Exclusive interview with Mohammed Dewji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Exclusive interview with Mohammed Dewji

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Makutano Show, Aug 9, 2012.

 1. Makutano Show

  Makutano Show Verified User

  #1
  Aug 9, 2012
  Joined: Aug 3, 2012
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Katika kipindi cha Makutano Jumamosi ijayo mgeni atakaeongea na Fina Mango ni mbunge wa Singida Mjini Mheshimiwa Mohammed Dewji atakaeongea masuala mbalimbali ikiwepo maisha yake binafsi, ya kisiasa na kibiashara.

  Kama una swali lolote ambalo ungependa Mheshimiwa Dewji alijibu tafadhali uliza na litasomwa hewani siku ya kipindi kuanzia saa tisa mchana kupitia 92.9FM Dar, 93.3FM Dodoma, 98.6FM Arusha/Moshi, 101.7FM Dodoma.

  Karibu
   
 2. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #2
  Aug 9, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Kwakuwa ni mkereketwa wa michezo ni kwanini asianzise team chini ya kampuni yake or yeye binafsi ya mpira kama ilivyofanya Bakhresa na Azam FC?
   
 3. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #3
  Aug 9, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  1. Kwanini kampuni yake ni notorius ya kuingiza vyakula ambavyo havifai kwa matumizi ya binadamu?
  2. Yeye kama mfanyabiashara na Mbunge wa Singida kwanini asifungue kiwanda cha mafuta ya alizeti ili kuwasaidia wapiga kura wake wa Singida wanaohangaika na zao la alizeti ambalo halina soko la uhakika? Na pia atasaidia kupunguza tatizo la ajira kwa wapiga kura wake.
  3. Kampuni yake Metl imeajiri WAPAKISTANI na WAHINDI wangapi? Je hao Wapakistani na wahindi wanafanya kazi gani amabazo haziwezi kufanywa na Watanzania?
   
 4. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #4
  Aug 9, 2012
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,891
  Likes Received: 6,085
  Trophy Points: 280
  Kwanza tuwashukuru sana kwa kutambua umuhimu wa JF katika kufanikisha kipindi chenu.

  Tatizo ukija hapa ujue wazi unakutana na Great Thinkers na kwa maana hiyo jitahidi kuwahost watu wenye upeo na uelewa wa mambo na walio wasafi kimaadili.

  ...Fina Mango hadhi yako itapanda na utaingia kwenye kundi la 'wapiganaji'.

  Mimi swali langu ni hili:
  Hicho kiwanja cha serikali kilichopo barabara ya Nyerere ambacho kilisemekana aliuziwa na aliyekuwa waziri wa fedha (Mkullo) alitumia njia halali kukipata au ali-tresspass?

  Na kama alitumia njia ya mkato, haoni ni busara kukirudisha ili kujiweka katika sehemu sahihi ya histori ya UFISADI Tanzania?
   
 5. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #5
  Aug 9, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Swali

  Kwanini makampuni yake yote yanatoa ajira kwa raia wengi wa kigeni hasa India na Pakistan? Ina maana waTanzania wazawa [weusi] hawana ujuzi wa kutosha au Mohamed Dewji ana vile vidharau vya wahindi walivyonavyo dhidi ya waTanzania?
   
 6. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #6
  Aug 9, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Fina, muulize huyu mheshimiwa kuwa analionaje lile wazo lililowahi kuzungumzwa na Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete la kutenganisha SIASA na BIASHARA?

  Kwa upande wa michezo muulize kwa nini yeye kama mbunge anaonaje kama atapeleka muswada bungeni wa kuanzisha 'soka ya kulipwa' hapa nchini ili wachezaji wa kitanzania walipwe kama hao wanaojiita 'maproo'..

  Swali la mwisho; Anaielewaje dhana nzima ya CSR (Corporate Social Responsibility)? Na kama anaifahamu ameitekelezaje kupitia kampuni yake ya Mohammed Enterprises!?
   
 7. K

  Kiguu na njia Member

  #7
  Aug 9, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 95
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Alishaanzisha African Leone ila imemshinda...!!
   
 8. e

  ebaeban JF-Expert Member

  #8
  Aug 9, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 1,834
  Likes Received: 600
  Trophy Points: 280
  Swali la 1:
  Kwanini anatoa misaada sana ya kijamii jimboni Sindida halafu anahusishwa na ufisadi chini ya kivuli cha kampuni yake ya Mohamed Enterprises kwa kununua kiwanja cha iliyokuwa GAPEX hapo nyerere RD kwa bei poa? Je, anatumia misaada hiyo kama kinga asibughuziwe na vyama husika?

  SWALI 2:

  YEYE na wenzie kama RAGE enzi za Nyerere walikuwa wanaomba uongozi walikuwa wanafukuzwa; Je, BAADA ya baba wa taifa kufariki kwanini wameingia chama cha CCM?
   
 9. Ben Mugashe

  Ben Mugashe Verified User

  #9
  Aug 9, 2012
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 940
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Swali:
  Je na yeye anachukua POSHO? aoni angeipeleka kwenye mfuko wa Jimbo kuwasaidia? au kwa watoto yatima?
   
