Exclusive interview with Mohammed Dewji

Mhe. Dewji, unaweza kuwahakakikishia Watanzania kama mali yako yote umeipata kihalali?
 
Mh. Dewji...maswali ni haya yafuatayo:

1. We umezaliwa kwenye familia yenye nafuu na umiliki wa mali,lakini kwanini uliamua kugombea ubunge? Kwani bila ubunge ungeshindwa kutoa misaada?

2. Je ni kweli upo kambi ya Lowassa ambayo ni maandalizi ya mbio za urais 2015?

3. Kwanini huwa hutoi michango sana bungeni na Mara nyingi nimekuona ukipiga tu meza?
 
Mh. Dewji!

Kutokana na kashfa ya mkopo wa mafuta kutoka Libya kampuni yako ilitaka kuingilia na hatimae kunufaika na dola za marekani 121.9 Millioni sawa na TSH 180 Billioni. Ilikuwaje mjasiliamali mmoja (ambaye ni wewe) kuingia katika Transactions baina ya nchi mbili? Na baada ya ubalozi wa Libya Tanzania kukana makubaliano yoyote kati ya MeTL na serikali yao ulichukua hatua gani?

Kama hukuchukua hatua basi ile dhana ya kuliibia Taifa kwa mtindo wa EPA umekua kinara kupitia Massoud Mohamed Nassr ambae pia anahusika na MeTL.


Msingi wa swali:
 
Nina maswali kadhaa kuelekea uendeshaji wa kampuni za Mohamed Dewji:

1..Je,anajua kwamba kwenye pale Head Office-Morogoro Road kuna kuna vyoo vya aina mbili,kuna kimoja kichafu kipo ground floor ambacho wanatumia watu weusi na vingine visafi ambavyo vinatumiwa na wahindi? Hata funguo kuna mbili ile ya wahindi hauwezi kupata mtanzania.Ubaguzi uliokithiri,Je amehalalisha 'Apatheid Policy' kwenye makampuni yake?

2..Je anajua kwamba baadhi ya kampuni zake zinakwepa kwa makusudi kuwalipia wafanyakazi wake ule mchango wa mifuko ya kijamii kama NSSF?

3..Je,anajua kwamba wafanyakazi hasa watanzania wanalipwa mishahara kupitia payment vouchers na pia mshahara karibia nusu unaandikwa kuwa allowance hewa ili kukwepa kuchangia kiasi stahili kwa wafanyakazi wake kwenye mifuko ya kijamii?

4..Je,ana mpango gani na yale mashamba makubwa(Mfano...Alavi sisal estate la Kibaha approx. 6000Ha) ambayo hayafanyii lolote na wala hawekezi kitu badala yake ananyonya kilichopo tu na kushindwa kabisa kuyaendeleza?Mikopo aliyochukua kwenye mabenki kwa kutumia yale mashamba amepeleka wapi?

5..Mheshimiwa Mohamed Dewji anajiita mtanzania mwenzetu lakini kwa nini amejaza wahindi huku akiwalipa mishahara hadi mara tatu ya ile wanayolipwa watanzania katika ngazi zile zile za kiutendaji?

6..Je, anajua kwamba wafanyakazi watanzania wananyimwa likizo kwa wakati kwa kuzungushwa saaaana wakati wahindi wanapewa ruhusu za kwenda likizo zilizogharamiwa na kampuni?

Naomba atoe majibu yenye kueleweka kuhusu haya mambo.
 
Sijui kama swali hili ninalielekeza kwa a "right person"

Endapo kama navyodhani, kampuni yake ndo ya kwanza kuanza kuingiza nguo za "mtumba" for business; Je, Mhe. haoni kwamba kampuni yake imechangia kuuwa uwezekano wa kuwa na viwanda vya nguo? Je hilo haliwezi kuwa limeipatia nchi hasara ya kiuchumi?
 
beahunja

Mkuu, Mbona maswali mengi namna hii, kama ukiombwa uchague swali moja tu katika haya ambalo aulizwe ili kutoa nafsi kwa maswali ya waulizaji wengine ungechagua swali gani?
 
Last edited by a moderator:

Ikiwezekana itabidi aje japo na Chief Accountant pamoja na HR Manager wake naona.
 
Swali la Mwisho:

Anajisikiaje kuwa na utajiri mkubwa katikati ya watu masikini sana, akitaka kutoa majibu ya jumla sawa, akionyesha kusita muambie achague jibu kati ya haya;
(a) Masikini wote ni kwa sababu ya kujitakia kwao
(b) Anaona Fahari na anajisifu kwa mafanikio yake
(c) Hajawahi kufikiria kitu kama hicho
(d) Ni Mapenzi ya Mungu kuchagua wachache awapendao na kuwapa mazuri yote ya dunia hii.
(e) It is non of his business
 
1. Katika kampeni 2010 aliahidi kuweka nyasi uwanja wa namfua tena mbele ya Rais na hajatekeleza hadi leo je ilikua ni danganya toto??

