Exclusive Interview na Mheshimiwa Mathias Chikawe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Exclusive Interview na Mheshimiwa Mathias Chikawe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Makutano Show, Aug 30, 2012.

 1. Makutano Show

  Makutano Show Verified User

  #1
  Aug 30, 2012
  Joined: Aug 3, 2012
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jumamosi katika kipindi cha Makutano nitakuwa na Mbunge wa Nachingwea ambaye pia ni Waziri wa Sheria na Katiba Mheshimiwa Mathias Chikawe tukiongea mambo mbalimbali ikiwemo suala la Katiba mpya.

  Mheshimiwa Waziri anataka kupokea maswali na maoni toka JF, unakaribishwa kuuliza na yatamfikia. Pia usikose kusikiliza akihojiwa Jumamosi kuanzia saa tisa mchana Magic FM 92.9 Dar, 93.3 Dodoma, 98.6 Arusha/Moshi,101.7Mwanza na online kupitia MakutanoShow on USTREAM: Makutano na Fina Mango..

  Karibu

  Wana-JF

  Mahojiano na Mheshimiwa Chikawe kwa Jumamosi hii yameahirishwa kutokana na kupata dharula hivyo kusafiri kikazi. Tunawaomba radhi kwa hilo badala yake atakuwepo mheshimiwa Basil Pesambili Mramba waziri wa zamani wa Fedha.

  Mahojiano yake yatakuwepo hapa baada ya kipindi.
   
 2. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #2
  Aug 30, 2012
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Dada jitahidi kutuletea viongozi watakao tupeleka mbele na siyo wanaotuhujumu sasa na wanaturudisha nyuma. hilo ni ombi langu tu na sina swali kwa huyo bwana.
   
 3. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #3
  Aug 30, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,943
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  Fina tunashukuru hata kwa karibisho wa Mathias chikawe katika kipindi chako.

  Nina swali moja tu kwake; Kama waziri wa katiba na sheria, yeye akiwa kama waziri amewahi kufikiri kufanya marekebisho ya sheria za wabadhirifu na wala rushwa hasa kwenye kipengele cha adhabu wanazopewa?

  Pia swali naloweza ongeza ni kwanini sheria kama ile ya rushwa haiipi TAKUKURU mamlaka halisi yaani yamefichwa chini ya uchunguzi wa DPP?
   
 4. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #4
  Aug 30, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  Unajuaje yupi anatupeleka mbele ? muache dada afanye kazi yake

  support her kwa kupendekeza majina sio comments za juu juu tu
   
 5. Marire

  Marire JF-Expert Member

  #5
  Aug 30, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 11,420
  Likes Received: 259
  Trophy Points: 180
  Muulize yeye ana maoni gani kutokana na wananchi na hata bungeni tumesikia wakipendekeza sheria kama za China kwa mafisidi kunyongwa hadharani endapo wanakutwa na hatia.

  Nina pendekezo pia kuwa tunaomba uite na viongozi wa Upinzani pindi upatapo nafasi ili tuweze kupata nafasi ya kutoa maswali dhidi yao.
   
 6. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #6
  Aug 30, 2012
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Maswali
  1. Je amejisikiajee kusikia na kusoma ushahidi uliotolewa na Mh Tundu Lissu kuhusu shutuma zake dhidi ya Uteuzi wa Majaji katika mahakama hapa nchini Tanzania?

  2. Kama waziri wa sheria anaguswa vipi na sheria zinazochochea kasi ya umaskini nchini kama ile ya zuio la maandamano''inayobakwa na Jeshi la Polisi kwa kisingizio cha sababu za usalama ili hali ikiwa ni maelekezo ya kulinda chama tawala na watawala wake?
   
 7. Tungaraza Jr

  Tungaraza Jr Senior Member

  #7
  Aug 30, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 196
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mh. Chikawe, kwa maoni yako wewe unadhani tume ya Katiba iko huru na hakuna shinikizo la viongozi hasa katika maoni yanayohusu madaraka ya Raisi na utawala wa sheria kwa kua kwa sasa tunaona madudu mengi bungeni?

  Kwa mfano: Kinachotakiwa kutojadiliwa sehemu nyingine ni maamuzi yatolewayo na mahakama na si kesi iliyopelekwa mahakamani, ila nashangaa viongozi wa CCM na serikali swala hili limekua kimbilio la maovu yenu.
   
 8. mgen

  mgen JF-Expert Member

  #8
  Aug 30, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 15,148
  Likes Received: 1,882
  Trophy Points: 280
  Maoni yangu ni tunataka Mkutano wa Katiba. Kama ni katiba mpya sisi wananchi tunataka Mkutano wa katiba ili tuweze kutoa maoni yetu kama vile juu ya masharti muajiri ili tukatae ama kukubali nini muajiri afanye/asifanye! Hio inakuwa kwa maslahi uma na sio mwajiriwa ama mwajiri.
   
 9. sembuli

  sembuli JF-Expert Member

  #9
  Aug 30, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 762
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Mh nina maswali matatu rahisi.

  1: ukiwa kama mbunge wa jimbo la nachingwea ,umefanikiwa vp kutekeleza ahadi zako ulizoahidi ktk uchaguzi wa mwaka 2010

  2(a): unakabiliana vp na changamoto ya kuongezeka kwa idadi wanafunzi wa kike wanaopata ujauzito na kukatiza masomo ktk shule za msingi jimboni kwako?

  2(b): mh rais Jk aliwahi kunukuliwa akisema kuwa "ujauzito kwa wanafunzi wa msingi ni kiherehere chao". Je,nini maoni yako juu ya kauli hii?