 10. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #10
  Aug 9, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Niulizie maswali haya:

  Swali la Kwanza
  Kwasababu kumekuwa na vijimaneno vingi vyenye kubeba ujumbe kwamba Anaendesha biashara zake kwa ukwepaji mkubwa wa kodi, Je, anaweza kujisafisha kwa kuchagua Kampuni binafsi ya Uhasibu kutoka kwenye the Big Five Auditing Firms wamfanyie Tax Health check na awaelekeze kuiweka report hiyo Public, ili kuziba watu mdomo?

  Swali la Pili
  Inasemekana kwamba na Yeye ni mmoja wa wanufaika wa sera ya Ubinafsishaji wakati wa utawala wa Ben Nkapa, na inasemakana kwamba Viwanda vingi alivyobinafsishiwa hivi sasa vimekufa kabisa tofauti ni pale alipovichukua.

  Je:
  (i) Anaweza akaweka wazi alinunua viwanda na mashamba mangapi?
  (ii) Je kama zingekuwa mali zake, kwa wakati huo, angeuza viwanda na mashamba aliyonunua kwa bei aliyouziwa yeye?
  (iii) Ni nini hasa hali halisi ya viwanda na mashamba aliyonunua kwa sasa?
  (iv) Kama jibu lake katika kipengele cha (iii) kitaonyesha hali ya viwanda na mashamba hayo ni mbovu kuliko wakati anauziwa, Je yuko tayari kuvirudisha serikalini at least kwa bei aliyonunulia?
   
 11. Sooth

  Sooth JF-Expert Member

  #11
  Aug 9, 2012
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 3,773
  Likes Received: 4,496
  Trophy Points: 280
  Kuna wakati aliwahi kuwakusanya walimu wa jimboni kwake na kuzungumza nao. Baada ya kikao aliwapatia t-shirt na fedha taslimu Tsh. 50,000/ (elfu hamsini).

  Swali:

  1. Inakuwaje anakuwa na moyo wa kuwapa pesa walimu lakini hawezi kuwatetea bungeni na kwenye chama chake ili waweze kupata mishahara itakayokidhi mahitaji yao ya msingi?
  NB: Sijawahi kumsikia akitetea walimu bungeni au hadharani. Pia sikumsikia ktk mgogoro wa walimu wa hivi karibuni.

  2. Haoni kwamba kwa kuwapa walimu pesa, anaenda kinyume na utamaduni wa kujitegemea na hivyo kuwafanya wananchi wawaone wabunge kama watu tajiri wenye fuko la pesa za kugawa kwa kila mtu? Ana pesa ya kumpa kila mpiga kura wake kila atakapohitaji?
   
 12. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #12
  Aug 9, 2012
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kampuni yake ya Mohamed Enterprise kwa mwaka uliopita imelipa kodi kiasi gani? Na mapato yake yalikuwa ni kiasi gani?

  Haya ni maswali ambayo tunatumaini utampelekea kabla na inabidi aje na fact. Itakuwa aibu kwakwe na wewe mtangazaji pale atakaposema hana data wakati maswali yapo kwenye public forum.

  Pamoja na kuwa ulitoka kule hatutegemei kuwa ulibeba na madudu yao!
   
 13. K

  Kevin.A Member

  #13
  Aug 9, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Fina,

  Ninaweza kusikiliza hiki kipindi live online? Kama ndio, naomba link.
   
 14. Kivumah

  Kivumah JF-Expert Member

  #14
  Aug 9, 2012
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 2,413
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  ..Mohamed Dewji mnamo mwezi Machi mwaka huu alishinda tuzo na kutangazwa na Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF) kuwa kiongozi bora mwenye umri mdogo Duniani(Young Global Leader) akiwa ni Mtanzania pekee!

  • Je, anafikiri ni kwanini yeye ndie ashinde?,
  • Je, ushindi huo ameutumiaje kushawishi vijana wa kitanzania kama yeye kufikia hatua aliyofikia akizingatia vijana wengi wanaotoka vyuoni sasa hivi wana dhana ya kuajiriwa badala ya kujiajiri?
   
 15. Ibambasi

  Ibambasi JF-Expert Member

  #15
  Aug 9, 2012
  Joined: Jul 25, 2007
  Messages: 6,659
  Likes Received: 2,465
  Trophy Points: 280
  Amesikia taarifa za yeye kushirikiana na Mwigulu Nchemba kumuundia "zengwe" Kitila Mkumbo ili asigombee ubunge 2015 hukoa Iramba kwa Nchemba? Nini maoni yake na kwa nini yeye ahusishwe?
   
 16. FortJeasus

  FortJeasus JF-Expert Member

  #16
  Aug 9, 2012
  Joined: Jan 19, 2012
  Messages: 568
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Moja, ningependa umuulize anatarajia lini kustaafu siasa? Halafu anaionaje kasi ya CHADEMA jimboni kwake? Na nini ni mwitikio wake?

  Pili, baadhi ya wananchi wa SINGIDA Mjini wanaulizia kuhusu ahadi ya nyasi za bandia alizoahidi kuweka katika uwanja wa Namfua!!

