngumu na usalama wa juu (maximum security) litakalochukua wahalifu wa kiuchumi katika maeneo ya Afrika ya Mashariki. Pia uboreshaji wa taasisi za usalama wa Taifa kwa kuanzisha mtandao wa kikompyut utakaounganisha taasisi za Kipolisi kuziwezesha kuwa na mawasiliano ya moja kwa moja ndani ya nchi za jumuiya hiyo.
d. Kutengeneza sera ya pamoja ya misaada ya kigeni ili hatimaye nchi hizo ziondokokane na utegemezi wa misaada ya kigeni katika bajeti zao. "lengo ni kuhakikisha kuwa nchi hizi zinaweza kufadhili bajeti zao wenyewe kwa asilimia mia moja, huku misaada yote ya kigeni ikienda na kuendeshwa na sekta binafsi bila kuingiliwa au kuingizwa serikalini" alisema ofisa huyo. "Katika kufikia lengo hilo, utaratibu mpya wa ukusanyaji, na udhibiti wa kodi unatarajiwa kubuniwa hasa kwa kuzingatia makubaliano ya kodi ya Afrika ya Mashariki ambazo kodi nyingi zitakuwa karibu zinalingana na hivyo kuwa na mchakato bora na wa kisasa wa ukusanyaji kodi.
e. Kufanya tathmini ya maliasili na utajiri wa asili wa nchi hizi ili hatimaye kuweza kuona ni mikataba gani ya uwezekaji haina manufaa na ifutwe ili hatimaye nchi hizi ziwe na msimamo na mwelekeo wa pamoja katika suala zima uwekezaji wa moja kwa moja wa fedha za kigeni (FDI). "Tuna utajiri mwinginei na hazina nyingi lakini mashirika makubwa ya kimataifa yanatumia ukimya wetu kutunyonya na kwa kweli kama kutunyonya wametunyonya; tunataka kurudi kwenye kukata mirija hii ya kiunyonyaji" alisema ofisa huyo.
Hata hivyo licha ya taarifa hizo baadhi ya watu kutoka Ikulu ya Dar-es-Salaam ambao wameulizwa juu ya mkutano huo wamekanusha kuwepo kwa mpango huo wakisema kuwa "tayari tumeshakutana na IMF/WB, tumekutana na Brown na mapendekezo yaliyotolewa na Rais kwa G20 yamepokelewa na kama unavyoona G20 wameahidi zaidi ya kile tulichowaomba, sasa mkutano wa sisi wa nini".
Afisa huyo alihoji ulazima wa mpango huo kama ulivyodokezwa akionesha kukerwa kuwa habari kama hizo zinavuja mapema na kusikitika kuwa kwa mtindo huo "mnafanya kazi ya watendaji serikalini kuwa ngumu sana, kwani hakuna siri yoyote". "Kama mpango wa mkutano huo kuwepo au kutokuwepo, hayo ni maswala ambayo yana wakati wake, sijui kwanini mnapenda kutafuta udaku wa kisiasa namna hii" alisema na kukata simu.
Naye afisa mmoja mwingine mwandamizi toka wizara ya mambo ya nchi za Nje alisema kuwa hana taarifa ya mkutano huo kwani ndiyo kwanza wamemaliza mikutano mingine na kuwa hakuna sababu ya kuwa na mkutano wa aina hiyo. "Tayari nchi wafadhili wamekubali kutusaidia na watatusaidia sana sasa sisi tuje na mipango hiyo mikubwa yote ya nini?" Alihoji katika hali ya kushangazwa agenda ambayo tuliidokeza kuwa tumeipata. "Hiyo mipango ni mikubwa sana kwa nchi zetu changa na maskini, labda mnaota ndoto" alisema kwa sauti ya kejeli.
Wakati huo huo, taarifa kutoka Jijini Dar zinadokeza kuwa mchakato wa kuendelea kuwafikisha watuhumiwa mbaliimbali wa ufisadi unatarajiwa kuendelea muda si mrefu hasa baada ya siku za hivi karibuni kuonekana kuna ukimya wa aina fulani huku baadhi ya watu wakidai kuwa "mafisadi wote wameshafikishwa mahakamani".
Kwa mujibu wa chanzo chetu, ruhusa iliyokuwa inasubiriwa imeshatolewa ya kuendelea na kusanya kusanya ya mafisadi na raundi inayokuja inatarajiwa kushtua taifa kwa wale watakaofikishwa kizimbani. "Hata hivyo, bado la kuangalia ni mashtaka gani yataletwa, kwani hii pia inaweza kuwa mbinu ya kuwasafisha baadhi ya watu kwa kuwaleta kwa mashtaka mepesi alimradi tu wamefikishwa mahakamani kwa mbwembwe zote" amesema mdokezaji wetu toka ofisi ya Mwanasheria Mkuu mwenye kujua mpango ulioko mbeleni.