  3: ukiwa kama waziri wa sheria, Je ni lini tatizo la uchakavu wa majengo ya mahakama za mwanzo litaisha? mfano ni jengo la mahakama ya mwanzo dodoma mjini, mahakama ya mwanzo mvumi-makulu wilayani chamwino, mahakama ya mwanzo chamwino-ikulu wilaya ya chamwino DODOMA. Licha ya uchakavu pia posho za wazee wa baraza hazilipwi kwa wakati .
   
 10. Kiganyi

  Kiganyi JF-Expert Member

  #10
  Aug 30, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 1,244
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  MODS mmefuta ujumbe wangu kwa Makutano show katika thread hii!

  Acheni Ubeberu!!
   
 11. K

  Kiranja JF-Expert Member

  #11
  Aug 30, 2012
  Joined: May 19, 2007
  Messages: 754
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Muulize kuhusu habari ya mwanahalisi kuhusu yeye kwa kushirikiana na wafanyabiashara wa Afrika ya kusini kuanzisha kiwanda cha ARVs amefikia wapi?

  Pili, kuhusu korosho , kwanini wananchi wanakosa sulphur kwa ajili ya mikorosho yao na yeye yuko kimya? pia anamsimamo gani kuhusu viwanda vya korosho?
   
 12. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #12
  Aug 30, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Je ilikuwaje mtu asiyekuwa na shahada ya sheria akateuliwa kuwa jaji wa mahakama ya rufaa?
   
 13. Wamunzengo

  Wamunzengo JF-Expert Member

  #13
  Aug 31, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 810
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  Fina, binafsi nina maswali mengi saana, lakini nikikumbuka jamaa alivyokuwa anajibu kwa kiburi hoja za wabunge siku anahitimisha mjadala wa makadirio ya bajeti ya wizara yake, napata hasira sana. kwa kifupi Fina hawa jamaa wa ccm hata ukiwauliza maswali, wanajibu kisanii tu, halafu wanavyotaka wao. swali nyeti, zito, lenye mantiki, halafu jamaa atakujibu ooh! ndo tupo kwenye mchakato, mara tutalifanyia kazi, mara maoni tumeyapokea, yaani upuuzi upuuzi tu. Hivi ccm, wanadhani sisi watanzania ni mali yao?? hakyanani we ngoja tu, lazima waipate hapa hapa duniani. wanajineemesha wao, tu utadhani Tanzani ni ya wabunge, baraza la mwaziri na rais peke yao. wanatia hasira sana hawa jamaa.  Tuendeleeni kuwaelimisha watanzania, waelimike ili tuliondoe madarakani hili li serikali la ccm magamba/mafisadi/majambazi/wauaji.
   
 14. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #14
  Aug 31, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Huyu hana jipya..hawa ni wale wale wastaafu akina Chibulunje.kipindi hakitakuwa na mvuto coz hawana majibu yenye tija zaidi ya kutetea matumbo yao.
   
 15. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #15
  Aug 31, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,210
  Likes Received: 3,774
  Trophy Points: 280
  Naomba niulize maswali yangu mawili mapema, kwakuwa sijui kama nitabahatika kuungana nanyi hapa siku ya j1:

  1. Kwa uzoefu wangu wakufuatilia nakujua mifumo ya uundaji katiba ktk baadhi ya mataifa ambayo sisi hupenda kuakisi ni kuwa, katiba hutengenezwa na chombo kiitwacho BARAZA LA KATIBA, Je Mh waziri, mfumo wetu wakutumia TUME unatuaminishaje kuwa tume hii itatuletea Katiba ya kiraia/umma?

  2. Kwamujibu wa sheria ya kutunga katiba mpya iliyosainiwa kabla ya uundwaji wa tume husika, moja ya mambo muhimu inampa rais wa nchi mamlaka ya:

  (a). Kuteua tume ya katiba, (b). Hadidu za rejea zitapelekwa kwake, (c). Atakaa na rais wa Zanzibar nakuamua kuitisha kura ya maoni.

  Kwakuzingatia sheria hiyohiyo, Je inampa rais wa nchi mamlaka kupendekeza na kuingiza mawazo/matakwa yake kwa ukomo gani? na nani anasimamia uingizaji wa mawazo hayo ya rais wa nchi kwenye mchakato huu wa katiba?
   
 16. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #16
  Aug 31, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Rais wa JMT...in waiting
   
 17. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #17
  Aug 31, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  Muulize chikawe:
  je ni kosa wananchi kuunga mkono, kushabikia vyama vya siasa;

  kwa mujibu wa sheria za nchi yetu, ni kosa gani ambalo ni kubwa zaidi kuliko mengine na ni nini hukumu ya hilo/hayo kosa/makosa.

  Morogoro wananchi walidaiwa kukaidi maelekezo ya polisi kuhusu maandamano, kanuni za jeshi zinasema nini kuhusu matumizi ya silaha za moto kwa waandamanaji wasio na silaha, kufanya vurugu wala kuhatarisha usalama wa mali na maisha?

  Kwa nini kila linapohusika jeshi kudai kulinda na kusimamia sheria hasa za vyama vya siasa ndipo nguvu zao husababisha maafa, na hawachukui hatua zipaswazo kuchukuliwa kwa wakiukaji wa taratibu za kazi zao.

  Kwanini wizara ya sheria na katiba inaogopa ccm kupoteza dola.
   
 18. TinyMonster

  TinyMonster JF-Expert Member

  #18
  Sep 1, 2012
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 235
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Tunaruhusiwa kumuuliza swali mheshimiwa Mramba?
   
Loading...