  Muulize, hata hivyo, kama kweli nyasi za uwanjani ndio vipaumbele vya wakazi wa jimboni kwake!!

  Muulize kwanini katibu wake jimboni, bwana Mazala ana mali na biashara nyingi ambazo uhalali wake unatiliwa mashaka?
   
 17. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #17
  Aug 9, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Naona maswali niliyotaka kuuliza yameshawekwa. Nitasikiliza kipindi kama nitakuwa na la nyongeza nitauliza!
   
 18. b

  beahunja Member

  #18
  Aug 9, 2012
  Joined: Feb 6, 2010
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  1. Kwa nini kiwanda chako kinatengeneza magunia chini ya kiwango kwa ajili ya export mpaka kuathiri biashara za mazao kama kahawa?

  2. Fedha za mfuko gani sijui ila ilihusika suala la LIBYA siku hiyo ambazo Waziri Membe aliziomba kupitia kampuni kujenga kiwanda cha saruji LINDI unazimendea kwa nini? Mbona mabenki yapo mengi, za bure au ndio riba hipo chini?

  3. Mchango wako katika soka unajulikana na kutambuliwa na kila mwanajamii lakini timu yako kuwa mshirika na Simba nini maana yake? au nyie ni washiriki na sio washindani?

  4. Tunatambua uwezo wako wa kifedha usingehitaji tuposho na mikopo ya gari, kwanini unaangahika na ubunge au ndio kulinda maslahi yako katika mhimili huo?

  5. Je, umechukua mkopo wa ubunge kwa ajili ya kununua gari? Kama jibu ndio, umenunua gari aina gani? Kwa hadhi yako na uwezo wa kiuchumi ulio nao ulikuwa na sababu gani au ulazima wowote wa kuchukua huo mkopo?

  6. Pamoja na kuhamasisha maendeleo na utekelezaji wa shughuli za kimaendeleo na miradi jimboni kwako, Je ni jambo la busara wabunge wa mikoani kukimbilia Dar es Salaam? Mnafuata nini huko ambacho hakipo huku mikoani? Je mmetimiza wajibu zenu ipasavyo kwa wananchi waliokuamini?

  7. Suala la viongozi waandamizi wa chama chako na serikali yake kushindwa kutekeleza ahadi zao ndogo sambamba na mara kwa mara kushindwa kuwataja wahujumu uchumi na wezi wa mali za umma japo walitamka wanawajua unaliongeleaje?

  Kitendo cha kukataa kuwataja pindi umma ukitaka kujulishwa ni sera ya chama kulinda waovu? Wewe haupo katika makundi hayo (wezi na wahujumu) ambayo mara kwa mara hawatajwi?

  8. Huduma muhimu za kibinadamu hazipatikani nchini kwetu, tumekuwa tukishuhudia watu maarufu, wabunge na viongozi wa serikali wakienda kutibiwa nje ya nchi ( mfano Kapt. Komba alienda kuchekiwa miguu nje India). Unaweza kuwaambia watanzania maskini na hasa waliopo jimboni kwako kuwa hii nchi ni ya HAKI na USAWA kuwa kodi zinafanyakazi kwa ajili yao?

  9. Ni nini mtizamo wako hali ya maisha kwa sasa kwa watanzania (kupanda bei kwa bidhaa muhimu na kuanguka kwa bei kwa mazao kama pamba,korosho na kahawa), hali ya kisiasa, migomo ya watendaji wa sekta nyeti serikalini. unajua sababu ya hao yote?

  10. Wewe binafsi umewahi kupata upendeleo kutoka kwa serikali katika kujipatia nafasi za kupata fedha, mali au utajiri?
   
 19. Wamunzengo

  Wamunzengo JF-Expert Member

  #19
  Aug 9, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 810
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  Kabla hajajibu haya maswali, mwambie kwanza amkumbuke Mwenyezi Mungu asije akadanganya!

  Maswali yangu ni kwamba;
  • Je, katika uchaguzi uliompa ridhaa ya ubunge, alihonga kiasi gani kwenye chama ili apate ugombea na aliwahonga kiasi gani wananchi ili wamchague?
  • Je chama chake na serikali yake wamefikia hatua gani katika kufuatilia pesa zilizotajwa na mabenki ya kule uswis hivi karibuni?
  • Hivi anadhani CCM na serikali yake ina nia ya dhati kweli kupambana na rushwa na ufisadi hapa nchini?
   
 20. Mjomba wa taifa

  Mjomba wa taifa JF-Expert Member

  #20
  Aug 9, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 232
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Namuuliza Mo maswali yafuatayo?

  1. Kwanini Kampuni zake hazilipii wafanyakazi wake Pensheni (NSSF/PPF)?
  2. Mgogoro wa Godown alilolipora National Housing na kushtukiwa na Mchechu limeishia wapi? maana siku ile ya ubomoaji aliomba msaada kwa JK kusitisha ubomoaji but Mchechu akaziba masikio na kusema Liwalo na liwe.
   
Loading...