2. Atumbie ni kiasi gani amekusanya toka kwa wahisani wa nje kupitia mfuko wa Singida yetu na kwanini amekua akificha hilo na kujidai kuwa miradi yote inaendeswa kwa fedha zake bila kuwataja wafadhili hao kitendo kilicho sababisha wajitoe??

3. Kwanini ameshindwa kuwajengea uwezo wananchi kwa kuwekeza jimboni kwake badala yake anawekeza zaidi mikoa mingine?? Haoni sasa wakati umefika wa yeye kugombea huko alikowekeza zaidi??

4. Kwanini yeye kama mbunge ameshindwa kuonyesha mfano kwa wakazi wa singida kwa kujenga nyumba ya kisasa jimboni kwake na badala yake amekua akiishi gest kama mgeni??

5. Kwanini muda mwingi haonekani jmboni wala bungeni? Na inapotokea unashida na mbunge hatujui pa kumpata na hata ukienda ofisini hupati ushirikiano wa kutosha kwani katibu wake nae muda mwingi anakua kwenye miradi yake binafsi.

6. Kwa matatizo haya kwnini asitangaze rasmi kustaafu ubunge kabla hatujamwajibisha??

7. Kwanini baada ya uchaguzi aliwaita wasimamizi wa uchaguzi na kuwapa hela SH. elfu 50 kila mmoja je ilikua ni malipo ya kazi aliyowatuma ya kumsaidia kuba kura??

8. Mradi wake wa kuweka nyasi uwanjani utakapokamilika utamfaidisha nani? Maana mkoa hauna timu na hata uwanja haujakamilika na yeye alisaidia kuhujumu timu yetu ya Singida United na kuihamishia Dar na kisha kuiua kwa alichodai inamtia hasara je nani alimwambia sisi tuliianzisha ili tupate faida badala ya burudani?
 
Pia muulize anaifahamu au alishawahi kuitembela JF? Kama ni ndiyo nini maoni yake kuhusu JF? Kama siyo anaweza kuja kuitembelea na kujibu maswali ya wananchi na wakazi wa Jimbo lake bila kusubiri tena "Makutano?"
 
Ikiwezekana itabidi aje japo na Chief Accountant pamoja na HR Manager wake naona.
Yes good idea itakuwa vizuri akija na hao watu pamoja na mmoja wa directors ambaye anaweza kutueleza japo kwa dondoo strategic direction ya MeTL.

-Huyo HR anapaswa ajibu kwa nini watu walioajiriwa hawapewi mikataba yao kila siku wanapigwa tarehe tu.
 
Kuna video clip moja naiona kituo flani cha TV akishangilia huku akiwa kifua wazi. Je, kwa hadhi yake ya ubunge haoni kuwa ile kitu inamdhalilisha? Je, ndio aina yake ya ushangiliaji kila anapofurahi?
 

Your company has been fairly successful as one of the first Tanzanian multinational companies.
What are some of the lessons that you can share with others in the private sector that seek to venture across our borders?
 
Mohamed Dewji wakati anagombea ubunge kwa mara ya kwanza, alishinda kwenye kura za maoni, ambapo mwenzake Musa Nkhangaa alilalamika kuwa Dewji alitoa rushwa ya unga kwa wapiga kura, matokeo yaliyotengua ushindi wake, na mshindi wa tatu akawa ndiye mgombea na kuwa mbunge.

Nakumbuka wakati anatenguliwa ushindi, kigezo alichotumia mwenyekiti wa ccm wakati ule Benjamin Mkapa ilikuwa ni kwamba Dewji bado ni kijana, na hajakomaa kisiasa. Dewji kwa hasira akasema ili Mkapa ajue nimekomaa kisiasa, atamalizia kuijenga ofisi ya ccm ambayo ilianza kujengwa tokea 1975.

Swali:
Ni vipi ile ofisi ambayo ilikuwa ghorofa moja tayari ameshaijenga kwa muda wote ambao ameshakuwa mbunge?
 
Aelezee sakata la pesa za walibya kujenga kiwanda cha cement,jinsi membe alivyofisadi pesa asiogope!
 
Swali

Kwanini makampuni yake yote yanatoa ajira kwa raia wengi wa kigeni hasa India na Pakistan? Ina maana waTanzania wazawa [weusi] hawana ujuzi wa kutosha au Mohamed Dewji ana vile vidharau vya wahindi walivyonavyo dhidi ya waTanzania?

Hili namjibia:

Kwa sababu:

Wafanya kazi wa Kitanzania wengi ni wavivu, wezi, waongo, hawaishi kufiwa na kuomba ruksa za kwenda kuzika, hawaishi kuumwa, hawaishi kuwa na kila sababu za kutokuhudhuria kazini. Watu wa India wanajuwa dhiki ya maisha na vipi kupata kazi ni kugumu na wao huchapa kazi na hawana visingizio kama Watanzania.

Inapaswa Watanzania wanaotaka maendeleo ya haraka wabadilike.

Oops, nilisahau:

Hawaishi kukopa (kujichotea) makazini, hata iwe ni viongozi wa vyama vya siasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…